Meneja Uhusiano Airtel Tanzania
Jackson Mmbando (kulia) akipata Maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa ufundi umeme
Hamadan Omary (kushoto) wakati wa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wanaopata
mafunzo ya ufundi stadi kupitia applikesheni ya VSOMO ambayo inaendesha na
Airtel kwa kushirikiana na VETA. Katikati ni mkufunzi wa Tehama VETA Kipawa
Abdul Mollel.
XXXXXXXXXXX
DAR ES SALAAM
Applikesheni ya VSOMO ambayo
inaendeshwa na kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania kwa kushirikiana na
VETA imetaja kuwa moja ya soluhisho ya Tanzania kuelekea kuwa nchi ya viwanda.
Hayo yamesemwa na mkufunzi wa
Tehama wa chuo cha VETA Kipawa Abdul Mollel wakati wa mafunzo ya vitendo kwa
wanafunzi ambao wamekuwa wakipata mafunzo ya ufundi kupitia applikesheni ya
VSOMO ambayo inalenga kuwawezesha vijana nchni kujiendeleza kielimu
kupitia application ya VSOMO kwa kupata masomo ya ufundi stadi ya VETA kupitia
simu zao za mkononi ili kuongeza ujuzi wao.
‘Tunao wanafunzi wengi hapa
Tanzania ambao wangetaka kupata elimu ya VETA. Wengine wako huko vijijini ambao
huduma zetu hazipatikani. Lakini hata hivyo inakuwa ni vugumu kwa wao wote
pamoja kupata nafasi hapa kwetu. Hata hivyo, kwa kupitia Applikesheni ya VSOMO
imekuwa ni rahisi kutimiza azma yao, alisema Mollel.
Ili kufikia malengo ya kuwa na
uchumi wa viwanda, ni muhimu kuwa na wataalam wengi wenye elimu ya ufundi
stadi. Huu mradi umekuwa ni muhimu sana kwani hata wale ambao hawana nafasi ya
kuhudhuria mafunzo ya darasani wanayo nafasi ya kusoma, aliongeza Mollel.
Wanafunzi wanapata mafunzo kupitia
simu zao za mkononi. Baada ya hapo ndio wanakuja hapa kwa ajili ya mafunzo ya
vitendo. Wengi hapa leo wanafanya mafunzo ya ufundi umeme, simu na kompyuta.
Kitu kikubwa tumeona ya kuwa vijana wanapata mafunzo kwa haraka lakini kikubwa
wanakosa kujiamini. Sisi kama waalimu ndio kitu kikubwa kwanza tunakifanya,
aliongeza Mollel.
Mafunzo ya vitendo yanachukua
takriban masaa 60 baada ya hapo tutawapa mtihani wa mwisho pamoja vyeti. Ni
vyema kwa vijana wengine huko mitaani kujiunga na applikesheni hii kwani
itawaongezea ujuzi na ufanisi zaidi, aliongeza Mollel.
Akiongea wakati mafunzo hayo ya
vitendo yakiendelea, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema
kuwa Airtel imeamua kushirikiana na VETA kutoa mafunzo ya ufundi stadi kupitia
applikesheni ya VSOMO baada ya kungundua ya kwamba kuna vijana wengi mtaani
ambao wana nia ya kupata mafunzo hayo lakini wanakosa nafasi ya kuhudhuria
darasani.
‘Tunatambua kwa Watanzania wengi
ambao wana nia ya dhati kabisa kujiunga na VETA lakini wanakosa nafasi ya
kuhudhuria darasani. Kupitia VSOMO ni fursa kwao kupata mafunzo kwa njia rahisi
na nafuu. Pia tunatambua ya kwamba serikali imedhamiria kufanya Tanzania kuwa
uchumi wa viwanda. Kuwa na vijana wengi wenye ujuzi wa fundi stadi ni moja ya
njia ya kufanikisha hilo, aliongeza Mmbando.
VSOMO imepata mafanikio makubwa
tangu kuanzisha kwake kwani mpaka sasa kuna vijana zaidi ya 30,000 ambao
wamepakua applikesheni ya VSOMO kati yao 9,000 wamejiandikisha ili kusoma kwa
mtandao. Tunatoa wito kwa watanzania hususani vijana kuchangamkia fursa hii kwa
kupakua application ya VSOMO kwenye simu zao na kusoma kozi hizi za ufundi
ambazo gharama yake ni 120,000/= hadi kumaliza na kupata cheti, alisema
Mmbando.
Kozi zinazopatikana katika
application ya VSOMO ni pamoja ni Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia
wateja, Matengenezo ya kompyuta,umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani,
Umeme wa magari. Vilevile Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi
wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo
pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.
VSOMO proves to be solution for the
country’s industrialization drive
The VSOMO application which is a
e-learning programme being implemented by Airtel Tanzania in partnership with
the Vocational Education and Training Authority (VETA) has proven to be one of
the key solutions towards the country’s drive on industrialization.
This has been said by the
VETA-Kipawa ICT Instructor Abdul Mollel during the practical sessions for the
students who have enrolled and register for courses offered by VETA through the
VSOMO application.
VSOMO application allows students
to get vocational training through their mobile phones and they only attend
classes during practical sessions.
‘We have a lot of students wishing
to get vocational training but we cannot accommodate them at once. VSOMO is now
our solution to that. The government is currently pushing for industrialization
in order to support the country’s economy. Courses offered through
VSOMO will expand the reach to studies willing to take vocational training
leading them to self-employment. More so, the courses also sharpen and equip
them with knowledge on small entrepreneurs. This is the most crucial area as
they can lead them towards on small scale industries’ said Mollel.
‘Confidence is the key for success.
Most of our students are youth who are dedicated on taking our country on next
level. We have been able to make them believe in their skills and as you can
see, most of them here have enrolled themselves for the courses in less than
six months but now they are able to perform practical’s themselves, added
Mollel.
What Airtel Tanzania has done to
support this programme clearly indicates the firm’s commitment in supporting
government initiative towards industrialization, said Mollel.
The ICT instructor said that after
the practical session which last for 60 hours, the students will be awarded
with certificates which will enable to get employment or employ themselves.
Speaking at the same event, Airtel
Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando said Airtel decided to
partner with VETA in providing vocational training skills to Tanzanians
interested in joining VETA through e-learning as they understand that there are
many of them out who want to get the skills but don’t have enough time to
attend classes.
‘VSOMO application allows students
to acquire vocational skills without physically attending to classes. All one
needs to register to the programme and pay tuition fee then will be able to
start enjoying classes even without internet buddle’s, said Mmbando.
The programme has so far attracted
over 30,000 studies that have been able to register and 9,000 out of that
number have registered for the studies. Each course is 120,000/- and a student
is issued with certificate after completion of the course.
Courses offered through VSOMO
are Cake Baking and Decoration, Catering and Food Service Techniques, PC
Maintenance, Industrial Electrical Installation, Domestic Plumbing and
Auto-electric.
No comments:
Post a Comment