Tangazo

January 23, 2018

Tigo yamwaga Mamilioni kwa Mawakala


Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari (katikati) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 15 mshindi wa promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa, Roida Kipinya mkaazi wa Newala, Mtwara katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Tigo Pesa,  Hussein Sayed. Jumla ya mawakala 73,000 wa Tigo walishiriki  katika promosheni hiyo


Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari (katikati) akimkabishi mfano wahundi ya shilingimilioni 10 mshindi wa pili katika promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa,Mojelwa Mlinga  mkaazi wa Pugu Mnadani, Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Hussein Sayed. Jumla ya mawakala 2,281 wa Tigo Pesa walipata zawadi mbali mbali katika promosheni hiyo iliyodumu kwa kipindi cha mwezi  mmoja.

Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani, George Lugata akimkabidhi mfano ya hundi ya shilingi milioni  2 mshindi wa kanda katika promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa, Vicky Ibrahim katika hafla iliyofanyika  katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi  Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari. Jumla ya Mawakala nane (8) wa Tigo Pesa walipata zawadi za TSH 2 milioni na shilingi 1  milioni kila mmoja baada ya kuibuka washindi katika kanda zao. 

Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari (aliyevalia tai katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi wa  promosheni ya Mawakala wa Tigo Pesa pamoja na wafanyakazi  wengine wa Tigo katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni hiyo. Roida Kipinya wa Newala, Mtwara aliibuka mshindi wa kitita cha shilingi milioni 15, huku Mojelwa Mlinga wa Pugu Mnadani, Dar es Salaam akijinyakulia shilingi milioni 10 katika promosheni hiyo iliyojumulisha mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo Pesa nchi nzima.  

Wakala wawili wa Tigo Pesa wajinyakulia TZS 15 milioni na TZS 10 milioni kila mmoja.
Tigo pia yatoa mamilioni ya fedha kama bonasi na zawadi kwa mawakala 2,281.  

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali Tanzania, Tigo leo imegeuza mawakala wawili wa Tigo Pesa kuwa mamilionea katika promosheni yake iliyofika tamati leo.

Roida Kipinya, Wakala wa Tigo Pesa kutoka wilaya ya Newala, mkoani Mtwara aliyepokea kitita cha TZS 15 milioni kutoka Tigo amesema, ‘Nimejawa furaha kubwa kwa kupokea zawadi hii kubwa kutoka Tigo Pesa kama shukrani kwa juhudi zangu za uwakala. Sasa nitaweza kukamilisha mahitaji yangu muhimu ya nyumbani pamoja na kupanua biashara zangu.’

Kwa upande wake, Mojelwa Mlinga wa Pugu Mnadani jijini Dar es Salaam ambaye ameshinda TZS 10 milioni katika promosheni hiyo iliyodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja, aliielezea promosheni hiyo kama ya kwanza na ya kipekee kuwahi kutolewa na mtandao wowote ule wa simu kwa mawakala wake nchini.

Akiongea na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya Tigo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Bw Simon Karikari alisema kuwa nia kuu ya promosheni hiyo ilikuwa ni kurudisha shukrani kwa mawakala wa Tigo Pesa katika kipindi cha sikukuu na Mwaka Mpya.  ‘Nina imani kuwa tumefanikisha malengo na ndoto za mawakala wetu katika kipindi,’ alisema.

Naye Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed alisema kuwa Tigo imetoa zawadi na bonasi kwa mawakala 2,281 kutoka sehemu mbali mbali za nchi. ‘Pamoja na bonasi hizi kubwa, leo  Tigo pia inatoa zawadi za shilingi milioni mbili na shilingi milioni moja kwa mawakala nane kutoka sehemu mbali mbali za nchi,’ aliongeza.  

Hussein alibainisha kuwa jumla ya mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo Pesa walishiriki katika promosheni hiyo kote nchini. ‘Tunajivunia mchango wetu mkubwa katika kurahisisha upatikanaji wa huduma rasmi za kifedha kwa watu wote nchini. Kupitia mtandao wetu mpana na uhakika wa mawakala wa Tigo pesa, tunaiwezesha jamii kutuma, kupokea na kufanya miamala ya fedha yenye mchango mkubwa katika uchumi wa watu binafsi, biashara, nchi na jamii yote kwa ujumla. Tigo Pesa ni zaidi ya huduma ya kutuma na kupokea pesa. Ni sehemu ya maisha.’

Tigo Pesa ni huduma ya fedha ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini.

Kampuni ya Tigo ilianza kutoa huduma nchini Tanzania mwaka 1995 na kwa miaka mitatu mfululizo ndiyo kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini.  Kwa sasa Tigo ndio kampuni ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini inayohudumia wateja zaidi ya 11.6 milioni.

Tigo ni kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini na inatoa huduma bora za kipekee za sauti, SMS na intaneti ya kasi ya juu ya 4G inayopatikana katika miji 24 nchini kote. Tigo pia inafahamika kwa promosheni kabambe na ofa bunifu kwa wateja wake.

No comments: