Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Ana Bodipo Memba
(kulia), akitoa hutuba yake kwenye uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya
Wazazi Nipendeni uliofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki. Uzinduzi huo ulifanyika kwa udhamini wa Shirika la
Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Wengine ni wadau wa sekta ya Afya
waliohudhuria uzinduzi huo
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Awamu
ya pili ya Kampeni ya ‘Wazazi Nipendeni , Onyesha Upendo’ imezinduliwa Jijini
Dar es Salaam huku sasa ikijumuisha pia mwaka mmoja wa kwanza wa maisha ya mtoto.
Hii
ni kufuatia mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya kameni hiyo
iliyoandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Shirika la USAID kwa kushirikiana
na wadau wengine katika sekta ya uzazi wa afya zikiwemo kampuni za simu ambazo
zilitoa huduma ya bure ya ujumbe mfupi kutangaza kampeni hiyo.
Uzinduzi
huo ulifanywa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Dkt, Neema Rusimayila katika viwanja vya Mwembe Yanga,
Temeke Jijini Dar es Salaam.
Alisema
kampeni hiyo imesaidia kupunguza vifo vya kina mama wajawazito, watoto wachanga
na pia kuhakikisha watoto wanaozaliwa wana afya njema kwa kuhakikisha kina mama
na wenza wao wanafuata hatua zote za afya ya uzazi.
“Hapa Tanzania, idadi ya vifo vya watoto ni 51 kwa kila 1000 wanaozaliwa ambayo bado ni kubwa ikilinganishwa na malengo ya serikali kupunguza idadi hii hadi wane kwa kila 1000 wanaozaliwa,” alisema.

kutokana na idadi hii ya vifo ambayo bado inaisha kidogo, kuna haja ya
kuendelea kuweka nguvu katika kampeni hiyo na kutaka mikoa yote na halmashauri
zake kuhakikisha wanaipa kampeni hiyo kipaumbele na kuitekeleza ipasavyo ili
kuhamasisha kina mama na wenza wao kufuata hatua za afya ya uzazi.
“Tunaamini kuwa awamu hii ya pili itaharakisha patikanaji wa habari kuhusu uzazi wa afya ili kupunguza vifo huku akiongeza kuwa Chuo Kikuu cha John Hopkins pia kimeungana na Shirika la USAID na wizara pamoja na wadau wengine katika kutekeleza awamu hiyo ya pili na kuhakikisha inafanikiwa,” alisema.
Mwakilishi wa Shirika la USAID, Bi. Ana Badipo-Memba alisema wameridhika na mafanikio yaliyopaikana ndani ya miaka miwili ambayo kampeni hiyo imefanyika.

“Leo
ni muendelezo wa mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya kampeni hii
ambayo ililenga kuwahamasisha kina mama waja wazito na wenza wao kuchukua hatua
zinazotakiwa katika kuhakikisha wanazingatia uzazi wa afya na pia kujifungua
salama, alisema huku akisisitiza kuwa katika awamu ya pili kampeni hiyo pia
itajikita katika muangalia maisha ya mtoto katika mwaka wake wa kwanza.
Kauli
mbiu ya awamu hii ya pili ya Kampeni hiyo kwa mujibu wa USAID, ni ‘Onesha
Upendo wako.
Alisema kampuni za simu zitaendelea kutoa huduma ya ujumbe mfupi bure ili
kutangaza kampeni hiyo na pia zaidi ya vituo vya afya 3500 vimekubali kubandika
matangazo ya kampeni hiyo.
No comments:
Post a Comment