![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiLghcUz-dI_KZRXoyQKdJP33EffduMA1IvsZuIZDb-skWyHWg2aWnMq_LJrThbnfRyBImKpET3C8sbcvYWoHoq7dO4L6T83GZuVBkPnj1W4GBDErxs1crk-JPhfeKTJpJaVqXdE_FByes/s280/1.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjHXvNkt1BEhzX9QKQDS1q_yD_yl7ajnj6WM93ZgGf0Z_o3AErl2_jQDMtj23fB1F_nWuTPiHSq2JeyRBcxhPgAdGopn9SsxWJjTZ0R7Py9TDtZ4wydVA5fzmVhRbtVX1N70xWtQ1V0atI/s280/3.jpg)
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Mbarali,Mbeya .
SHIRIKA
la Hifadhi
za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio la kupatwa kwa jua
linalotarajia kuonekana Septemba mosi mwaka huu kufungua lango la Ikoga
katika
wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika HIFADHI
ya Taifa ya Ruaha
Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya
kuingilia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction
ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
Pascal Shelutete anasema kuongezeka kwa
geti la Ikoga ni fursa kubwa ya
kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa eneo la Ihefu
linakivutio kikubwa cha wanyama
wa aina mbalimbali .
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune, anasema
Wilaya hiyo ina vivutio vingi, hivyo
amewataka wananchi watakaofika kuangalia
kupatwa kwa jua hiyo Septemba Mosi , kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio
vilivyopo Wilayani humo.
Tukio la kupatwa kwa jua linategemea kutokea Septeba mosi
majira ya nne asubuhi hadi saa nane mchana katika kata ya Rujewa eneo la Mpunga
Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kueleka Mbeya.
No comments:
Post a Comment