![]() |
Ally Choki |
NA MWANDISHI WETU
BENDI ya muziki wa dansi ya
Extra Bongo inayoongozwa na mwanamuziki mkongwe nchini Camarade Ally
Choki ndiyo itakayopamba shindano la Redd’s Miss Pwani lililopangwa
kufanyika juni 27 2014 katika ukumbi wa Maisha Plus (Police Mess).
Mbali ya Choki ambaye atakuwa na
kikosi chake kikali cha wacheza shoo kinachoongozwa na Mussa Hassan Nyamwela
pamoja na wanenguaji wa kike kama Maria Soloma , Asha Said ‘Sharapova’ , Otilia
na wengineo watanogesha na kuacha historia siku hiyo .
Hayo yalisemwa jana jijini Dar
es Salaam na Mkurugenzi wa Kampuni ya Linda Media Solutions (LIMSO), Khadija
Kalili ambaye pia ndiyo Mratibu wa shindano hilo.
Kalili aliongeza kwa kusema
kuwa anawaahidi wakazi wa mkoa wa Pwani na wilaya zake zote kwa jumla kupata
burudani ya aina yake siku hiyo hivyo amewaomba wajitokeze kwa wingi.
Alisema katika shindano hilo warembo
kumi ndiyo watakaopanda jukwaani ikiwa ni katika kumsaka malkia wa Pwani ambaye
atauwakilisha Mkoa katika shindano la kanda ya Mashariki na baadaye
katika fainali za Redd’s Miss Tanzania 2014.
Kalili aliongeza kwa kusema kuwa
maandalizi ya shindano hilo yanaendelea ambapo pia anawataja wadhamini wa
shindano hilo kuwa ni wadhamini wakuu Redd’s Premium Cold, DIRA Media
Group, Eden Herbalist Clinic ya Jijini Dar es Salaam, CXC Africa,
Kitwe Traders, Michuzi Media Group, Jambo Concept, Bongoweekend.blogspot.com,
Maisha Plus (Police Mess) , Montage (Teddzzzzz), Filbert Bayi Foundation
(FBF).Kiingilio ni sh. 10,000.
No comments:
Post a Comment