Temeke wasichana wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la
uchampioni wa Airtel Rising Stars 2016. Temeke waliishinda Ilala 5-4 katika
changamoto ya mikwaju ya penati.
|
xxxxxxxxxxxxxxxx
DAR ES SALAAM
Goli pekee lililofungwa na
mshambuliaji hatari Tepesi Evans wa Morogoro lilitosha kuifanya timu hiyo kuwa
mabingwa wa michuano ya vijana chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2016
kwa kuwafunga Ilala 1-0. Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya kuvutiwa yenye upinzani
mkali ilishuhudiwa na mamia ya mashabiki akiwepo Waziri wa Habari, Sanaa,
Utamaduni na Michezo Nape Nnauye.
Baada ya kosa kosa nyingi,
Evans aliachia shuti kali mnamo dakika 77 ya mchezo, shuti ambalo lilienda moja
kwa moja na kuamsha shangwe na nderemo kutoka kwa mashabiki. Juhudi za Ilala
kuzawashisha hazikuzaa matunda mpaka mchezo unamalizika.
Mchezo huo ulikuwa ni kama
marudio ya mechi ya Alhamisi ambapo timu hizo zilikutana kwenye hatua ya
makundi huku Ilala ikitoka kichwa chini kwa kukubali kichapo cha 2-0.
Akifunga michuano hiyo ya
kila mwaka, Waziri Nnauye alisema kuwa serikali inaunga mkono juhudi za
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na wadhamini. ‘Kwa kuwapa
fursa wasichana na wavulana hawa kuonyesha vipaji vyao, ni kusaidia kubadilisha
maisha yao kwani mpira wa soka ni zaidi ya burundani – ni kufahamiana, kupata
uzoefu na zaidi, ni ajira’, alisema Nnauye.
Naye Mkurungenzi Mtendaji
Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema kampuni yake inajivunia mafanikio ya
Airtel Rising Stars yaliyopatikana miaka tano iliyopita. ‘Wachezaji ambao
waliisaidia Uganda kufuzu kwenye michuano ya AFCON 2017 Gabon ni uzao wa Airtel
Rising Stars na ni uhakika hayo yatatokea Tanzania hivi karibuni’. Alisema
Colaso huku akiongeza kuwa Airtel mpaka sasa ishawekeza Tshs2.4 billioni kwenye
michuano hiyo.
Kwa upande wake Raisi wa
TFF Jamal Malinzi alielezea michuano ya Airtel Rising Stars kama michuano ya
kutumainiwa katika kuibua vipaji. ‘Serengeti Boys na timu ya Taifa ya Wanawake
ni ushuhuda tosha wa mafainikio ya michuano hii’, alisema Malinzi.
Timu bora, wachezaji bora,
waamuzi pamoja na makocha walipewa tuzo wakati wa fainali za michuano hiyo.
Timu ya Temeke wasichana
walishinda ubingwa wa michuano hiyo kwa penati 5-4 baada ya kwenda sare ya 2-2
kwenye muda wa kawaida.
Wakati huo huo, timu ya
Temeke wavulana walishinda nafasi ya tatu ya michuano hiyo kwa changamoto ya
mikwaju ya penati ya 5-4 dhidi ya Kinondoni baada ya kutoka sare ya 0-0 kwenye
muda wa kawaida.
Kinondoni wasichana
walipata nafasi ya mshindi wa tatu baada ya kuwafunga wenzao Arusha 2-0. Magoli
yote ya Kinondoni yalifungwa na Veronica Mapunda.
No comments:
Post a Comment