Tangazo

October 14, 2013

Mwandishi wa ITV alivyopigwa risasi na Mama yake kuuawa

MWANDISHI wa habari wa ITV, Ufoo Saro, aliyejeruhiwa kwa risasi jana asubuhi, alilazimika kuvumilia majeraha ili kujiokoa yeye mwenyewe na wadogo zake watatu waliokuwa wakipigwa risasi, baada ya mama yake mzazi, Anastazia Saro (58), kuuawa.

Mauaji hayo ya kusikitisha, yalifanyika katika eneo la Mbezi Kibwerere, nyumbani kwa mama yake Ufoo, ambako alikuwa akiishi na wadogo zake Ufoo ambao ni Goodluck, Innocent na Jonas. Mtuhumiwa wa unyama huo ametajwa kuwa ni Anthery Mushi, ambaye ni baba mtoto wa Ufoo na siku ya tukio wawili hao walitokea Mbezi Magari Saba nyumbani kwa Ufoo, kwenda kuzungumza kifamilia na mama mzazi wa mwandishi huyo.

Mushi (40) ni Mhandisi wa Kitengo cha Mawasiliano katika Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) nchini Sudan na aliwasili nchini juzi na kwenda moja kwa moja nyumbani kwa Ufoo eneo la Mbezi Magari Saba.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, Ufoo amejeruhiwa katika paja na tumboni, mama yake mzazi alikufa papo hapo baada ya kupigwa risasi ya kifuani na mtuhumiwa Mushi ambaye naye alijiua baada ya kujipiga risasi kichwani katika eneo la kidevuni. Akizungumza na gazeti hili jana mdogo wake Ufoo, Goodluck alisema:

Walikuja wakiwa pamoja (Ufoo na Mushi) mapema alfajiri wakiwa ndani ya gari ya Ufoo, saa 12 na kabla ya kuingia ndani, alitusalimia kisha wakaingia sebuleni na kuanza mazungumzo na mama. More News tembelea habarileo.co.tz

No comments: