Tangazo

September 24, 2013

Tanzania Wasichana mabingwa mashindano ya kimataifa Air Rising Stars


Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Nigeria, Segun Ognsanya (katikati) akiwakabidhi Nahodha wa timu ya Wasichana Tanzania na Kocha wa timu hiyo, Rogacian Kaijage zawadi za ushindi mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika.

Mwakilishi na kiongozi wa Airtel Tanzania, Bi Lilian Kibiriti akifurahia ushindi na Wachezaji wa timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Nigeria, Segun Ognsanya Katikati akiwakabidhi kombe Nahodha wa Timu ya Wasichana Tanzania, Stumai Abdallah  mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika jana jijini Lagos Nigeria.
 *********************
Timu ya wasichana ya Tanzania imeibuka mabigwa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yaliyokuwa yanafanyika mwaka huu  nchi Nigeria.

Tanzania ilipata ubigwa huo baada ya kuchuana vikali na timu ya Kenya katika mechi ya Fainali  na kuifunga Kenya goli moja bila na kuibuka mabingwa . Donisia Daniel ndio alipeleka furaha kwa upande wa Tanzania.

Tanzania ilikua kundi moja na Sierra-Leone , Malawi , na Uganda. Walishinda mechi moja dhidi ya Sierra-Leone 2-1 , wakapoteza mchezo dhidi ya Uganda na kutoka sare na Malawi 1-1.

Wakashinda 4-2 katika mikwaju ya penati dhidi ya DRC katika robo fainali mechi zilizopigwa katika uwanja wa NIS Sports. Na wakawatoa Uganda kwa mvua ya magoli 8-1

Mbali na ushindi huo wa wasichana watanzania walijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo , Mchezaji bora kwa upande wa wasichana Tatu Iddi, Mfungaji bora wa mashindano kwa upande wa wavulana Athanas Mdam na Mfungaji bora kwa upande wa wasichana Shelda Boniface

Kwa upande wa wavulana Timu ya Niger wametetea tena ubingwa  baada ya kuifunga Zambia kwa mikwaju ya penati 7-6  katika mechi ya fainali ya Airtel Rising Stars ilifanyika kweny uwanja wa Agege nchini Nigeria.

Niger wamefanya vizuri kuanzia hatua ya makundi  baada ya kushinda michezo yote katika makundi na kufikisha magoli 12 na kuruhusu magili matatu tu katika mechi sita . Jumla ya mechi 58 zimechezwa katika mashinda

Aidha timu ya wavulana ya Tanzania imeshikilia nafasi ya nne kati ya timu zaidi ya 16 zilizoshiriki michuano hiyo

Michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu yamefanyika nchini Nigeria katika viwanja vinne Agege, Township Stadium, Legacy Pitch, National Institute for Sports Fiels na  Main bowl .

Kulianza na “ gala night” jumapili usiku ikafatia  sherehe za ufunguzi , na mechi za ufunguzi za makudi katika uwanja wa AgegeTownship .

Mashindano ya kiamataifa ya umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya pili , mashindano haya yamekua bora kwa vijana wadogo na kwakuzingatia jinsia.


No comments: