June 6, 2012

ZIARA YA NAPE MKOA WA NJOMBE

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye  akihutubia mkutano wa hadahara katika kijiji cha Mlangali, Wilayani Ludewa mkoani Njombe, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa Chama na kukagua miradi ya maendeleo mkoani humo, jana.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye  akicharaza ngoma wakati wa mapokezi yake katika kijiji cha Mlangali mkoani Njombe juzi 4/6/2012.

Wanachi wakijipa sehemu nzuri ya kusimama ili waweze kumuona na kumsikia vizuri Nape alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mlangali, mkoani Njombe.

Mama aliyebeba mtoto wakishangilia kwa furaha wakati wa uzinduzi wa tawi la wakereketwa wa CCM la Liwigi, Ludewa mkoani Njombe uliofanyuwa na Nape katyika ziara hiyo.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifurahi na watoto wa Mlangali, alipopiga nao picha ya pamoja na watoto hao baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara eneo hilo.


Msafara wa Nape ukiongozwa na pikipiki wakati ukiingia mjini Njombe kwa ajili ya mkutano wa hadhara na kufungua matawi kadhaa aya CCM.

Nape akimbeba mtoto  Goodluck John wa shule ya awali ya Lutheran, iliyopo Melizine nje kidogo ya mji wa Njombe, baada ya kumkuta mtoto huyo akiwa na wanafunzi wenzake miongoni mwa watu waliokuwa wakisubiri msafara wa wake kupita eneo hilo akiwa njiani kuingia mjini Njombe.

Nape akizindua shina la wakereketwa wa CCM la Melizine mjini Njombe wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa Chama mkoani Njombe.

Wanafunzi wa shule ya awali ya Melizine wakionyesha alama ya dole, wakati Nape alipopita eneo la shule yao mjini Njombe  leo 5/6/12.

No comments:

Post a Comment