May 29, 2012

Hatimaye Mtuhumiwa John Warburg atiwa nguvuni na Polisi baaya ya Kuruka Dhamana Kituo Cha Urafiki




Kachero kutoka Polisi Arusha, D/CPL Fortunatus (mwenye tisheti ya pundamilia kushoto), akiimarisha ulinzi wakati Mtuhumiwa wa Kesi ya Wizi wa Kuaminiwa, Bw. John Warburg (mwenye tisheti nyekundu), akiteremka kutoka kwenye Bus la Ngorika katika Kituo cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam leo Mei 29.2012, wakitokea jijini Arusha ambako Mtuhumiwa Warburg alikamatwa kufuatia kuruka dhamana aliyopatiwa katika Kituo cha Polisi cha Urafiki takribani Miezi Mitatu iliyopita. John Warburg alidhaminiwa katika Kituo cha Polisi Urafiki baada ya kukamatwa akituhumiwa kwa kosa la kujipatia Gari aina ya Toyota Cresta GX 100 lenye namba za usajili T 796 AVQ na kuliuza kwa manufaa yake bila idhini ya mwenye mali kesi yenye kumbukumbu namba URP/RB/2412/2012 -.URP/IR/1544/2012. PICHA/DAILY MITIKASI BLOG

Mdhamini wa Mtuhumiwa John Warburg bwana Max Kafipa (kulia), akiwa bega kwa bega na mtuhumiwa wake kuhakikisha anafika Kituo cha Polisi Urafiki.Kushoto ni D/CPL Fortunatus wa Polisi Arusha, aliyemu-escort mtuhumiwa hadi hapa jijini.

11 comments:

  1. AnonymousMay 29, 2012

    Yaani usharobaro wote huo jamani kumbe jamaa tapeli kweli kwa kuangalia kwa macho huwezi kumdhania kabisa jamani

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2012

    Nina huyu?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2012

    Mshkaji umeacha kuuza unga siku hizi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2012

    Warburg kweli za mwizi arobaini uliniibia na kunitapeli mimi huku morogoro Mali zangu za thamani na kutorokea dar na nilishindwa kukufuatilia sabab ya vitisho vyako vya uanajeshi kumbe unatumia cheo chako kufanya mambo ya kipuuzi, kila mwanzo una mwisho

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2012

    Kumbe mjeda aibu pumbaf

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2012

    Arusha tulikuheshimu kumbe shemeji umekimbia soo, pole sana

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2012

    huyu jamaa kijiwe chake kilikuwa maryland mwenge ni tapeli huyooo! kaliza wengi hasa wadada

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2012

    huyu jamaa kijiwe chake kilikuwa maryland mwenge ni tapeli huyooo! kaliza wengi hasa wadada

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 10, 2012

    Jeshi limekushinda? Mkuu wamajeshi unaona vituko vya wamajeshi watu Kama hawa wanalichafua jeshi la Tanzania mulika mwizi

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 15, 2012

    Huyu ni tapeli professional alimliza ndugu yangu Stargell amekamatwa za mwizi arobaini

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 21, 2012

    Hhaa baba Sandra umeanza lini utapeli? Huyu tulikuwa tunakaa nae lugalo fleti tunatazamana Leo kweli umefikia hatua hii kweli maisha yanabadilika, usipoangalia jirani utaishia pabaya

    ReplyDelete