June 6, 2012

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wala Kiapo


Mbunge Shy-Rose Banji akila kiapo chake.

Mh. Samuel Sitta ni muwakilishi wa Tanzania.

Shy Rose Banji akitia saini nyaraka za kiapo.

Mh. Alhaji. Adam Kimbisa.

Mhe. Anjela Charless Kizigha.

Mhe. Bernard Musomi Murunyana.

Mh. Abdullah Ali Hassan Mwinyi.

Mh. Nderkindo Perpetua Kessy.

Mh. Charles Makongoro Nyerere.

Dkt. Twaha Issa Taslima.
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) jana  wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hulo.

Wabunge hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.

Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo hii leo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose SaddrudinBhanji.

Wengine ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya,Mh.Nderkindo Perpetua Kessy, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Mhe Bernard Musomi Murunyana Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa wake wa Uwaziri.

Wabunge hao wameapisha pamoja na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda. SOURCE: FATHER KIDEVU BLOG

No comments:

Post a Comment