Tangazo

October 23, 2017

Airtel Timiza Vikoba suluhisho tosha kwa vikundi vya akinamama

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Airtel Money  Bw, Isack Nchunda akiongelea mafanikio na mikakati yao katika kuikuza na kuieneza huduma ya ‘Airtel Money Timiza vikoba’ jinsi inavyotoa suluhisho kwa akinamama na vikundi mbalimbali vya Vikoba nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Bw, Ibrahimu Mwangalaba akitangaza mafanikio ya huduma ya Timiza vikoba inayotolewa na kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Banki yake kwa kufikia mafanikio ya kutoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini wiki hii.
xxxxxxxx
·   Kwa sasa ndio njia rahisi na nafuu kwa vikundi vya Vicoba kupata mikopo.
·  Kusambaa nchi kote hivi karibuni.

Huduma ya Airtel Timiza vikoba imeendelea kuwa suluhisho tosha kwa makundi ambayo yanataka kuweka akiba na kujipatia mikopo ili kuendesha biashara zao vizuri.

Makundi mengi ya Vikoba sasa hivi yameamua kutumia huduma ya Airtel Timiza Vikoba kwani imewasaidia kuweka utaratibu mzuri huku serikali ikitaka vikundi vya vikoba visambae zaidi nchini ili watu wengi waweze kufaidika.

Hivi karibuni akizindua mradi wa vikoba katika eneo la Bunju Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi aliwataka viongozi wa vikoba kuhaikisha wanatanua mitandao yao ili wananchi wengi zaidi wafaidi.

“Natoa wito kwa viongozi wa Vikoba kuhakikisha wanatanua mtandao wao wa vikoba nchinzima ili watu wengi zaidi waweze kufaidi,” aisema Mkuu wa Wilaya.

Airtel Timiza Vikoba imekuwa gumzo kubwa sasa hivi hasa baada ya kampuni ya Airtel kushirikiana na Benki ya Maendeleo kuhakikisha Vikoba vinakuwa rasmi zaidi na vinafanya shughuli zake kwa umakini zaidi tofauti na hapo mwanzo.

“Hadi sasa tangu mradi huu uanze imeshatolewa mikopo 487 yenye thamani ya Tsh milioni 20.5 kwa wanachama wa vikoba,” alisema Ibrahim Mwangalaba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo.

Alisema jumla ya wateja 5,685 wameshajiunga na mfumo huu na kuunda makundi huku akaunti mpya 1,1810 zikifunguliwa. Alitoa wito kwa wanachama zaidi kujiunga na mfumo huo kwani ndio imekuwa suluhisho tosha kwa matatizo yanayokumba vikundi vingi vya vikoba.

Tangu mradi huu uzinduliwe, makundi 18,166 yenye wanachama 178, 638 yameshasajiliwa Mwangalaba aliongeza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko na huduma ya Airtel Money wa Airtel Tanzania Isack Nchunda alisema wanajivunia kwa kuweza kuleta suluhisho na sasa hivi wamelenga kuhakikisha malengo ya serkali ya kuhakikisha kunakuwepo na vikoba nchi nzima yanatimia kikamilifu.

“Makundi mengi ya vikoba yalikuwa yanapata shida hasa katika kuweka kumbukumbu na wakati mwingine vitabu vyao hupotea hivi kuwafanya washindwe kuwa na kumbukumbu sahihi. Wengine walikuwa wanatunza fedha kwenye vibubu, chini ya magodoro lakini huduma hii itawasaidia kuweka akiba zao vizuri kupitia Airtel Money ambapo wanachama wote wanaweza kufuatilia,” alisema huku akiongeza kuwa mwenyekiti tu ndiye mwenye mamlaka ya kuwa na nywila wanachama wanatumiwa ripoti tu.

Alisema huduma hii pia imesaidia kuimarisha uwazi katika makundi ya vikoba na Airtel itaendelea kufungua milango zaidi ili kuhakikisha watu wengi zaidi hasa wafanyabiashara wadogo wanapata huduma sahihi za kifedha.

Airtel Timiza Vikoba ilizinduliwa miezi mitano iliyopita ikiwa na lengo la kusaidia makundi mbalimbali kufikia malengo yao.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Airtel Timiza Vikoba best solution to groups
·   Timiza Vikoba a quick solution for women Vicoba groups to acquire loans
      - Set to roll out countrywide

Airtel Timiza Vikoba project has continued to be the best solution so far especially for most groups that want to save and acquire small loans to run their businesses.
This comes in the wake of most groups opting to use the Airtel Timiza Vikoba service which has helped them to be more organized in terms of their operations at a time when the government is also advocating for an increase in the Vikoba network around the country to ensure more small scale business people benefit.

Recently, while launching a Vikoba project at Bunju in Dar es Salaam, the Kinondoni District Commissioner, Ally Hapi called on Vikoba leaders to ensure they expand their networks so that more people can benefit from this service to improve their businesses.

“Am calling on Vikoba leaders to ensure they expand their network all over the country so that more business people can benefit,” said the DC.

Airtel Timiza Vikoba service is now the talk in town as Airtel teamed up with Maendeleo Bank to ensure more Vikoba groups become formal and operate in a more organized way.

“So far since this project was launched a total of 487 loans worth tsh 20.5 million have been disbursed to different Vikoba members,” said Maendeleo Bank Managing Director Ibrahim Mwangalaba.

He said cumulatively 5,685 unique customers have joined and created groups with 1,810 new accounts opened at Maendeleo Bank and appealed to more members to use the Timiza Vikoba service as it has proved to be the best solution for the well-being of their groups.

Since the launch, Mwangalaba says 18,166 unique groups have started their registration on the system with a potential of 178,638 group members.

Airtel Tanzania Marketing Director Isack Nchunda Said they were proud to be seen as a solution to the Vikoba problems that most groups were experiencing and their focus is to ensure the government’s target to have more parts of the country covered by Vikoba is well achieved.

“Most groups were struggling to keep records in books and at times they lose them and cannot keep track of their balances, some kept money in boxes, others under mattresses and so on but with Airtel Timiza Vikoba all this has changed as all savings are kept in Airtel Money where all members can trace the balances,” he said adding that only the chairman has the password but members receive updates.

‘“We are happy to see this great response which indicates that our customers are pleased with this innovative service that is aimed at enhancing and simplifying transaction activities for Vikoba groups of between 5 and 100 members’, added Nchunda.

He said this has enhanced a lot of transparency among Vikoba groups and that Airtel will continue opening more doors to ensure more people especially small scale businesses get proper financial services in their groups.

Airtel Timiza Vikoba was launched with the aim of helping groups realize their dreams in a more effective way.

Airtel's Timiza Vicoba was launched five months ago with the aim of helping groups realize their dreams in a more effective way.


No comments: