Mbunge wa
jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa akiongea na baadhi ya walimu wa shule za sekondari na shule za msingi jinsi gani ya kutatua kero zilipo shuleni ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi
Mbunge wa
jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa akiwakabidhi zawadi ya mbuzi kwa walimu wa shule za msingi waliofanya vizuri katika moja ya kata iliyopo jimboni kwake.
Na Fredy Mgunda, Iringa
Wananchi wa jimbo la Mufindi
kaskazini wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule kwa lazima kwa kuwa elimu
inatolewa bure na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Mafuli kwa lengo la kuhakikisha kila mwanafunzi
wote waweze kupata elimu na kuondoa ujinga na kuleta maendeleo kwa taifa.
Hayo yamesemwa na mbunge wa
jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa alipokuwa kwenye ziara ya kukagua
miundombinu ya shule zilizopo katika jimbo hilo ili kuweza kuzitatua changamoto
zilizopo katika maendeo hayo.
Akiwa bado yupo kwenye ziara
hiyo mbunge huyo aligundua kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwanzo cha kuwapeleka
shule watoto wa hivyo akawataka viongozi wote wa serikali za vijiji kuwa
chukulia hatua wazazi ambao hawatawapekeka shule watoto wao.
Mgimwa alisema kuwa yupo tayari
kunyimwa kura na wananchi ambao atawachukulia hatua za kisheria kwa kutowapeleka
shule watoto wao kwa ajili ya faida ya
maisha yao.
“Nasema kweli nitakubali
kuachia ngazi ya kuwa mbunge kwa kunyimwa kura za wananchi wasiopenda maendeleo
ya watoto wao,hadi sasa shule zimefungua lakini wazazi hawawapeleki shule
watoto nitahakikisha wanachukuliwa hatua za kisheria” alisema Mgimwa
Aidha Mgimwa
alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuwa
soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo
baadae.
“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika
daresalaam utasikia katoka Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini sasa sitaki kusika
swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali
ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya
nchi”alisema Mgimwa
Mgimwa alisema kuwa wazazi wa jimbo la Mufindi
la Mufinda watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi
wamalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza maendeleo yao.
“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi
anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubali hata kidogo maana nimegundugua
wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka
wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule
nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Mgimwa
Mgimwa aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya
ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya
maisha wakiwa watoto wadogo na kufanya hivyo kutawapelekea kufungwa jela kwa
kuwa sheria itachukua mkondo wake.
“Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa
“Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa
Mgimwa
aliwapongeza walimu wa shule za msingi za jimbo la Mufindi Kaskazini kwa
kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza
vizuri jimbo hilo kupitia elimu.
“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii
kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua
katika jimbo la Mufindi Kaskazi na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Mgimwa
nao baadhi ya walimu wakuu wa shule zilizopo jimbo la Mufindi Kazskazini walisema kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.
“Hapa katika kata hii ya Kibengu wazazi wengi
hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao
mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi
kusoma kwa uhuru” alisema walimu
Walimu walimuomba mbunge wa jimbo la Mufindi
Kaskazini kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi ili kukuza
taaluma kwa wanafunzi wa kata hiyo.
“Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hizi ni
mzuri lakini kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu wamekuwa
hawawapeleki watoto wao sekondari wakifaulu mitihani ya shule ya msingi hivyo
inapelekea upungufu wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya Ilogombe” alisema
Walimu.
Mfikwa alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano
ya mara kwa mara lakini bado tatizo kubwa hivyo jitihada zinahitajika kukomesha
tabia hiyo kwa kuwa bila hivyo watoto wa kata hiyo wataendelea kuwa wafanyakazi
za ndani tu
Zakayo Kilyenyi ni diwani wa kata ya Kibengu alikiri
kuwa wazazi wengi wa kata hiyo hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya
elimu katika maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.
“Kweli kabisa wazazi wa kata ya Kibengu wamekuwa
wakiwaambia watoto wasifanye mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa wakifaulu
watakuwa na gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda kuwafanya kazi
za ndani na ndio furaha kwa wazazi wa kata ya Kibengu” alisema Kilyenyi
Kilyenyi alisema kuwa uongozi wa kata ya Kibengu
utaendelea kutoa elimu kwa wazazi hao ili kurudisha morali ya kuendelea kuwapa
mahitaji muhimu yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la kuboresha maisha ya
watoto hao.
“Zana potofu zimekuwa kikwazo kikubwa sana
katika maendeleo ya wananchi wa kata ya Kibengu hivyo tukiondoa zana hiyo elimu
itakuwa kwa wanafunzi wa kijiji hichi” alisema Kilyenyi
No comments:
Post a Comment