Tangazo

Tangazo

Tangazo

DIVAS PARTY GALA

August 3, 2015

Zahara Muhidin Michuzi kura hazikutosha dhidi ya Irene Uwoya - Tabora


Zahara Muhidin Michuzi akiwa nje ya ukumbi wa uchaguzi leo mapema.

Leo hii mchana binti ya mpiga picha na blogger maarufu nchini anayeambatana na rais Kikwete katika ziara zake, Muhidin Issa Michuzi Bi Zahara Michuzi alishindwa kupata kura za kutosha kumwezesha kushinda nafasi ya ubunge wa vijana kupitia tiketi ya CCM mkoa wa Tabora baada ya msanii wa filamu Bi Irene Uwoya kupata kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.


Zahara ambaye ni mhitimu wa shahada ya uchumi toka chuo kikuu cha UDOM aliyakubali matokeo hayo bila kinyongo  na kusema "Napenda kuwashukuru wagombea wenzangu na wajumbe wote, pamoja na kura mlizonipigia hazikutosha leo lakini nitabaki na azma yangu ya kuwatumikia wana Tabora" wajumbe walimshangilia sana na kumpongeza kwa ukomavu wa kisiasa aliouonesha ambapo mwenzie Mariam Shamte alisusia na kuondoka ukumbini. Mariam alimteua nduguye Hapsa kumwakilisha ktk uhesabuji kura hizo ambazo yeye Mariam alipata kura 3. Hakuingia ukumbini katika usomwaji wa matokeo.

Awali mgeni rasmi wa mkitano huo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Bw Hassan Wakasuvi aliwaeleza wajumbe kuwa Obama alizaliwa na baba raia wa Kenya na mama Mmarekani lakini leo hii anaiongoza Marekani, hivyo wasione ajabu kama pana mgombea asiyetokea Tabora kiasilia. Bila shaka alikuwa akimzungumzia Irene Uwoya ambaye kabla ya uchaguzi wakazi wengi wa Tabora walielekea kutomkubali kwa kusema kwa nini CCM ituletee mgombea toka Arusha, Moshi au Dar es Salaam, na kwa nini Irene asigombee Dar anapoishi au Kwao kaskazini? kwani Tabora hakuna vijana wenye uwezo wa kugombea? waliendelea kuhoji kuwa ni vipi Irene atayajua matatizo ya vijana wa Tabora ambao hawajui wala hana uelewa na mkoa huo? Lakini hayawi hayawi hatimaye yamekuwa kwa Irene ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho. Kama maneno ya Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Tabora yalifanya kazi kusababisha Irene Uwoya achaguliwe kwa kishindo mimi na wewe hatujui.
Zahara Michuzi akiwa na wagombea wenzie Mariam katikati na Irene (kulia).
Irene Uwoya mcheza sinema maarufu nchini alishinda uchaguzi huo kwa kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.
Mariam Shamte alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 3.
Zahara Muhidin Michuzi alishika nafasi ya 3 kwa kupata kura 2 katika kura 39 zilizopigwa.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo maalum.
Bi Mariam Amir Katibu wa UVCCM mkoa wa Tabora akisoma tamko la kuunga mkono na kupongeza kuchaguliwa Bw John Magufuli kuwa mgombea urais wa Jamhuhuri ya muungano wa Tanzania.
Katibu mkuu wa CCM mkoa wa Tabora Bibi Janeth Kayanda akisalimia wajumbe leo hii mapema.
Mwenyekiti mstaafu UVCCM wilaya ya Tabora mjini Nassor Wazambi akifuatilia mchakato.
Wagombea wakiwasalimia wajumbe wa mkutano maalumu leo mapema.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tabora Bw Seif Gulama (Kazuge) akitoa yake machache.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi akihutubia mkutano huo.
Sunday Kabaye akiwa amebeba sanduku la kura mara baada ya kura hizo kuhesabiwa nyuma akifuatiwa na Irene Uwoya na Zahara Michuzi.
Irene Uwoya akitokwa machozi kabla ya kutangazwa mshindi.
Kada wa CCM Jaha Kaducha kushoto akiwa na Mwalimu Nassoro Wazambi.

Msimamizi wa uchaguzi Bw Mwambeleko akisoma matokeo ya uchaguzi huo leo mchana mijini Tabora.
Team Irene wakifuatilia mchakato.

TAKUKURU YAKANUSHA TUHUMA ZA RUSHWA DHIDI YA NAPE

ALEX MSAMA:MAANDALIZI YA UZINDUZI WA ALBAM YA BONNY MWAITEJE YAKAMILIKA

????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu Uzinduzi wa albam ya muimbaji wa nyimbo za injili Bonny Mwaiteje utakaofanyika jumapili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, uzinduzi huo utashirikisha mwimbaji wa nyimbo za kutoka Zambia Ephraim Sekereti Faustine Munishi pia atashiriki kwenye uzinduzi huo na waimbaji wengine wengi kutoka hapa nchini.

Fedha zitakazopatikana katika uzinduzi huo zitanunua baiskeli kwa ajili ya kuwapatia walemavu katika mikoa ya Ruvuma na Morogoro ambayo haikupata katika mgao wa kwanza na pia zitanunua Chakula kwa ajili ya vituo vya watoto yatima.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DSM)
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam.
???????????????????????????????????? ???????????????????????????????????? ????????????????????????????????????

WAKRISTO WA ITALIA WAWEZESHA ZAHANATI YA KISASA VIKAWE

IMG_0282
Mkuu wa Masista Waabuduo Damu ya Kristo, Euprasia Julius akimtambulisha mgeni rasmi na meza kuu kwa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe (hawapo pichani) katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa Maria De Mathias (MDM) Vikawe, Kibaha.

Na Mwandishi wetu, Kibaha

MGANGA Mkuu wa halmashauri ya Mji Kibaha, Dk. Happniness Ndosi amepongeza shirika la masisita wa Waabuduo Damu ya Kristo kwa kufanikisha ujenzi wa zahanati ya kisasa katika kijiji cha Vikawe wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Mganga huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa zahanati hiyo,pamoja na kuwapongeza amesema serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yote kwa lengo la kuwezesha kila kijiji kiwe na zahanati na kila kata kituo na kila wilaya kuwa na hospitali.

Aliwapongeza masista hao kwa kuonesha upendo na huruma kama Biblia inavyomsimulia msamaria mwema ambaye alikuta mtu aliyepigwa na majambazi na kumsaidia.

Aliahidi ushirikiano wa serikali katika kufanikisha usajili wa zahanati hiyo na kuendelea kuisaidia hatua kwa hatua hadi inakuwa kituo mpaka watakapofanikisha safari yao ya kuwa hospitali kubwa ya kisasa.

Mganga huyo pamoja na kutoa ahadi hiyo aliwataka wananchi wa Vikawe kutumia huduma hiyo na kwamba zahanati hiyo itakapohitaji msaada wa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) wataletewa kuchukua mgonjwa na kumfikisha panapohusika.

Zahanati hiyo ya DA.MA Africa imejengwa kwa ufadhili wa wakristo wa Italia chini ya usimamizi wa Muitalia, Germano Frioni.

Akitoa salamu zake Muitalia huyo amesema kwamba anawashukuru wakazi wa Vikawe kwa kumpa nguvu ya kusonga mbele hasa kwa kutambua kwamba yeye na marafiki zake wamefanyakazi usiku na mchana kutafuta fedha kwa ajili ya kusaidia marafiki wa Afrika.
Alisema atajitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha changamoto za zahanati hiyo zinafanyiwa kazi.

Aliwaomba wananchi wa Tanzania kuendelea kumuombea yeye na wenzake kama Papa Francis anavyoagiza ili malengo ya safari ya kuwapo duniani yafanikiwe.

Alisema kwamba watoto wake Daniel na Marco (kwa sasa wote ni marehemu) ambao ndio kifupi cha zahanati hiyo DA.MA wamemfanya kujitambua na kusaidia wengine katika kuonesha upendo.
Aidha alisema kwamba ataendelea kukumbuka Vikawe kwani alifika mara ya kwanza mwaka 2005 na kuona hali ilivyokuwa ambapo sasa lipo jengo la zahanati hiyo likiwa limekamilika.

Wazo la ujenzi wa zahanati hiyo , lilitolewa na wananchi wa Vikawe kwa Masisita Waabuduo Damu ya Kristo mwaka 2004 wakati wakiwa katika eneo hilo baada ya kununua ekari 40 kwa ajili ya kilimo mwaka 1994.

Alisema pamoja na maombi hayo na wao wenyewe kutambua kwamba kuna mahitaji makubwa ya huduma ya afya japokuwa kuna zahanati ya serikali, hawakuweza kutekeleza maombi ya wanavijiji hadi mwaka 2011 walipofanikiwa kupata ufadhili kutoka Italia na kuanza ujenzi mwaka 2013.

Katika risala yao walisema kwa ushirikiano kati yao na wafadhili hao wamefanikiwa kuwapo kwa zahanati hiyo yenye mahitaji yote ya msingi kwa mujibu wa taratibu za serikali na kuzidi.

Msoma risala alisema kwamba wataendelea kupanua miundombinu mpaka zahanati hiyo ifikie ngazi ya cha afya na baadae hospitali.

Pamoja na ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa masisita hao wameanzisha shule ya awali kuwaandaa wanafunzi wa darasa la kwanza.

Wamesema kwamba wanaamini kwamba wataendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa afya katika kuimarisha huduma za hospitali hiyo.

Zahanati hiyo pamoja na vifaa tiba pia ina raslimali ya visima vya maji ya mvua ujazo zenye ujazo wa lita laki moja na kingine lita 49 elfu, wanatumia umeme wa sola na jenereta.

Walisema kwamba wanachangamoto ya kukosa umeme wa Tanesco, barabara nzuri na nyumba za wafanyakazi.
IMG_0289
Mwenyekiti wa kijiji cha Vikawe, Kibaha, Shabaan Mgini akiwasalimia wageni waalikwa wakati wa utambulisho.
IMG_0301
Sr. Theresia Rogatus akisoma risala katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa DMD iliyopo Vikawe, Kibaha.
IMG_0323
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa -DMD kijiji cha Vikawe, Kibaha. Kutoka kushoto ni Mdau wa Zahanati hiyo, Dr. Zuberi Mzige wa Hospitali ya Mwananyamala,
IMG_0335
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi akimpa mkono wa shukrani Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Raia wa Italia, Germano Frioni kwa ujenzi wa Zahanati hiyo itakayohudumia wakazi wa kijiji cha Vikawe, Kibaha.
IMG_0341
Masista Waabuduo Damu ya Kristo wakielekea meza kuu kwa mwendo wa madaha huku wakiwa wamebeba zawadi kwa ajili ya kumkabidhi mgeni rasmi na wafadhili waliojitolea kujenga Zahanati hiyo.
IMG_0348
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi (kulia) akimkabidhi zawadi Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Raia wa Italia, Germano Frioni. Anaye shuhudia tukio hilo ni Baba Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Kalmeri Bunju...
IMG_0351
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi akikabidhi zawadi kwa wadau waliombatana na Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Muitalia, Germano Frioni.
IMG_0354
IMG_0194
Mganga Mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dr. Happniness Ndosi (wa pili kulia) pamoja na Mfadhili wa ujenzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa ya kijiji cha Vikawe, Kibaha, Muitalia, Germano Frioni wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Zahanati hiyo inayosimamiwa na Masista Waabuduo Damu ya Kristo nchini.
IMG_0230
Muonekano wa ndani ya Zahanati ya Da. Ma Africa-DMD iliyop Vikawe, Kibaha mkoa wa Pwani.
IMG_0211
Mganga Mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dr. Happniness Ndosi akiangalia chumba cha dawa katika Zahanati hiyo mara baada ya kuzinduliwa.
IMG_0235
Wageni waalikwa wakijadiliana jambo mara baada ya kufungiliwa rasmi Zahanati hiyo nje ya moja ya chumba cha upasuaji mdogo.
IMG_0128
Baba Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Kalmeri Bunju akiendesha ibada takatifu ya misa maalum kabla ya ufunguzi rasmi wa Zahanati hiyo.
IMG_9973
IMG_0089
Wanakijiji wa Vikawe wakishiriki ibada maalum wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Da. Ma Africa.
IMG_0126
IMG_0086
IMG_0265
Kwaya ikitoa burudani.
IMG_0017
Wageni waalikwa na wanakijiji wakishiriki kuimba pamoja na kwaya.
IMG_0102
Pichani juu na chini ni baadhi ya wanakijiji na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
IMG_0140
Umati wa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe.
IMG_0361
Mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wafadhili waliojenga Zahanati hiyo.
IMG_9898
Masista Waabuduo Damu ya Kristo wakifurahia taswira za picha za mnato kutoka kwenye kamera.
IMG_0224
Jenereta la Zahanati ya Da.Ma Africa linalotumika kutoa umeme katika Zahanati hiyo.
IMG_9881
Muonekano wa nje wa jengo la Zahanati ya Da.Ma Africa kabla ya kuzinduliwa rasmi.
IMG_0247
Wanakijiji wa Vikawe na wageni waalikwa wakiingia kukagua Zahanati hiyo mara baada ya kuzinduliwa.