Tangazo

March 31, 2012

KAMPENI ZA CCM ENEO LA PATANDI, TENGERU ARUMERU MASHARIKI

Wananchi wakisoma toleo maalum la uhuru.

MZEE MKAPA AMNADI SIOI - TENGERU

Mkapa akihutubia mkutano wa kampeni eneo la Patandi, Tengeru Machi 30.12.

Umati wa watu wakimsikiliza Mkapa kwenye mkutano wa Patandoi, Tengeru.

Mkapa akimnadi Sioi mkutano wa Patandi Tengeru.

NHIF yazidi kusonga mbele, sasa yakutana na wadau Kagera

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emmanuel Humba akitoa maelezo ya utangulizi kwa wadau.

Mjumbe wa Bodi ya NHIF, Prof. Joseph Shija akitoa salaam za bodi kwa wadau wa Mfuko huo.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NHIF, Eugen Mikongoti na Mkurugenzi wa Takwimu na Utafiri, Michael Mhando wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa.

JESHI LA POLISI KUBORESHWA ILI KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI: SERIKALI

IGP Said Mwema
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi - Moshi

Serikali imeahidi kuendelea kuliboresha Jeshi la Polisi ili liweze kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi katika maeneo mbalimbali.
Hayo yamesemwa jana mjini Moshi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mh. Mbara Abduluwakili wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa Askari wapya wa Jeshi la Polisi yaliyokuwa yakifanyika kwenye Chuo cha Taaluma ya Jeshi la Polisi Moshi (Moshi Police Academy).

Mh. Abduluwakili amesema kutokana na mabadiliko ya Kisayansi, hali ya uhali ya uhalifu nayo imekuwa ikibadilika kutokana na mazingira hayo na hivyo aina na mbinu za uhalifu nazo zimebadilika na hakuna budi sasa kwa Jeshi la Polisi nalo likabadilika kimbinu na kujiongezea ujuzi zaidi ili kuwashinda wahalifu.

Amesema pamoja na changamoto hizo, lakini kwa siku za hivi karibuni, Jeshi la Polisi limeweza kupata mafanikio makubwa katika Nyanja mbalimbali hasa kwenye suala la kupambana na wahalifu wakiwemo wakorofi na wale wanaotumia silaha za moto na hata kuwashinda na kuwatia nguvuni.

Amesema hivi sasa hata takwimu za makosa ya Jinai yanayoripotiwa katika vituo mbalimbali vya Polisi yamepungua hali inayoonyesha kuwa hali ya uhalifu nayo imepungua kwa kiasi kikubwa.

Amepongeza juhudi zinazofanywa na makamanda wa Polisi wa Mikoa chini ya Uongozi wa Mkuu wa Jeshi hilo Inspekta Jenerali Saidi Mwema katika kuhakikisha kuwa hali inazidi kuwa salama na utuliu kuongezeka siku hadi siku.

Kuhuusiana na ajali za barabarani, Mh. Abdulwakili, amewata Polisi kuhakikisha kuwa wanaendeleza juhudi zao za kupambana na madereva wakorofi na hata ikiwezekana kuwanyang’anya leseni kwa madereva na kuyaondoa barabarani magari mabovu ili kuepusha ongezeko la ajali.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta  Jenerali Saidi Mwema,  amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga ili kuhakikisha kuwa uchaguzi mdogo katika Jimbo la Arumeru Mashariki na chaguzi nyingine ndogondogo kwa nafasi za udiwani hapa nchini zinafanyika kwa amani na utulivu.

Amewataka wananchi waliopo kwenye maeneo ya upigaji kura waweze kupiga kura zao na kurudi majumbani kusubiri matokeo na kuepuka kufanya vurugu kwani kwa kufanya hivyo watalilazimisha Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua za kisheria.

Akizungumzia kazi inayowakabili askari hao wapya, Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Saidi Mwema amesema kuwa kazi ya Polisi ni kuhakikisha kuwa inapambana na changamoto mbalimbali na amewataka kuzigeuza changamoto hizo ili ziwe ni fursa ya kutumia rasilimali chache zilizopo kwa kuleta mafaniko ya kiutendaji kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Awali akitoa taarifa ya Mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi cha Moshi ACP Matanga Mbushi, amesema kuwa pamoja na mambo mengine, wahiitimu hao wamejifunza kazi za Polisi, utoaji wa huduma bora kwa mteja anayefika katika kituo cha Polisi, Polisi Jamii na sheria mbalimbali za kitaifa na za Kimataifa.

Jumla ya Askari Polisi 3264 wakiwemo wanaume 2373 na wanawake 891 wamehitimu mafunzo yao ya awali ya miezi sita na kupangiwa kazi katika mikoa mbalimbali.

Sherehe hizo ambazo pia zilihudhuliwa na Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa na Wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Wakuu wa Vyuo vya Polisi, JWTZ, Magereza, Uhamiaji na wananchi, zilitanguliwa na Mgeni Rasmi kukagua gwaride na kutoa zawadi kwa askari 12 waliofanya vizuri zaidi ya wengine kabla ya kuona maonyesho ya Ujasiri na utayari wa wahitimu.

Kutojiunga na CHF kunaleta picha mbaya kwa Mkoa wa Kagera - RC

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe akifungua mkutano wa wadau mkoani humo jana. 

Na Grace Michael, Kagera
MKUU wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe amesema afya ni hazina kubwa kwa kila mwananchi ambayo inatakiwa kulindwa kwa gharama yoyote hivyo akazitaka Halmashauri mkoani humo kushindana katika uandikishaji wa kaya zinazojiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

Amesema kuwa kitendo cha kushindwa kujiunga na Mfuko huo kinaleta picha mbaya mkoani humo kutokana na ukweli kwamba wananchi wanazo fursa nyingi za kujiiingizia kipato.

Massawe aliyasema hayo jana mkoani hapa wakati akifungua mkutano wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambao ulilenga kujadili mambo mbalimbali zikiwemo changamoto zinazoukabili Mfuko huo hatimaye huduma zake ziweze kuboreshwa.

"Afya ni hazina kubwa kwa kila mwananchi hivyo ni lazima suala hili tulione ni la muhimu na tulifanyie kazi, uchumi wa Mkoa huu ni mzuri tu...tusiwekeze afya zetu katika hali ya mashaka...wenzetu waheshimiwa madiwani, wabunge na viongozi wengine, hamasisheni wananchi kujiunga na Mfuko huu kwa kuwa unayo manufaa makubwa kwa afya zetu," alisema.

Aliongeza kuwa ni lazima Halmashauri zishindane katika uandishaji wa kaya kujiunga na Mfuko huu ili lengo la kuwa na afya bora kwa wote lionekane kwa vitendo.

Alisema kuwa kutokuwepo kwa CHF ndani ya Halmashauri ni kuonesha kushindwa viongozi waliopo ndani ya Halmashauri husika, hivyo akaonya kuwa hali hiyo asingependa kuiona mkoani kwake.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka wadau hao kutokuwa  wanaharakati katika kuchangia hoja mbalimbali kuhusiana na suala la Mfuko wa Afya ya Jamii hivyo akasisitiza kila mdau kuwa na mchango chanya ili kusaidia kuboresha huduma za Mfuko huo.

"Tusiwe kama wanaharakati ambao wanaangalia mambo kwa mtizamo hasi...lazima tuangalie kama kuna mahali pa kupongezwa Mfuko upongezwe na kama kuna eneo la kusahihiswa basi ifanyike hivyo ili kuutendea haki na uweze kudumu na kuhudumia wananchi wetu," alisema Massawe.

Aliongeza kuwa umuhimu wa suala la afya upo katika kila nchi na akasema kuwa katika nchi zingine kila mwananchi anatakiwa kuwa kwenye mfumo wa bima ili aweze kupata matibabu.

Aidha aliupongeza Mfuko kwa hatua ya kusogeza huduma kwa wanachama wake hasa kwa kusogeza ofisi katika ngazi ya Mkoa kwani hiyo ndiyo hatua nzuri na yenye kuoneshwa mafanikio.

"Natoa agizo kwa wakurugenzi wote kuhakikisha mnachangamkia fursa hii ya mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo ili huduma katika vituo vyetu ziwe bora zaidi," alisema.

Massawe alitumia fursa hiyo kuuomba Mfuko kuendelea na uwekezaji katika miradi ya maendeleo katika sekta ya afya ikiwemo uwekezaji au ujenzi wa vituo vya matibabu vya mfano.

Naye Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Prof. Joseph Shija, alitoa wito kwa watoa huduma kutumia fursa zinazotolewa na Mfuko huo kwa uzalendo na uadilifu mkubwa ili badae wananchi wote waweze kunufaika na mfuko.

Akitoa maelezo ya utangulizi, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba, aliwataka wadau hao kutoa michango yao bila woga kwa kuwa ndio njia nzuri ya kusaidia kuboresha huduma zake.

Baada ya mkutano huo wa wadau mkoani Kagera, timu nyingine ya Mfuko itaendesha mikutano katika Mikoa ya Tabora, Kilimanjaro na Tanga, lengo ni kuhakikisha wadau wanakutana na kujadili kwa pamoja ili kupata majibu ya uboreshaji wa huduma kwa wanachama na wananchi kwa ujumla.

March 30, 2012

Waziri wa Mazingira Terezya 'ateta' na Balozi Mpya wa Umoja wa Ulaya

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dkt. Terezya Huvisa akimkaribisha Balozi Mpya wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Bw Filiberto Ceriani mara baada ya kujitambulisha  Ofisini kwa Waziri Mtaa wa Luthuli Mjini Dar es Salaam Machi 30.12. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dkt. Terezya Huvisa akiwa katika mazungumzo na  Balozi Mpya wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania  Bw Filiberto Ceriani Sebregondi alipokwenda kujitambulasha kwa waziri, Mtaa wa  Luthuli Mjini Dar es Salaam.[Picha na Ali Meja]

Mungu Ibariki Afrika... Tunusuru na majanga haya


MZEE MKAPA ATUA ARUMERU LEO

Rais na Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa akiwa kwenye chumba cha kufikia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) baada ya kupokewa kwenye uwanja huo na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (kushoto), leo asubuhi. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye. (Picha na Bashir Nkoromo)

Radio One sasa tunawafikia - TABORA


Kwa wasikilizaji wa Radio One Stereo mkoani Tabora hivi sasa Radio One inapatikana na kusikika vizuri kabisa katika masafa ya 98.1 Fm. Tabora, tumewasikia na sasa tumewafikia

March 29, 2012

CAG Utouh akabidhi ripoti yake kwa Rais Kikwete Ikulu jijini Dar

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bwana Ludovick Utouh akikabidhi ripoti yake kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi Machi 29.12.Kushoto ni Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bwana Atanas Tarimo. (picha na Freddy Maro) 

****************
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, leo, Alhamisi, Machi 29, 2012, amepokea rasmi Ripoti ya Mwaka ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bwana Ludovic Utoah kwa mujibu wa mahitaji ya Kifungu 143 (4) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika shughuli hiyo iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, Rais Kikwete kwa zaidi ya saa mbili amemsikiliza Bwana Utoh akiwasilisha Ripoti hiyo ya Mwaka wa Fedha wa 2010/2011 na ambayo zamu hii imepanuliwa kwa kiasi kikubwa kulingana na mahitaji ya sasa ya ukaguzi na ikilinganishwa na ripoti za miaka iliyopita.

Bwana Utoah amewasilisha Ripoti yenye sehemu  mbili kuu ambazo ni (1) Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali Kuu na (2) Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali za Mitaa. 

Mbali na ripoti hizo mbili kuu, Bwana Utoah pia amewasilisha Ripoti ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma, Ripoti ya Ukaguzi wa Balozi wa Tanzania nje, Ripoti ya Miradi Mikubwa ya Maendeleo, Ripoti ya Ufanisi na Uchunguzi na Ripoti ya Ajali za Barabarani nchini.

Kwa kila ripoti, Rais Kikwete ametoa maelekezo ya usambazaji na hatimaye utekelezaji wa ripoti hizo kama ifuatavyo:

(a)          Moja, Rais Kikwete ameagiza maandalizi kufanywa na ofisi yake ili kuwasilisha rasmi Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali Kuu kwa Waziri wa Fedha na kuwasilisha Ripoti ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya ripoti hizo kuwasilishwa rasmi Bungeni ili zijadiliwe na kutolewa ushauri kama ipasavyo.

(b)         Pili, Rais Kikwete amemwelekeza Bwana Utoah kujiandaa ili aweze kuwasilisha hoja kuu zilizopo kwenye Ripoti hizo kwenye Baraza la Mawaziri ili washauri hao wakuu wa Rais waweze kujua kina nini kipo kwenye Ripoti hizo na yapi yanasemwa kuhusu Wizara mbali mbali.

(c)           Tatu, Rais amemwelekeza Bwana Utoah kuhakikisha kuwa Ripoti ya Hesabu za Serikali za Mitaa inawasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa ALAT.

(d)         Nne, Rais Kikwete amewaelekeza Mawaziri na viongozi katika ngazi mbali mbali kuzipitia Ripoti zinazohusu maeneo yao ya kazi na kuzifanyika kazi kama ipasavyo.

Rais Kikwete amemshukuru Bwana Utoah na ofisi yake kwa kazi nzuri na kumtaka kuendelea na kasi hiyo kwa sababu kazi ya kufanya bado ni kubwa.
Rais amesema kuwa amefurahi kuona ofisi ya CAG imeanza kazi ya ukaguzi wa uchunguzi na ufanisi (forensic audit) kuhusu miradi mbali mbali ya maendeleo na shughuli nyingine zinazotumia fedha za umma.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
29 Machi, 2012 

Joaquine De-Mello atunukiwa Tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania 2012

Ofisa wa Mambo ya Nje wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Dana Banks akizungumza wakati wa hafla ya kumtunuku Tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania 2012, Bi. Joaquine De-Mello iliyofanyika katika ubalozi huo jijini Dar es Salaam leo Machi 29.12. De-Mello ni Mwanasheria Kitaaluma na amekuwa Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora tangu Mwaka 2008. Aidha Ubalozi wa Marekani hapa Nchini umeamua kumtunuku tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kutetea Haki za Wanawake hapa nchini. PICHA ZOTE/JOHN BADI

Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.

Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini, Robert Scott  akisoma hotuba kabla ya kukabidhi tuzo hiyo.

Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.

Wimbo wa taifa wa Tanzania na Marekani ulipigwa na Kwaya ya Vijana ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzani la Kijitonyama (Haipo pichani).
Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini, Robert Scott akikabidhi Tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania 2012, Bi. Joaquine De-Mello.

Mwanamke Jasiri Tanzania 2012, Bi. Joaquine De-Mello akitoa neno la shukrani baada ya kupokea tuzo.
Robert Scott akimpongeza De-Mello baada ya kutoa neno la shukrani.

Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Alice Foundation ambaye pia ni Mkurugenzi wa Alice Fashion World, Alice James Dosi akikabidhi zawadi ya maua kwa De-Mello kama ishara ya kumpongeza.
Pongezi ziliendelea kumiminika.

De-Mello akiwa katika picha ya pamoja na Robert Scott na Dana Banks.
De-Mello akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Wa (tatu kulia) ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Amir Manento.

De-Mello akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) ambaye ni mmoja kati ya waliowahikupata tuzo kama hiyo Mwaka 2010, Bi. Ananilea Nkya (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Under The Same Sun (UTSS) Tawi la Tanzania, Bi. Vicky Ntetema (kulia).

MAZISHI YA MAREHEMU DENIS OSWALD KAPINGA

Ndg. Joseph Oswald Kapinga

Ndugu Joseph Kapinga (pichani hapo juu) anapenda kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki kuwa Ratiba ya mazishi ya mpendwa mdogo wetu Denis O. Kapinga yatafanyika leo Tarehe 29/03/2012 katika makaburi ya Sinza karibu na ukumbi wa mwika.

Ratiba itakuwa kama ifuatavyo:

Mwili wa marehemu utafika Nyumbani maeneo ya Sinza karibu na New White Inn Bar bara bara ya Sinza Uzuri mnamo saa 6.00 Mchana kutoka Hospitali ya Mwananyamala.

Mwili utaagwa nyumbani saa 7.00 Mchana na baadae utapelekwa kanisa la Roman Catholic Sinza kwa Ibada.

Baada ya hapo Saa 8.30 Mchana mwili wa marehemu utapelekwa Makaburi ya Sinza kwenye nyumba yake ya milele.

"BWANA ALITOA NA BWANA

WANASIASA WANAOJITAPA KUIGEUZA ARUMERU TUNISIA KUKIONA: POLISI

DCP Isaya Mngulu
* Yasema imejiandaa kisawasawa kusambaratisha vyanzo vyote vya vurugu vitakavyojitokeza
 
* Watakaozianzisha kuwa wa kwanza kushukiwa

USA RIVER
Zikiwa zimebakia siku tatu ufanyike uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki,  Jeshi la Polisi limewaonya wanasiasa wanaojitapa kuwa jimbo hilo litageuka Tunisia kwa umwagaji damu, na kusema kwamba jeshi hilo limejiandaa kikamilifu kukabiliana na yeyote atakayejaribu kuvuruga amani tangu sasa hadi mwisho wa uchaguzi.

Limesema limeshasikia kauli za baadhi ya wanasiasa wakijitapa na kuwashawishi kwenye mikutano ya kampeni kwamba vyama vyao visipopata ushindi Arumeru Mashariki patachimbika na kuwa kama Tunisia, kauli ambayo limesema ni ya hatari sana kwa wapenda amani na utulivu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Operesheni Jimbo la Arumeru Mashariki, Naibu Kamishna wa Polisi Isaya Mngulu alisema jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kila hatua moja kunakuwa na doria imara zikiwemo za askari waliovaa kiraia.

Akitoa taarifa ya hali ya hali ya ulinzi na usalama katika kipindi cha kampeni zinazoendelea, Mngullu alisema jumla ya matukio 36 ya uhalifu wa kisiasa yameripotiwa na kuendelea kuchukuliwa hatua mbalimbali.

Mngulu alisema  miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kwafikisha mahakani kwa hatua zaidi za kisheria na kuyataja matuki hayo kuwa ni ya kujeruhi, matumizi ya lugha za matusi, kuchana picha za wagombea, kushambulia mwili, kuchana bendera, kutishia kuua, kuchoma moto bendera, wizi wa bendera na kuharibu mali na kwamba matukio hayo yapo kwa idadi mbalimbali.

“Mpaka sasa kesi nne namba USR/IR718.2012 CC No. 227/2012 kuharibu mali, USR/IR/721/2012 CC No. 228/2012 shambulio, USR/IR/780/2012 CC No. 241/2012 shambulio ,USR/IR/749/2012 CC No. 230/2012 shambulio zimepelekwa mahakamani" alisema Mngullu na kuongeza.

“Kesi mbili USR/IR/687/2012  shambulio la kudhuru mwili na USR/IR/694/2012  shambulio  la kudhuru mwili zimepelekwa ofisi ya mwanasheria kwa hatua za utendaji na zilizobakia zipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.".

Mbali na taarifa hiyo jeshi hilo pia limebainisha kwamba linaendelea kufanyia kazi matamko yaliyotolewa na baadhi ya vyama vya siasa vinavyoshiriki kufanya kampeni kwa kutumia lugha za matusi, kudhalilishana, uchochezi na vitisho kwa vyombo vya dola kuwa ushindi usipopatikana  Arumeru patachimbika na kuwa mfano wa Tunisia.

Mngulu alisena Jeshi la polisi limestushwa sana na kauli hizo kutolewa na wanasiasa wawapo majukwaani huku Asasi za kiraia zinazopigania haki za binadamu na utawala bora hususani wanaharakati wakiwa wamekaa kimya na kushindwa kujitokeza na kukemea vitendo hivyo badala yake kusubiri kutoa matamko ya kulaumu polisi pale linapoingilia kati na kuchukua hatua za kurudisha hali ya utulivu na amani kutokana na vitendo vya uvunjifu amani vinavyosababishwa na kuchochewa na viongozi.

Mbali na kuonyesha kusikitishwa, jeshi hilo limekemea na kuvitaka vyama vya siasa vinavyojifanya maandamano na misafara batili mara baada ya kumaliza mikutanio yao ya kampeni kuacha mara moja kwani kuendelea kufanya hivyo ni kuvunja sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani.

Mngullu alisema, zipo taarifa kwamba moja ya vyama ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa kufanya maandamano ni CHADEMA na kutoa mfano kwamba  baada ya mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Jumatatu mjini Usa River, walionekana wakiongoza misarafa ya wanedesha pikipiki kuzunguka mitaani wakiandamana na malori yao Fuso ya chama hicho jambo ambalo lingeweza  kuhatarisha amani.

Kamishna Msaidizi Mngulu aliwataka wanasiasa wanaohamasisha wafuasi wao, wakereketwa na wanachama kulinda kura za mgombea wao kuacha mara moja kitendo hicho kwani kila Chama kimeweza kutoa wakala ambaye kimemuamini kwa kazi hiyo.

“Wanachama hawana sababu ya kuhamasishana kulinda kura kwani kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 80 (2) (G) cha sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 ya Mwaka 2010 inabainisha wazi kuwa kila Chama kitakuwa na wakala wake wa kuhakiki na kulinda kura za mgombea ndani ya kila chumba cha kupigia kura,” alisema Kamishna Msaidizi Mngulu.

Kamishna Msaidizi Mngulu alivitaka vyama vya siasa kujipanga baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo, ambapo alikitaka Chama kitakachokuwa kimeshinda kuainisha mapema sehemu, muda na taratibu za kusherehekea ushindi wao bila kuathiri na kubughudhi shughuli au mali za watu wengine.

Uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki, utafanyika Aprili Mosi mwaka huu, kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM Jeremiah Sumari mapema mwaka huu ambapo jumla ya vyama vinane vimeweka wagombea.
Source: Nkoromo Daily Blog


Wanafunzi wa CBE watakaokiuka Sera ya Mavazi kukumbana na Adhabu.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dar es Salaam,  Bw. Athman Ally Ahmed akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo Machi 28.12, kuhusu kuanza kutumika kwa sera ya mavazi chuoni hapo yenye lengo kupiga vita mavazi yasiyo ya heshima kufuatia kukithiri kwa vitendo vya uvaaji wa mavazi yasiyokuwa na staha vinavyofanywa na wanafunzi  wa kike na wale wa kiume wawapo chuoni. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

Aina ya mavazi yasiyostahili kwa Wanafunzi wa CBE

Na. Aron Msigwa – MAELEZO

Uongozi wa Chuo cha elimu ya biashara (CBE) kampasi ya Dar es salaam umesema kuwa hautasita kumchukulia hatua mwanafunzi au mfanyakazi  yeyote atakayefika chuoni hapo akiwa amevaa mavazi yasiyo ya heshima huku ukitoa wito kwa wananchi kuunga mkono kampeni hiyo yenye manufaa katika kujenga taifa lenye maadili mazuri.
 
Akizugumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Machi 28.12, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dar es Salaam, Bw. Athman Ally Ahmed amesema chuo hicho kimefikia uamuzi huo kufuatia kukithiri kwa vitendo vya uvaaji wa mavazi yasiyokuwa na staha vinavyofanywa na wanafunzi  wa kike na wale wa kiume wawapo chuoni hapo hali inayosababisha udhalilishaji wa utu wa wanafunzi ndani na nje ya chuo.
 
Amesema wanafunzi ambao wengi wao ni vijana chuoni hapo wamekuwa mstari wa mbele katika kuiga kila aina ya vazi kutoka tamaduni za watu wa magharibi hali ambayo ameielezea kuwa ni ukiukaji wa mila , desturi na tamaduni za mtanzania .
 
“Mtindo huu wa kuiga tamaduni za magharibi pasipokuangalia wapi tunakwenda haukubaliki hata kidogo,ukiangalia katika vyuo vingi vya elimu hapa nchini wanafunzi wamekuwa wakivaa mavazi ya ajabu na yasiyofaa kabisa katika maeneo ya chuo” amesema.
 
Amesema kuwa Chuo hicho  kimekaa na kubuni sera  ili kuyaondoa mavazi ambayo hayaruhusiwi kuvaliwa katika maeneo ya chuo  na kubuni sera ya mavazi kwa ajili ya wanafunzi  hali itakayowajengea  nidhamu wasomi  hao  wa fani mbalimbali pindi watakapomaliza masomo yao chuoni hapo.
 
Amefafanua kuwa  adhabu mbalimbali zitatolewa kwa wanafunzi watakaokiuka agizo la uvaaji wa mavazi yenye heshima amabazo ni pamoja na kuzuiliwa kupita getini kwa mwanafunzi husika kuingia katika eneo la chuo kwa wale wanaotoka nje ya hosteli na wale wanaoishi ndani ya eneo la chuo hawatapewa huduma yoyote kama vile kuingia darasani,kantini , maktaba au ofisi yoyote ya chuo.
 
Aidha amefafanua kuwa wanafunzi  ambao  hawatakua  tayari kufuata utaratibu huo watafikishwa mbele ya kamati ya nidhamu huku akibainisha kuwa adhabu itakayotolewa ni mwanafunzi kusimamishwa  chuo kwa  muda wa miezi mitatu.
 
Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni mkurugenzi wa mafunzo Bi. Bertha Kipillimba amesisitiza kuwa zoezi hilo litawahusu wafanyakazi wote wa kampasi ya Dar es salaam na wanafunzi  zaidi ya 6000 wa chuo hicho.
 
Amesema hivi sasa taratibu hizo za uvaaji wa mavazi yenye staha zimeingizwa kwenye kanuni za chuo  na kuongezwa kwenye masharti ya fomu za kujiunga na chuo hicho huku akifafanua kuwa tayari wametoa kipindi cha wiki mbili kwa utekelezwaji wa kanuni hizo na watakaokiuka kuadhibiwa kwa mujibu wa kanuni hizo.
 
Naye mlezi wa wanafunzi wa hicho (Dean of Students) Bw. Faustin China amefafanua kuwa umefika wakati wa wanafunzi hao kujitambua huku akisisitiza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakinyoshewa vidole na jamii kuhusu suala la uvaaji na mienendo ya wanafunzi chuoni hapo.
 
“Tumesemwa vibaya kwa muda mrefu hatuwezi kuachia suala hili likaendelea, tunataka wanafunzi wetu wavae vizuri kwa mujibu wa kanuni tulizojiwekea ili kujenga heshima ya chuo” amesema.
 
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na uanzishawaji wa sera ya mavazi chuoni hapo wakieleza kuwa inaingilia uhuru wao wa kuamua huku wengine wakiupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuliona suala hilo na kulichukulia hatua ili kuleta na kulinda heshima ya chuo hicho.

Rais Kikwete aongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM - Ikulu

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmshauri kuu ya CCM Ikulu jijini Dar es Salaam Machi 28.12. (picha na Muhidin Issa Michuzi)

Malalamiko, Lawama na Manung'uniko ni Ugonjwa uliowakumba Watanzania: Rais Dk. Kikwete

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua warsha ya siku mbili ya mikakati ya kiuchumi ya kuondoa umaskini iliyoandaliwa na REPOA katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam Machi 28.12.
******************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa moja ya magonjwa makuu yanayowakumba Watanzania kwa sasa ni ugonjwa wa Kitanzania wa kulalamika, kunung’unika wakimlaumu kila mtu isipokuwa wao wenyewe.

Aidha, Rais Kikwete amesisitiza kuwa Serikali yake itahakikisha kuwa utajiri na manufaa yanayopatikana na yatakayopatikana kutokana na raslimali za madini na gesi asilia nchini yanamnufaisha kila Mtanzania.

Rais Kikwete pia ameahidi, kwa mara nyingine tena, kuwa Serikali yake itaendelea kuwekeza katika huduma za jamii kwa kuboresha huduma za elimu na afya, kuendeleza kilimo na kuinua hali ya uchumi wa vijijini kama njia ya kuwainua Watanzania wengi zaidi, na hasa wale masikini zaidi, kutoka kwenye umasikini.

Rais Kikwete ameyasema hayo, jana Jumatano, Machi 28, 2012, wakati alipofungua Warsha ya 17 ya Utafiti ya Mwaka ya shirika lisilokuwa la kiserikali la Research on Poverty Alleviation (REPOA) inayofanyika kwa siku mbili kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
 
Rais Kikwete amewaambia washiriki wa Warsha hiyo wanaotoka nchini na nje ya nchi, na hasa wale kutoka nje ya nchi kujitahidi sana kuepukana kuambukizwa ugonjwa wa Kitanzania wa kulalamika, kunung’unika na kulaumu wakati wanapojadili changamoto na njia bora zaidi na za haraka zaidi kupunguza ama kumaliza umasikini nchini.
 
 “Nawaombeni nyote mlioko hapa leo kutumia nafasi ya Warsha ya Utafiti hii kwa kutathmini kwa kina kabisa changamoto zinazohujumu dhamira yetu ya kupata mageuzi ya haraka zaidi ya kiuchumi na kijamii“, amesema Rais Kikwete na kuongeza: “Mnaweza kufanya hivyo kwa kutumia ujuzi wenu wa nyuma ama kwa kutumia uzoefu wa nchi nyingine. Tafadhalini sana epukeni  na jizuieni sana kutokuambukizwa ugonjwa wa Kitanzania wa kulalamika na kulaumu wengine wote isipokuwa sisi wenyewe. Ni ugonjwa usiokuwa na tija.”

Kuhusu nafasi ya raslimali za madini na gesi asilia nyingi iliyogunduliwa nchini, Rais Kikwete amerudia tena ahadi yake ambayo ameitoa huko nyuma kuwa Serikali yake itahakikisha kuwa raslimali hizo zinawanufaisha Watanzania wote bila kubagua kwa sababu kila Mtanzania anayo haki ya kunufaika na raslimali za nchi yake.
 
Katika hotuba yake, Rais Kikwete ambaye amesisitiza mageuzi makubwa ya sera ambako sasa wajibu wa Serikali ni kufungua njia za uwezeshaji na sekta binafsi kufanya biashara tofauti na sera za zamani ambako Serikali ilikuwa inafanya hata biashara ya bucha za nyama na maduka ya sindano na viberiti amewaambia washiriki wa Warsha hiyo:
 
“Serikali kwa upande wake itaendelea kutekeleza mipango na sera ambazo zinamnufaisha kila mtu na zenye kuhudumia maslahi ya jamii zilizo masikini zaidi na zisizojiweza. Tutaendelea pia, kuwekeza zaidi katika huduma za jamii kwa kuinua kiwango na ubora wa elimu, huduma za afya, kuboresha kilimo na uchumi wa maeneo ya vijijini.”

TBL MEDIA BONANZA 2012: Kwa raha zaoooo

 Chezea wanahabari weweeeeeeee ............

March 28, 2012

UZINDUZI WA UTAFITI WA KUKU WA ASILI

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga fimbo mfano wa umbo la  yai  ikiwa ni ishara ya kuzindua matokeo ya utafiti wa kuboresha ufugaji wa kuku wa asili katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dares Salaam Machi 28.12.PICHA ZOTE NA MAGRETH KINABO - MAELEZO

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia  chanjo dhidi ya magonjwa ya mdodo na kideri  huku akipata maelezo kutoka kwa Dk. Gabriel Shirima  wa Maabara Kuu ya  Mifugo ya Temeke.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifurahia ubunifu wa mfano wa  umbo la mfano wa  yai.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo ya ufugaji kuku wa asili kutoka kwa  mfugaji , Godfrey Mwaipopo mkazi wa  Kibaha wakati wa uzinduzi wa  matokeo ya utafiti wa kuboresha ufugaji wa kuku wa asili katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Baadhi ya  wadau wa uzinduzi wa  matokeo ya utafiti wa kuboresha ufugaji wa kuku wa asili wakiwa katika uzinduzi huo.

RAIS KIKWETE AFUNGUA WARSHA YA MIKAKATI YA KUONDOA UMASKINI JIJINI DAR LEO

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo, Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe, Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek, Katibu Mtendaji a Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Saidi Meck Sadick muda mfupi kabla ya kuondoka hoteli ya White Sands Hotel alikofungua warsha ya siku mbili ya Utafiti.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Profesa Ibrahim Lipumba baada ya picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya siku mbili ya utafiti juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini.

Profesa Do Duc Dinh toka Vietnam akitoa mada ya jinsi nchi yake ilivyofanikiwa kuondoa umaskini warsha ya siku mbili ya utafiti juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini nchini.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Katibu Mtendaji a Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango  kwa mada nzuri. Kati yao ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe na Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza  Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango  akitoa mada ya ufunguzi wa warsha hiyo ya siku mbili ya REPOA. Wengine toka shoto  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe na Balozi wa Uholanzi nchini Dkt. Ad Koekkoek.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa kwa hotuba nzuri ya ufunguzi na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe. PICHA/IKULU

March 27, 2012

MICHUZI BLOG 'atoka' na WiFi

Tovuti yako uipendayo inakupa huduma ya kujivinjari bure kutoka Uhuruone

Muhidini Issa Michuzi akishikiriana na Uhuruone wanawapatia wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya “Wifi hotspots” ambayo itawapa wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya bure ya kutembelea tovuti ya Michuzi. Kwa kupitia mitambo yao ya “Wifi Mesh” iliyopo Dar es Salaam ambayo imeunganishwa na tovuti ya Michuzi,wakazi wa Dar es Salaam wanatangaziwa kwamba wawashe kompyuta zao na kuunganishwa na taarifa za punde bila gharama yoyote.

Akikaririwa katika mahojiano ndugu Issa Michuzi alisema hivi, “Ni mapinduzi ya kweli ambapo Watanzania wanachukua hatua katika kuleta taarifa mbalimbali kwa wananchi katika viwango nafuu. Ninaamini hii itaongeza mawasiliano kwa watu wetu na ni ndoto yangu kwamba tovuti ya Michuzi itakua huru kufika kwa Watanzania wote hivi karibuni”.

Akiwa ofisini Bwana Rajabu Katunda alisema, “Uhuruone imejikita katika kutoa huduma kwa jamii na tumegundua kwamba taarifa za kijamii zinatakiwa kuwafikia wanajamii kwa urahisi. 

Tovuti nyingi zinatembelewa na Watanzania waliopo nchi za nje kuliko wananchi waliopo nchini na hii siyo haki. Kama nina uwezo kupata taarifa kwenye tovuti ya Michuzi ni jukumu letu kama kampuni kuwawezesha watanzania waliopo nchini pia kupata huduma. 

Watanzania tunatakiwa kuwa na utamaduni wa kusaidiana na kupeana moyo na hii itasaidia kukuza uchumi wetu sio tu kununua na kuuza bidhaa kutoka nje.

Kwa pamoja Bwana Michuzi na Katunda wamesema huu ni mwanzo tu na wanaamini kwamba hili wazo litafuatwa na wengine. Kwa msisitizo Bwana Michuzi aliongea “Lazima tuonyeshe mfano kwa vitendo sio maneno tu. Tumechukua hatua ya kwanza katika kufanikisha ndoto, wengine wanatakiwa kujiunga kwenye mapinduzi haya na kufanikisha”

Kutembelea tovuti ya Michuzi bila gharama washa Wifi kwenye Ipad, Tablet, Simu au Laptop. Tafuta Michuzi blog Wifi, Unganisha ,fungua browser yako uipendayo mfano Chrome, Internet Explorer, Safari au Firefox na nenda kwa Issa Michuzi.blogspot.com.

Kama hautaona tovuti ya Michuzi Wifi, tafadhali wasiliana na Uhuruone kwa email ifuatayo, issa.michuzi@uhuruone.com au piga simu namba 255779477477 ili uweze kuunganishwa.
 

Mpigie Kura yako Mwanamuziki umpendaye ili aweze kushinda Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2012

Piga Kura yako kwa Mwanamuziki umpendaye ili aweze kushinda tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2012.ili kupiga kura yako, Bofya hiyo Link
http://www.kilitime.co.tz/awards/2009/nominees_2007.php

Mradi wa Maji wa Vodacom Foundation kunufaisha wanakijiji 4,000 mkoani Dodoma


Mkuu wa Mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Tanzania (Vodacom Foundation), Yessaya Mwakifulefule akimtwisha Amina John ndoo ya maji ya kunywa yaliyochotwa katika kisima kilichotolewa msaada na Vodacom Foundation kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Inyumbu Mkoani Dodoma,Mradi huo umegharimu thamani ya shilingi milioni 40.

Mkuu wa Mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Tanzania(Vodacom Foundation) Yessaya Mwakifulefule (kulia )akiwa na wakazi wa kijiji cha Inyumbu Mkoani Dodoma wakinywa maji salama yaliyotokana na mradi wa Kisima kilichojengwa na Vodacom ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 40 uliotolewa na Vodacom Foundation.
**********************************
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusaidia Jamii (Vodacom Foundation) imekabidhi mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 40 katika kijiji cha Inyumbu ikiwa ni mwendelezo wa azma yake ya kusaidia jamii hapa nchini.

Kukabidhiwa kwa mradi huo kunapunguza shida ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi zaidi ya 4,000 wa kijiji cha Inyumbu na maeneo jirani.

Akipokea mradi huo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Yona Ngobito aliishukuru kampuni ya Vodacom kwa kuwekeza shilingi Milioni 40 ili kuokoa maisha ya wananchi ikifahamika wazi kuwa maji ni bidhaa muhimu na nyeti katika maisha ya binadamu.

"Kila msaada ni muhimu kwa walengwa husika ila tunapozungumzia maji tunagusa moja kwa moja uhai wa binadamu, hili ni jambo jema kwenu wanakijiji wa Inyumbu ambao sasa wanawake na wasichana wanaweza kutumia muda mfupi kupata bidhaa hiyo na kutumia muda wa ziada kufanya shughuli nyengine za kifamilia"Alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa kijiji ametumia pia fursa hiyo kuwasihi wanakijiji kuona thamani ya mradi huo na njia pekee ya kurudisha shukrani kwa Vodacom ni kuutunza mradi huo ili uwasidie kwa muda mrefu zaidi.

 "Ndugu zangu hasa wakina mama tukitambua shida ambayo tulikuwa nayo hapo kabla ya kuletewa mradi huu na Vodacom ni wazi tutaona thamani yake na kila mmoja atakuwa mlinzi wa mradi huu dhidi ya aina yoyote ya uharibifu, hiyo si tu kwamba itatusaidia kuwa na uhakika wa maji bali tutawapa nguvu Vodacom kurudi tena kuangalia eneo jingine la kutusaidia"Aliongeza Ngobito.

Nae Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,alisema Vodacom Foundation imekua ikithamini maisha ya watanzania wengi na hivyo kujitolea katika kusaidia na kufadhili shughuli mbalimbali za maendeleo ya kijamii hapa nchini.

Aliongeza kuwa kutokana na kwamba Mkoa wa Dodoma una ukame katika baadhi ya maeneo yake na hivyo kuleta changamoto katika upatikanaji wa maji safi na salama kwamatumizi ya binadamu hasa maeneo ya vijijini jambo lililoigusa kampuni ya Vodacom kupitia mfuko huo na kufikia uamuzi wa kufadhili mradi huo wa maji kupitia teknolojia ya upepo.

 "Katika jitihada zetu za kuboresha ustawi wa jamii za watanzania kwa kuwa washirika wa huduma za kijamii nchini zimetufikisha hapa katika kijiji cha Inyumbu kukabidhi mradi huu, ni matumaini yangu kwamba sasa mama zangu wa hapa kijijini wamefurahi kwa kupunguziwa hali iliyokwepo hapo awali ya kutumia muda mrefu kusaka maji kwa shughuli mbalimbali za kifamilia"Alisema Mwakifulefule.

Kila mwaka tunatenga fedha kusaidia maeneo mbalimbali ya kijamii hasa elimu,afya, maji,mazingira na ujasiriamali, tunafanya hivyi tukitambua kuwa biashara kwetu ni sehemu moja ila namna tunavyokuwa karibu kusaidia wale wanaotuzunguka katika baishara zetu ni jambo moja muhimu sana katika shughuli zetu, tutaendelea kufanya hivyo tukiamini kwamba azma yetu ya kubadili maisha ya wananchi inatekelezeka" Aliongeza Mwakifulefule.

Vodacom kupitia Vodacom Foundation iliufadhili mradi huo kwa shilingi Milioni 40 kupitia Mamlaka ya maji ya kijiji cha Inyumbu kwa kushirikiana na mradi wa maji wa C.P.P.S.