Tangazo

December 21, 2016

WAZIRI MUHONGO AIPONGEZA KAMPUNI YA ACACIA KWA KUWA KAMPUNI YA KWANZAYA MADINI KUWA NA HATI FUNGANI



Kwa mujibu wa Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Migodi nchini, (Acting Chief Inspector of Mine), Mhandisi Noel Baraka, alisema, nijukumu la kisheria kwa migodi yote nchini, ya kati na mikubwa kuandaa mpango wa kufunga mgodi ambao shughuli hiyo inasimamiwa na kamati ya kitaifa ya kusimamia shughuli za ufungaji migodi (National Mine Closure Committee).

Kamati hiyo inaundwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishatina Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira, (NEMC), Wizara ya Maliasili na Utalii , Wizara ya Maji na Umwagiliaji, National Land Use Planning Commission, viongozi wa Serikali ya mkoa na Wilaya ulipo mgodi husika.

Mhandisi Baraka alifafanua kuwa Kampuni ya Acacia, iliandaa mipango ya ukarabati wa mazingira pindi shughuli za uchimbaji zitakaposimama na gharama zinazohusiana na ukarabati huo wamigodi yake mitatu ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara.


“Chini yamkatabahuu, dhamana (bonds) ya gharama za ukarabati kwa mgodi wa Bulyanhulu, ni Dolaza Kimarekani 3,287,714, Mgodiwa North Mara ni Dola za Kimarekani 19,164,344 na Mgodi wa Buzwagi ni Dola za Kimarekani 18.628,489.” Alifafanua
“Sheria hii, kampu ni ya uchimbaji madini inapaswa kuweka hati fungani (rehabilitation bonds) kwenye kampuni ya bima au benki, ili shughuli za uchimbahji zinapo koma kwa sababu yoyote ile, basi fedha hizo ziweze kutumika kukarabati mazingira ya eneo la shughuli ya uchimbaji nakuyarejesha katika hali bora na salama.” Alisisitiza.

Kwaupande wake, Mshauri Mkuu wa Mazingira wa Kampuni ya Acacia, Bi. Rebecca Stephen, alisema kampuni yake imefurahi sana kufikia hatua hiyo ya kusaini mkataba huo, kwani  ni hakikisho kwamba fedha tayari zimetengwa kwaajili ya shughuli hiyo.

“Kazi hii ilikuwa na mchakato mrefu uliochukua takribani  miaka miwili, na ulianza kwa kuandaa mpango wa ufungaji mgodi na gharama zake, na kupitiwa na Wizara na kamati nzima na kupitishwa.” Alisema

Alisema Kampuni ya Acacia katika utekelezaji wa shughuli zake, inazingatia siku zote kutii sheria za nchi na tukio la leo nimoja ya vielelezo, alisema Bi. Rebeca.

“Sheriayamadini ya 2010 inahitaji kuwepo na hakikisho kutoka kwetu ya namna gani tutakarabati mazingira pindi shughuli za uchimbaji zitakaposimama na kuhakikisha pesa za kufanya ukarabati huo zipo,”  alisema na kuongeza Acacia imetekeleza hiyo sheria tukiwa ndio kampuni ya kwanza kufikia hatua hii, alisema Bi. Rebecca.



Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (kulia), na Makamu wa Rais wa Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (anayeshughulikia kampuni), Bw. Deo Mwanyika, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa hati fungani makao makuuya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Acacia imekuwa kampuni ya kwanza ya uchimbaji madini nchini, kutekeleza sheria ya madini ya mwaka 2010 inayotaka kila kampuni kuwasilisha mpango wake wa ukarabati wa mzingira na kuweka bond fedha pindi shughuli za uchimbaji zinapokoma. Wanaoshuhudia ni wanasheria wa Wizara na kampuni ya Acacia


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (kulia), na Makamu wa Rais wa Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (anayeshughulikia kampuni), Bw. DFeo Mwanyika, wakitia saini mkataba wa hati fungani makao makuuya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Acacia imekuwa kampuni ya kwanza ya uchimbaji madini nchini, kutekeleza sheria ya madini ya mwaka 2010 inayotaka kila kampuni kuwasilisha mpango wake wa ukarabati mzingira na kuweka bondi fedha pindi shughuli za uchimbaji zinapokoma.

 Profesac Muhongo, (kulia), akimsikiliza Bw. Mwanyika mwanzoni mwa hafla hiyo ya kutia saini, mkataba wa hati fungani
 Waziri Muhongo (kushoto), akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo
Makamu wa Rais wa Acacia, Bw. Deo Mwanyika, (kulia) na Mshauri Mkuu wa Mazingira wa kampuni hiyo, Bi. Rebeca Stephene, wakipitia nyaraka hizo kabla ya kusaini
Makamu wa Rais wa Acacia, Bw. Deo Mwanyika, (kulia) na Mshauri Mkuu wa Mazingira wa kampuni hiyo, Bi. Rebeca Stephene, wakipitia nyaraka hizo kabla ya kusaini

  Waziri Muhongo (kulia), akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo
 Waziri Profesa Muhongo, akitia saini mkataba huo wa hati fungani
Makamu wa Rais wa Acacia, Bw. Deo Mwanyika akitia saini mkataba huo wa hati fungani

No comments: