Meneja Miradi Airtel
Tanzania Jane Matinde akizungumza wakati wa semina kwa vijana kuhusu umuhimu wa
kusoma kwa kutumia mtandao kupitia aplikesheni ya VISOMO inayotumiwa na VETA
kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika makao makuu ya
kampuni hiyo Morocco, Dar es Salaam.
Dar es Salaam
Takribani wanafunzi 10,000 tayari wameshajiandikisha na
masomo ya ufundi ya VETA kupitia application ya VSOMO ili kusoma kozi
mbalimbali za ufundi nchini. Mafunzo hayo ya ufundi ya VSOMO yanapatikana
kupitia simu za mkononi kwa ushirikiano kati ya kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel na mamlaka ya mafunzo ya ufundi stadi (VETA) yamekuwa nikichocheo
kikubwa katika upatikanaji wa elimu kwa njia ya mtandao na kuongeza idadi ya
wanafunzi wanataraji na wanaosoma masomo ya ufundi katika nyanja mbalimbali
nchini.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam kuhusu program hiyo, Kaimu Mkuu wa chuo cha ufundi cha VETA Kipawa, Bw. Harold
Mganga alisema mafunzo ya ufundi ya muda mfupi yamekuwa yakitolewa na
katika vyuo cha VETA kwa miaka mingi na hivyo idadi ya wanafunzi kuongezeka
kila mwaka.
Aidha alisema kuwa kwa kuliona hilo VETA ikaona ni
vyema kutanua wigo kwa kushirikiana na Airtel ili kutoa mafunzo haya kwa njia
ya mtandao ili kuwawezesha vijana katika maeneo mbalimbali hususani maeneo ya
pembezoni au walio katika shughuli zao za kazi kupata nafasi ya kusoma
masomo ya nadharia kupitia simu zao mahali popote wakati wotote kisha kufanya
mafunzo ya vitendo katika vyuo vyetu vya VETA mara baada ya kafaulu mitihani
yao.
“Najisikia fahari kusema kuwa ushirikiano wetu na
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel umekuwa na tija kubwa katika kuwafikishia
watanzania wote mafunzo haya kwa urahisi na ufanisi mahali popote nchini”,
alisema Bw. Mganga.
Mpaka sasa wanafunzi 9975 wamejiandikisha kupata
mafunzo haya na Zaidi ya watanzania elfu 33 wameshapakuwa application ya VSOMO
kupitia simu zao za mkononi. Kwetu sisi haya ni mafanikio makubwa na tuaamini
kuwa mapinduzi haya ya elimu kupitia mtandao ndio yatakayoleta tija na
kutuwezesha kuwa na nguvukazi yenye uledi ili kwenda sambamba na mahitaji ya nchi
katika kufikia uchumi wa viwanda kwani nguvukazi ni moja kati ya nguzo muhimu
katika kuendesha viwanda hivyo.
Kwa upande wake Meneja Mradi wa VSOMO Airtel, Bi
Jane Matinde alisema “ Tunayo mikakati mingi mwaka huu itakayowezesha
watanzania wengi hususani vijana kuvutiwa na kujiunga na masomo haya ikiwemo
kuongeza idadi ya kozi, kutoa elimu kwa uma juu ya upatikanaji wamasomo haya,
kuboresha namba yetu ya kituo cha simu cha VSOMO ya 0699859573 na0699859572 na masaa ya kupata huduma
na vilevile kutanua wigo wa upatikanaji wa huduma hii na kuboresha malipo
ya ada pamoja na mikakati mingi zaidi.
Lakini pia mkakati tulionao mpaka kufikia
mwezi wa februari mwisho mwaka huu tutazindua kozi tano mpya ambazo
ni pamoja na kozi ya usafi, kutengeneza Keki, kuoka mikate, ufugaji wa
kuku pamoja na upambaji wamaua.
Mpaka sasa tunazo kozi kumi na moja ambazo tayari
tumeshazizindua na zinapatikana katika application hiyo ya VSOMO ambazo ni
pamoja na kozi ya Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo
ya kompyuta,umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa magari,
kutengeneza na kupamba keki, ufundi wa simu, ufundi pikipiki, Utaalamu saluni
na urembo, ufuni wa kuchomelea pamoja na ufundi wa Aluminium.
Tunaamini upatikanaji wa kozi mbalimbali
kutawezesha watanzania wengi kujiunga na kusoma masomo haya na kutanua wigo wa
wanafunzi wengi zaidi kusoma na kupata vyeti kila mwaka. Tunatoa wito kwa
vijana , wazazi na walezi kutumia mfumo huu kujiendeleza nakupata ujuzi zaidi
aliongeza Matinde
Mpaka sasa mikoa minayoongeza kwa kuwa na
mwitikio mkubwa wa wanafunzi kujiandikisha ni pamoja na Dar es saalam, Mwanza ,
Arusha, Morogoro na Dodoma huku vijana toka mikoa 26 nchini wamejiandikisha na
mafunzo haya.
1 comment:
Namba zenu na mm natafuta chuo hicho
Post a Comment