Tangazo

August 26, 2011

MAKAMPUNI YACHANGAMKIA KUDHAMINI MISS UTALII DODOMA -2011/2012

Wakati fainali za Miss Utalii Dodoma 2011/2012, zimepangwa kufanyika siku ya Jumamosi, tarehe 17-9-2011, katika ukumbi mpya wa kisasa uliopo ndani ya Royal Village Dodoma, makampuni mbalimbali ya mkoani Dodoma imethibitisha kudhamini shindano hilo kwa hali na mali.

Makampuni ambayo imethibitisha kudhamini hadi sasa ni pamoja na Asante Water, Kifimbo FM Radio, Sade Way Lodge na New Dodoma Hotel zote za Dodoma, wadhamini wengine ni Image Masters, Mlonge By Makai Enterprises, Dar City Collage na Cloud FM za Dar es Salaam, pia Tanzania National Parks (TANAPA) na Ngorongoro Conservation area Authority (NCAA) za Arusha.

Hadi sasa jumla ya udhamini wote wa hali na mali unathamani ya shilingi 21,000,000/= ikiwa ni wa hali na mali.

 Akizungumzia mwamko huo wa wafanyabiashara na makampuni ya Dodoma, katika kudhamini shindano hilo, Mkurugenzi wa Miss Tourism Tanzania Oganaizesheni, Mkoa wa Dodoma na Vyuo Vikuu Kanda ya Kati, Charles Aloyce Gabriel , alisema "hii ni dalili kuwa Dodoma sasa ina kua kwa kasi na ina wafanya Biashara na makampuni wenye hadhi ya makao makuu ya nchi na kimataifa, ambao kwa hakika, sasa wanathibitisha nia yao ya dhati ya kuunga mkono sio juhudi za Miss Utalii Tanzania tu, bali pia juhudi za Serikali ya mkoa na Tanzania kwa ujumla ya kuutangaza mkoa wa Dodoma kitalii, kitamaduni na kiuwekezaji, na kutafsiri kwa vitendo sera za Taifa za Utalii na Utamaduni, pamoja na kukuza Utalii wa Ndani na Utalii wa kitamaduni kama moja ya nyenzo madhubuti za kupambana na umasikini na tatizo la ajira nchini na Dodoma kama mkoa".

Aliwashukuru pia wadhamini hao kwa kudhamini shindano hilo na kuahidi kuwa wata watangaza kupitia shindano hilo ndani na nje ya nchi,pia aliomba makampuni na watu binafsi kujitokeza kudhamini kwani gharama za maandalizi na kufanyika kwa fainali za Miss Utalii Dodoma ni kubwa sana zinazo fikia zaidi ya  shilingi 39,400,000/- ambapo pia itakuwa fulsa kwa wadhamini hao kujitangaza kitaifa na kimataifa.

Jumla ya warembo 18, wakiwakilisha wilaya zote za Mkoa wa Dodoma, wataanza mazoezi 1-9-2011 katika hoteli ya New Dodoma Hotel, chini ya ukufunzi wa Miss Utalii Vyuo Vikuu 2010/11 – Kanda ya kati Tabia Msuta,Miss Utalii Njombe 2010/11 – Neema Isdori. Miss Utalii Tanzania 2010/11 – Mshindi wa Tano, Sophia Athuman na Miss Utalii Tanzania 201/11 – Vipaji Deissy Vedasto.

Washindi wa 1-5 na wa Vipaji watawakilisha mkoa wa Dodoma katika fainali za Miss Utalii Kanda ya Kati 2011/2012 , zitakazo fanyika mkoani Tabora mwezi Disemba 2011, na washindi wa kanda watawakilisha mikoa ya kanda ya kati katika fainali ya Taifa ya Miss Utalii Tanzania 2-011/2012, zitakazo fanyika mwezi Februari 2012 na hatamaye washindi kuwakilisha Tanzania katika fainali za Dunia za Miss Utalii dunia, Miss Umoja wa Mataifa, Miss Utalii dunia Vyuo Vikuu, Miss Urithi wa Dunia.
 
 .

No comments: