Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel imekabidhi Gari aina ya
Toyota IST kwa mshindi wa Tatu wa droo ya kwanza Promosheni ya Airtel
Yatosha Zaidi inayofanyika kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo jumla ya magari
60 yatatolewa kwa wateja wanaotumia mtandao huo.
Gari hilo la tatu limetolea
kwa mshindi kutoka mkoani Mtwara ambaye ni mwalim mstaafu Seif
Namtapika Katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya mashujaa. Namtapika
amesema hakuweza kuamini mpaka hapo alipouliza katika ofisi za
Airtel za mkoani hapo.
“Ndugu zangu sikuamini kabisa
nilipopigiwa kuambiwa nimeshinda, wala nilikuwa sijui kama kuna siku ntamiliki
gari na tena ukizingatia mimi nimeshastaafu, kweli nawashukuru Airtel pamoja na
mungu wangu kwa kunipa zawadi hii” Alisema Namtapika .
Naye mkuu wa wilaya ya Mtwara
Mh, Willman Ndile Kapenjama aliehudhuria hafla ya makabidhiano ya gari hiyo
iliyofanyika viwanja vya mashujaa Mtwara alisema “hii ni njia bora kwa kampuni
ya Airtel kurudisha faida kwa wananchii ambao kwa kiasi kikubwa wanatumia
mtandao huo na ninawasihi endeeni kushirikiana na jamii kwa kila njia ili
kubadilisha maisha na ndoto za wateja wengi”
Nae mkuu wa Mauzo wa kanda ya
kusini Albert Majuva anasema imekuwa faraja kwa mshindi kutoka katika kanda ya
kusini kutokana na wananchii waliowengi kutumia mtandao wa Airtel.
Promosheni hiyo ya Airtel
yatosha zaidi inafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo inampa Fursa
mtumiaji wa Airtel kujipatia muda wa maongezi zaidi,idadi SMS zaidi na kumpa
mteja Internet zaidi kwa ajili ya kuperuzi awapo mahali popote na vile vile kutoa
nafasi kwa mteja mmoja kujishindia TOYOTA IST moja kila siku kwa muda wa miezi
miwili.
No comments:
Post a Comment