June 5, 2012

TBL YAMZAWADIA BAJAJ MSAMBAZAJI BORA KANDA YA KUSINI

Wafanyakazi wa TBL, wakiangalia Ghala la kisasa la kuhifadhia bidhaa lililojengwa na kampuni ya Massawe Grocery eneo la Mwendapole, wilayani Kibaha.

Wafanyakazi wa TBL, wakiwa ndani ya ghala hilo.

Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Kusini, James Bokela (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Massawe Glosery, Jacob Massawe (wa pili kulia) ufunguo wa Bajaj yenye thamani ya sh. mil. 4.7, baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa kanda hiyo kwa usambazaji na uuzaji wa bidhaa za TBL. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Kibaha, Pwani juzi, ni mke wa Massawe, Anna Massawe na Meneja wa Huduma za Biashara wa TBL, Reginald Mosha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Massawe Glosery, Jacob Massawe na mkewe Anna Massawe, wakifurahia zawadi ya Bajaj yenye thamani ya sh. mil. 4.7.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Massawe Glosery, Jacob Massawe (wa pili kulia) na mkewe Anna Massawe (kulia), wakifurahia zawadi ya Bajaj yenye thamani ya sh. mil. 4.7, kwa kugongeana chupa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na wamiliki wa baa wilayani  Kibaha, waliyokabidhiwa na TBL, baada ya kampuni yao kuwa washindi wa kwanza Kanda ya Kusini kwa usambazaji na uuzaji bora wa bidhaa za TBL. Hafla hiyo ilifanyika Kibaha, mkoani Pwani juzi.

No comments:

Post a Comment