|  | 
| Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza | 
Rais wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini
 Vyamhokya katikati akiongoza kuimba wimbo wa wafanyakazi wakati wa 
kikao na  wanahabari mjini  Iringa .
.................................................................................................................................................. 
Na  MatukiodaimaBlog 
WAKATI  maadhimisho ya  siku 
ya  wafanyakazi duniani  kwa 
nchini  Tanzania  yaliyoandaliwa na  shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) yakitaraji 
kufanyika  mkoani  Iringa  
kitaifa  mkuu   wa
mkoa  wa Iringa  Amina 
Masenza  amesema  mkoa 
wa Iringa  kuwa  mwenyeji wa 
mei  mosi ni  heshima 
kubwa katika  Taifa .
 Akizungumza  na  wanahabari 
leo  ofisini kwake    kuhusiana na maandalizi ya  Mei 
Mosi  Kitaifa  alisema 
kuwa  mkoa  wa 
Iringa  umeteuliwa  kuwa mwenyeji 
wa maadhimisho hayo  ambapo  mgeni 
rasmi atakuwa  ni  Rais 
Dkt  John Magufuli .
Alisema  kuwa
katika  maadhimisho hayo ya  Mei 
Mosi  kitaifa  kauli  
mbiu  ni Kuunganishwa kwa  mifuko ya
hifadhi ya  jamii kulenge  kuboresha mafao ya  wafanyakazi  na 
kuwa  kupitia maadhimisho hayo
wakazi  wa  mkoa wa 
Iringa na  wafanyabiashara  watapata  
fursa  kubwa  ya 
kujitangaza  pamoja na  kuonyesha shughuli  zao.
|  | 
| Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza akila kiapo mbele ya Rais Dkt Jonh Magufuli pindi alipoteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa | 
Katika maadhimisho hayo 
ambayo   kilele  chake 
kitafanyika  uwanja  wa Samora 
mjini Iringa  kabla ya  kilele 
kutakuwa na  michezo mbali  mbali 
kama mpira wa miguu, kuvuta kamba ,bonanza la  michezo 
tofauti  ,mpira wa pete ambayo
yote yameanza toka  April  17 hadi 
April  30 mwaka   huu .
Hata  hivyo  mkuu 
huyo wa mkoa   wa Iringa mwenyeji
wa  Mei 
mosi kitaifa  mwaka  2018 
Bi Amina Masenza alisema 
sherehe  hizo zitahusisha  maonyesho 
ya  shughuli ,huduma na  bidhaa mbali mbali  za wafanyakazi ,taasisi  za 
umma na  binafsi ,wawekezaji  na wajasiliamali  zitakazofanyika  uwanja 
wa Kichangani  Kihesa  mjini 
hapa .
Hata  hivyo  alisema 
kwa ajili ya  kuufanya mkoa wa
Iringa  uzidi  kuwa fursa kwa  wageni 
kutembelea  vivutio  vya 
utalii kama  hifadhi ya  Ruaha 
na vingine   serikali  imekaa na 
wafanyabiashara  wa  nyumba 
za  kulala wageni na  Hoteli 
ili  kuepuka  kutumia mei 
mosi  kupandisha   gharama 
za  vyumba  kwa wageni .
Bi  Masenza  amewataka  
wananchi wa  mkoa  wa 
Iringa  na  wafanyakazi 
wote   kujitokeza kwa wingi  kumlaki Rais 
wetu mpendwa  wetu Dkt  John 
Magufuli .
 

No comments:
Post a Comment