Daily Mitikasi Blog

March 6, 2013

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda avamiwa, ajeruhiwa vibaya

Ndugu Absalom Kibanda akiwa amelazwa kwenye moja ya chumba cha matibabu,hospitali ya Taifa Muhimbili.Get Well soon Absalom Kibanda.Picha kwa hisani ya Mtandao wa Mabadiliko. 
  
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri,na Mhariri Mkuu wa Mtendaji wa New Habari Coperations Ltd, Ndugu Absalom Kibanda, amevamiwa usiku  wa kuamikia leo akiwa anashuka nyumbani kwake Mbezi Beach na watu wasiofahamika na kumpiga kichwani. Amepata majeraha Makubwa kichwani na hasa jichoni,aidha taarifa inaeleza kuwa baada tukio hilo Kibanda alikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu.

Wadau hii ni taarifa ya kushtua sana,lakini tutazidi kutaarifiana kadiri ya habari zitakavyokuwa zinapatikana,kikubwa tumwombee Mungu amponye haraka mpiganaji mwenzetu.
John Hans Badi kwa 1:01 PM
Share

No comments:

Post a Comment

‹
›
Home
View web version

About Me

My photo
Dar es Salaam, Tanzania
View my complete profile
Powered by Blogger.