Wachora katuni kutoka kundi la WAFANYE WATABASAMU: Said Michael
‘WAKUDATA’, Nathan Mpangala ‘KIJASTI’ na Abdul King O ‘KABOKA MCHIZI’ wanao wakilisha
vyombo mbalimbali vya habari nchini, wakitoa mafunzo ya uchoraji kwa watoto
walio katika kituo cha kukuzia vipaji cha KokoTEN Art Centre, Lushoto, mkoani
Tanga.
Wafanye
Watabasamu na wachoraji wa kesho wa KokoTEN Art Centre, Lushoto,
mkoani Tanga. Mafunzo hayo ya siku moja ya uchoraji yaliyofanyika Novemba 16 yaliandaliwa na KokoTEN Art Centre. Wachoraji katuni Nathan
Mpangala, Abdul King O na Said Michael 'Wakudata' waliwatabasamisha watoto wa Lushoto.
Mchora katuni, Nathan Mpangala 'kijasti' akiwafundisha watoto jinsi ya kuchora.
Abdul King O akiwapa maelekezo ya matumizi ya rangi za uchoraji.
Wachora katuni, Said Michael 'Wakudata' na Abdul King O wakijiandaa kutoa mafunzo.
Nathan Mpangala akitoa maelekezo kwa watoto waliokuwa mafunzoni.
Nathan Mpangala akitoa maelekezo kwa watoto waliokuwa mafunzoni.
Watoto wakichora michoro wakati wa mafunzo hayo.
Wachora katuni, Said Michael 'Wakudata' na Nathan Mpangala 'kijasti' wakiwafundisha watoto kuchora katuni.
No comments:
Post a Comment