Katibu wa timu ya TBC Jesse John (kulia) akipokea vifaa vya
michezo mipira na viatu kutoka kwa Meneja Masoko wa Isere Sports, Abbas Ally
Issere kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya soka ya waandishi wa habari za
Michezo yanayodhaminiwa na NSSF (Picha na Mpiga Picha Wetu)
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na
Mwandishi Wetu
WAKATI
zimebaki siku chache kwa timu za waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali
vya habari kuanza kinyang'anyiro cha kuwania ubingwa wa Kombe la NSSF, timu
kongwe ya TBC imepokea vifaa vya michezo kutoka Kampuni ya Isere Sports kwa
ajili ya michuano hiyo.
Katibu
wa timu ya TBC, Jesse John alisema vikosi vyake vinajifua usiku na mchana
kuhakikisha ukongwe wao katika fani ya habari unaonekana kwa ushindi wa
uwanjani.
"Tunaishukuru
Kampuni ya Isere kwa kutusaidia vifaa vya michezo vitakavyokuwa chachu ya
kujituma kwetu kuhakikisha tunachukua ubingwa mwaka huu" alisema Jesse
John ambaye ni kipa namba moja wa timu hiyo.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Isere Soprts, Abbas Isere alisema kampuni hiyo itaendelea
kushirikiana na wadau wa michezo na kuwa mstari wa mbele kutoa vifaa vya
michezo kwa wanamichezo na pia iko mbioni kuanzisha bonanza maalum kwa wapenda
michezo hapo baadaye.
Alisema
Isere Sports ambayo ni familia ya wanamichezo inaonelea kuwa ikisaidia kuinua
michezo nchini tkaokoa maisha ya vijana watanzania ambao badala ya kukaa vijiweni
na kujiingiza kwenye biashara haramu wanaingia viwanjani kufanya mazoezi ili
kuiweka mili yao fiti.
No comments:
Post a Comment