Tangazo

Showing posts with label Uchumi. Show all posts
Showing posts with label Uchumi. Show all posts

April 20, 2018

SERIKALI YAANZISHA MPANGO WA KUTOA MAFUNZO KWA VIJANAKUKIDHI MAHITAJI YA VIWANDA VYA NGUO


Mhe. Charles J. Mwijage (Mb), Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal, NFRA
Baadhi ya wakuu wa mikoa inoyozalisha Pamba kwa wingi wakifatilia mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Mgeni-Rasmi Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, Mhe. Charles J. Mwijage (Mb), akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt Mary Mwanjelwa akijadiliana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Waziri wa kilimo, Mhe. Dkt Charles Tizebawakati akifatilia kwa makini mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Baadhi ya  wadau wa sekta ya pamba wakifatilia kwa makini mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.

Na Mathias Canal, Dodoma

Serikali kwa kushirikiana na viwanda vya nguo na mavazi imeanzisha mpango maalum wa kutoa mafunzo ya ushonaji kwa vijana kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya viwanda vya nguo.

Upatikanaji wa ujuzi wa aina hiyo utapunguza gharama kwa wawekezaji na kuongeza ufanisi katika uzalishaji. Vilevile, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kupitia msaada wa Gatsby Africa, kimeendelea kutoa mafunzo ya Shahada ya Teknolojia ya Nguo (Textile Degree) ambapo, mwaka 2016/2017, Chuo kilitoa wahitimu 44 ikilinganishwa na wahitimu 13 kwa mwaka 2015/2016. Lengo ni kuhakikisha kuwa kuna wataalam wa kutosha wa fani ya ubunifu na uzalishaji mavazi nchini.

Hayo yamebainishwa na Mhe. Charles J. Mwijage (Mb), Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, wakati akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018
Alisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazozalisha pamba kwa kiasi kikubwa barani Afrika, ikiwa na zaidi ya wakulima 500,000 wanaolima pamba katika eneo linalokadiriwa kufikia hekta 412,000 katika mikoa 13 nchini. Sekta ya nguo na mavazi ni moja ya sekta za Kipaumbele katika kusukuma gurudumu la maendeleo nchini na inahusisha mnyororo mrefu wa uongezaji thamani kuanzia kuchambua pamba (ginneries); kusokota nyuzi (spinning); kuseketa vitambaa (weaving); kufuma vitambaa (knitting), kuchapa na kutia rangi (processing) na kushona mavazi (garments).
Aliongezaa kuwa Sekta hii ni moja ya sekta muhimu katika kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuanzisha viwanda vinavyoajiri watu wengi kwa wakati mmoja. Sekta hii itawezesha kupunguza uingizaji wa nguo kutoka nje na kuongeza matumizi ya pamba inayolimwa nchini pamoja na malighafi nyingine zinazopatikana nchini kama vile magadi na gesi asilia.
Hata hivyo, Serikali imeendelea kuzishawishi taasisi za Umma kwa kuanzia majeshi na hospitali ili wanunue nguo na mavazi yanayozalishwa na viwanda vya ndani.  Lengo ni kuhakikisha kuwa utaratibu wa makusudi unawekwa kwa Taasisi za umma kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu hapa nchini. Kwa mfano uvaaji wa fulana aina ya Polo Shirt kwa wafanyakazi wote katika siku moja ya wiki, na pia wanafunzi wote shule za msingi na sekondari kuvaa sare hizo. Inakadiriwa kuwa kuna jumla ya wanafunzi milioni 15 na wafanyakazi wa sekta zote za umma wanafika 25,000.
Mhe Mwijage alisema kuwa Utengenezaji wa fulana moja ya polo unakadiriwa kutumia wastani wa gramu 300 za pamba, sketi moja inakadiriwa kutumia gramu 600 za pamba, kaptula moja inakadiriwa kutumia gramu 600 za pamba. Hivyo jumla ya gramu 900 za pamba zitahitajika kutengeneza sare kwa mwanafunzi mmoja awe wa kike au wa kiume.
Kama ikikadiriwa kila mwanafunzi atavaa wastani wa sare (sketi & shati au kaptula na shati) mbili tu kwa mwaka gramu 1800 (sawa na kilo 1.8) za pamba zitahitajika kwa mwanafunzi mmoja, hivyo wastani wa kilo 27,000,000 (sawa na tani 27,000) zitahitajika kwa mwaka. Endapo mahitaji yaliyokusudiwa yakipitishwa tunategemea kwamba viwanda vya ndani vitakuwa na uwezo wa kutumia asilimia 17 ya pamba yote inayozalishwa nchini kwa mwaka. Hii itahamasisha uzalishaji wa pamba, kuongeza ajira na kuongeza kipato.
“Serikali inakamilisha taratibu za kuidhinisha ‘’ Blue Print’’   ambayo imeainisha maeneo ya kufanyia maboresho ya Kisera na Kisheria ili kuhamasisha uwekezaji katika Sekta mbalimbali za uchumi ikiwemo sekta ya pamba nguo na mavazi” Alikaririwa Mhe Mwijage

Pia,aliwashukuru Wadau wa sekta ndogo ya pamba, nguo na Mavazi kwa kazi kubwa wanayofanya katika uzalishaji, biashara na wadau wengine kwa michango yao katika kuendeleza sekta hii. 

Mkutano huo umehusisha Wizari ya Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara wa Fedha na Mipango, Wizara ya Kilimo; Waheshimiwa Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge za Viwanda, Biashara na Mazingira; Bajeti; Kilimo, Mifugo na Maji; na Uwekezaji Mitaji ya Umma, Wakuu wa Mikoa; Makatibu Wakuu, Wawakilishi wa Sekta Binafsi, Maafisa wa Serikali na Taasisi za Serikali.

April 11, 2018

SERIKALI YAWAONYA WAFANYABIASHARA WA BIDHAA ZA MAGENDO MKOANI TANGA




MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya Mamlaka hiyo kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim




Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya Mamlaka hiyo kulia Afisa Mtekelezaji Mkuu wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa



PRO wa Bandari ya Tanga Moni Jarufu akizungumza wakati akiwakaribisha wageni kwenye sherehe hizo zilizofanyika kwenye viwanja v ya Bandari Jijini Tanga


Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akifuatilia matukio mbalimbali kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia ni Afisa Mtekelezaji Mkuu wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire
Afisa Tehama wa Bandari ya Tanga Ally Isaka akimueleza kitu Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo katikati ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Bandari leo akiwa ameambatana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Tanga (OCD) Jumanne Abdallah na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akisalimiana na wafanyakazi wa Bandari ya Tanga

Sehemu ya wafanyakazi wa Bandari ya Tanga wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Sehemu ya wafanyakazi wa Bandari ya Tanga wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

Zoezi la utoaji wa damu likiendelea kwenye sherehe hizo

SERIKALI mkoani Tanga imesema kuwa haitakuwa na simile na wananchi watakaokamatwa kujihusisha na kuingiza bidhaa za magendo kupitia bandari bubu kwani wanachangia kuikosesha mapato serikali.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya Mamlaka hiyo.

Alisema kuwa kumekuwepo na wimbi kubwa la wafanyabiashara wasio waaminifu kutumia bandari bubu kupitishia bidhaa za magendo ambazo sio salama kwa matumizi ya binadamu.

“Katika hili hatutakiwa na msamaha wala kumuonea mtu haya tukikukamata chombo tutakitaifisha pamoja na mali zake huku muhusika atachukuliwa hatua kali za kisheri nilazima wananchi wajifunzi kuona umuhimu wa kutumia bandari rasmi”alisema DC Mwilapwa.

Aidha aliitaka Mamlaka ya usimamizi wa bandari Mkoani Tanga kuhakikisha utendaji kazi wao unaendana na kasi ya maboresho ya bandari hiyo unaofanywa na serikali kwa sasa.

Awali Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama alisema kuwa maboresho ya vifaa na vitendea kazi katika bandari hiyo yameweza kusaidia kuongeza ufanisi wa kuhudumia shehena za mizigo kutoka siku kumi hadi nne.

Alisema kuwa kuhudumia shehena za mizigo katika kipindi kifupi kumesaidia kupunguza gharama kwa wateja wanaohudumiwa na bandari hiyo . “Licha ya kuhudumia mizigo kwa awamu mbili lakini uwepo wa vifaa umesaidia kuboresha uwezo wa bandari yetu ya kuhudumia mizigo kwa ufanisi zaidi”alibainisha Mkuu huyo.

Sherehe hizo zinakwenda sambamba na kauli mbiu Bandari za TPA ni chachu ya uchumi Viwanda na Ustawi nchini Tanzania (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

March 7, 2018

WAJIBU WA WACHIMBAJI WADOGO NI KUFUATA MAELEKEZO YA SERIKALI NA KULIPA KODI KWA UAMINIFU

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwaeleza wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Bululu, kilichopo katika Kata ya Nyamtukuza Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita juu ya umuhimu wa kufuata taratibu na sheria katika uchimbaji, Jana 6 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Bululu, kilichopo katika Kata ya Nyamtukuza wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita, Jana 6 Machi 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwaeleza akisisitiza jambo wakati aliokuwa akihutubia wananchi wakati akiwa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita, Jana 6 Machi 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kulia) na Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale Mhe Hussein Nassor Amari Kasu (Kulia) wakisikiliza kero za wananchi wakati wa ziara ya kikazi Wilaa ya Nyang'wale Mkoani Geita, Jana 6 Machi 2018.

Na Mathias Canal, Geita

Serikali imesema kuwa imedhamiria kuwanufaisha wananchi wake kupitia rasilimali za nchi hususani sekta ya Madini hivyo jukumu la Wachimbaji hao ni kufuata maelekezo ya serikali ikiwemo taratibu na sheria katika uchimbaji.

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ametoa rai hiyo Jana 6 Machi 2018 wakati akizungumza na wachimhaji wadogo katika Kijiji cha Bululu, kilichopo katika Kata ya Nyamtukuza Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita.

Alisema kuwa Serikali tayari imetenga maeneo maalumu kwa wachimbaji wadogo katika mkoa wa Geita na maeneo mengi nchini huku akisisitiza kuwa kuna leseni za utafiti na uchimbaji mdogo 20 ambazo zinaisha muda wake 30 Machi mwaka huu katika Wilaya ya Nyang'wale hivyo wananchi wanapaswa kuwa wavumilivu katika kipindi hicho kwani serikali inatazama namna ya kuwapatia wachimbaji wadogo baadhi ya maeneo hayo.

Mhe Biteko alisisitiza hayo wakati akijibu maswali ya wachimbaji wadogo waliohudhuria mkutano wa hadhara na kuiomba serikali kuwapatia maeneo rasmi kwa ajili ya uchimbaji kwani katika kipindi kirefu wamekuwa wakizuiwa kuchimba katika maeneo mbalimbali ambayo yana leseni za uchimbaji.

Alisema kuwa serikali itatoa leseni kwa ajili ya maeneo ya uchimbaji lakini haitatoa leseni hizo kwa mtu mmoja mmoja badala yake amewasihi wachimbaji hao kuanzisha vikundi ili kupatiwa leseni hizo.

Mhe Biteko pia alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wwale Mkoani Geita Mhe Hamim Gwiyama kuitisha kikao ndani ya wiki moja kwa kuwaalika wananchi wote wenyewe vikundi ili kuwaelekeza namna bora ya kufanya kazi za uchimbaji kwa kufuata taratibu na sheria.

Aidha, amewataka Wachimbaji hao Mara baada ya kupewa maeneo ya uchimbaji kuwa waaminifu kwa serikali yao kwa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kuboresha huduma za maendeleo ikiwemo sekta ya Afya, elimu na miundombinu.

February 5, 2018

NAIBU GAVANA WA BoT DKT. BANZI AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUTANGAZA KWA KINA JITIHADA ZA SERIKALI ZA KUJENGA UCHUM

 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Julian Raphael Banzi, akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha kwa waandishi wa habafri za Uchumi, Biashara na Fedha, mkoani Mtwara leo Februari 5, 2018.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mtwara
WAANDISHI wa Habari za uchumi na Fedha, wameaswa kutumia kalamu zao vema ili kuongeza tija katika jitihada za serikali za kujenga uchumi wa viwanda nchini ifikapo mwaka 2025, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt.Julian Raphael Banzi amesema leo Februari 5, 2018 wakati akifungua semina ya waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha kwenye ukumbi wa BoT , mkoani Mtwara.
“Waandishi mnao wajibu wa kuamsha ari ya uelewa kwa wananchi kuwaelimisha nini serikali inafanya kwa ajili ya nini na kwa utaratibu upi.” Alisema Dkt. Banzi na kuwaasa badala ya waandishi kutumia muda mwingi kuandika maswala ambayo hayasaidii sana katika kusaidia ujenzi wa uchumi, ni vema sasa wakaangazia katika kuelimisha umma juu ya jitihada za serikali wakati huu ambapo kuna utekelezaji wa miradi mbali mbali ya kiuchumi kama vile jenzi wa reli ya kisasa, (SGR).
Naibu Gavana pia amewataka waandisjhi wa habari kuwafichua wale wanaokatisha tama au kukwamisha uwekezaji nchini kwani kwa kutofanya hivyo waandishi wa habari watakuwa hawawatendei haki wananchi na umma kwa ujumla.
Alisema kuwa BoT inaposema pato la taifa limeongezeka, haimaanishi kwamba wananchi wanajazwa pesa mfukoni lakini pia mwananchi inabidi ajiulize yeye mwenyewe anashiriki vipi katika ujenzi wa uchumi ili kuweza kufaidika na pato lenyewe.
“Kwa msingi huo elimu mtakayopata hapa katika kipindi cha siku tano, itawaongezea uwezo wa kufanya uchambuzi wa kina mnapoandika makala ze uchumi, biashara na fedha ili ziweze kuufikia umma kwa usahihi na kuepuka upotoshaji.” Alisema Dkt. Banzi.
Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Itifaki cha BoT, Bi. Zalia Mbeo, alisema semina hii ni ya tano ambazo BoT imekuwa ikifanya kila mwaka, ili kujenga uelewa kwa waandishi kuweza kuandika kwa usahihi shughuli za BoT.
“Tumezidi kuona mafanikio makubwa tangu tuanze kutoa semina kwa waandishi wa habari kwa waandishi wamekuwa wakijitahidi kuandika kwa usahihi taarifa za BoT.” Alisema.
Bi Mbeo pia alisema katika semina ya mwaka huu, waandishi watapata fursa ya kuelimishwa mambo mbalimbali kutoka Kurugenzi ya sera na tafiti za uchumi, kurugenzi ya masoko ya fedha, kurugenzi ya usimamizi wa ,mabenki, kurugenzi ya huduma za kibenki na kurugenzi ya mifumo ya malipo, na pia kuna ushiriki kutoka kurugenzi ya bima ya amana.
“Mwaka huu tuna kurugenzi ya Katibu wa Boadi ambayo itaelezea dawati ambalo linashughulikia matatizo ya watu wanayoyapata katika huduma mbalimbali za kibenki, na kwa kupitia waandishi wa habari, tunategemea wataelimisha umma kuhusu dawati hili.” Alisema Bi. Mbeo.


 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Julian Raphael Banzi, akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha kwa waandishi wa habafri za Uchumi, Biashara na Fedha, mkoani Mtwara leo Februari 5, 2018. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Itifaki, Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Zalia Mbeo na Mwenyekiti w aSemina, Bw. Ezekiel Kamwaga,
 Baadhi ya waandishi wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye warshan hiyo
 Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Itifaki, BoT, Bi. Zalia Mbeo, akielezea maudhui ya semina hiyo ambayo itafanyika kwa siku tano kuanzia leo Februari 5, 2017.
 Meneja wa tawi la Benki Kuu ya Tanzania Mkoani Mtwara, Bw.Lucas Mwimo, akitoa hotuba ya ukaribisho

 Bi.Vicky Msina, kutoka Kitengo cha Uhusiano na Itifaki BoT. akizunguzma mapema wakati wa ufunbguzi wa warsha hiyo.
  Bi.Vicky Msina, kutoka Kitengo cha Uhusiano na Itifaki BoT. akizunguzma mapema wakati wa ufunbguzi wa warsha hiyo.
 Baadhi ya washiriki

 Mwenyekiti wa Warsha hiyo, Bw. Ezekiel Kamwaga akitoa hotuba yake.


 Dkt. Banzi akipeana mikono na Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uchumi BoT, Bw, Johnson Nyella

 Dkt. Banzi, (katikati), Bi Zalie, na Bw.Mwimo





  Maafisa waandamizi wa BoT.
 Mkurugenzi wa Uchumi BoT, Bw, Johnson Nyella, akitoa Mada ya Mabadiliko ya mfumo wa kuandaa sera ya fedha, ambapo pa,moja na mambo mengine alisema pato la taifa ni mjmuiko wa thamani ya vitu vyote vilivyozalishwa katika uchumi kwa kipindi husika.
Meza kuu

January 19, 2018

MHE BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUTAMBUA UMUHIMU WA KULIPA KODI

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza jambo wakati wa mkutano na wachimbaji wa madini ya Jasi na Chumvi Mkoani Mtwara, Leo 19 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Wachimbaji wa madini ya Jasi na Chumvi Mkoani Mtwara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa Mkutano wa pamoja na wachimbaji hao kwenye ofisi za Madini Kanda ya kusini, Leo 19 Januari 2018.
Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Kanda ya kusini Ndg Peter Ludovick akieleza kero za wachimbaji mbele ya Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa mkutano na wachimbaji wadogo, Leo 19 Januyari 2018.

Na Mathias Canal, Mtwara

Wizara ya Madini imesisitiza wachimbaji wadogo na wakubwa nchini kutambua umuhimu wa ulipaji kodi kwa kila wanachozalisha kwani itasaidia kuongeza pato la Taifa kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi ikiwemo ukarabati wa miundombinu, Ujenzi na uimarishaji Wa sekta ya afya, elimu, Sekta ya umeme na sekta ya maji.

Akizungumza Mkoani Mtwara wakati wa mkutano na wachimbaji wa madini ya Jasi na Chumvi Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesema kuwa jamii bado haina elimu ya kutosha juu ya ulipaji kodi hivyo ofisi za madini nchini zinapaswa kuongeza msukumo Wa utoaji elimu juu ya ulipaji kodi na utunzaji wa kumbukumbuku za shughuli za uvunaji Madini kwa kila mahali kwenye leseni.

Mhe Biteko alisema kuwa wachimbaji wadogo kote nchini wanapaswa kutambua kuwa hawatakiwi kusalia kukwepa kodi badala yake wanapaswa kutoka kwenye uchuuzi na hatimaye kuhamia kwenye ufanyabiashara na kuhifadhi taarifa zote kwa mujibu wa kanuni kwa kipindi cha miaka 5.

Alisema kuwa mtu yeyote anapoitwa mfanyabiashara anatambulika katika jamii na serikali kwa ujumla wake hivyo kigezo kikubwa na muhimu kwa mfanyabiashara ni kulipa kodi kwa mujibu Wa kanuni, sheria na taratibu.

Akizungumza kwa msisitizo Mhe Biteko alisema kuwa watanzania wamempata Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuongoza Taifa akiwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitano hivyo wanapaswa kuunga mkono juhudi za utendaji wake kwa kulipa kodi kwa manufaa ya jamii nzima.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Wa Madini ameupongeza uongozi Wa Ofisi ya Madini Kanda ya Mtwara kwa ushirikiano mzuri na wachimbaji jambo ambalo limeimarisha utendaji wao pasina malalamiko dhidi ya serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti Wa Chama Cha wachimbaji Mkoa Wa Mtwara Ndg Festo Balegele akizungumza wakati Wa mkutano huo alimsihi Naibu Waziri wa Madini kutilia mkazo uongezaji thamani wa chumvi inayozalishwa nchini kwa kuikausha (Drying) na kuisaga (Grinding) sambamba na kuongeza Madini joto kwani itapelekea serikali kuokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumiwa na serikali kuagiza chumvi nje ya nchi.

Alisema kuwa kila mwaka jumla ya tani 350 za chumvi huagizwa nje ya nchi ambapo ikiwasili nchini inauzwa kwa shilingi 500 kwa gramu 500 sawa na shilingi 50,000 kwa kilo 50 kiasi ambacho ni kikubwa Mara tano ya gharama za chumvi inayozalishwa nchini kwani inauzwa kwa shilingi 5000 kwa kilo 50.

Alisema kuwa chumvi inayoagizwa nje ya nchi ni kiasi cha Tani 350,000 kila mwaka huku akisisitiza kuwa serikali ingetilia mkazo na kuboresha miundombinu nchini ingerahisisha upatikanaji wa chumvi nyingi nchini ambayo inauzwa kwa kiasi kidogo chenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya watanzania.