Daktari
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Dennis David
akimpima mkazi wa Jiji la Tanga Octaviani Moshiru kwenye banda lao
lililopo kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho
ya sita ya biashara ya kimataifa
Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Dennis
David akimpima mkazi wa Jiji la Tanga Octaviani Moshiru kushoto
akimsikiliza kwa umakini mkazi wa Jiji la Tanga
Daktari
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Lawi Kupaza
akimpa ushauri mkazi wa Jiji la Tanga mara baada ya kupima afya.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Hillary Ngonyani akisaini kitabu cha
wageni mara baada ya kutembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) lililopo kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika
Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Korogwe Jumanne Shauri kulia ni Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina
Clemens anayefuata ni Afisa Masoko na Elimu kwa Umma Makao Makuu Hawa
Duguza
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Korogwe Jumanne Shauri kushoto akisaini kitabu cha
wageni kulia ni Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens anayefuata
ni Afisa Masoko na Elimu kwa Umma Makao Makuu Hawa Duguza
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Jumanne Shauri kushoto akizungumza na
maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tanga kulia ni
Afisa Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens anayefuata kushoto ni
Afisa Masoko na Elimu kwa Umma Makao Makuu Hawa Duguza
Afisa
Matekelezo wa Mfuko huo Macrina Clemens kulia akisisitiza jambo kwa
wananchi waliofika kwenye banda lao kupata elimu ya mpango wa kujiunga
na bima ya Afya
Katibu
Tawala wa mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi akiwa na tisheti
akijiandaa kuwapa watoto zawadi wakati alipotembelea banda hilo kushoto
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Ally
Mwakababu
sehemu ya watoto waliojiunga na mpango wa Toto Afya kadi
NA MWANDISHI WETU, TANGA.
WATANZANIA wametakiwa kujiunga na
mpango wa bima a Afya ili waweze kunufaika na huduma za matibabu ya
uhakika wakati wanapokuwa wakiugua na hivyo kuwapunguzia mzigo wa
kuingia gharama kubwa.
Hayo yalisemwa leo na Afisa Masoko na
Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) Makao Makuu Hawa
Duguza wakati akizungumza kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
kunakoendelea maonyesho ya biashara ya kimataifa.
Licha ya mfuko
huo kutoa elimu juu ya umuhimu wa mpango wa bima lakini pia wanaendelea
kutoa huduma za upimaji wa afya na kutoa ushauri kwa wananchi ambao
wamekuwa wakifika kwenye banda lao lililopo kwenye maonyesha hayo.
Alisema
mpango wa bima ni mzuri kutokana na kuwapa uhakika wa matibabu wakati
wanapokuwa wakikumbana na maradhi mbalimbali na hivyo ni muhimu kujiunga
nao ili waweze kuona manufaa makubwa wanayoweza kuyapata.
Aidha
pia aliwahamasisha kujiunga na mpango wa kikoa na toto Afya kadi ambazo
ni muhimu kwa ajili ya kuweza kupata huduma nzuri kipindi ambacho
wanapatwa na changamoto za kuugua hususani watoto wadogo wakati wa
ukuaji wao.
“Ndugu zangu maradhi huwezi kujua yanakuja lini hasa
kwa watoto wadogo wakati wa ukuaji wao hivyo niwasihi muone njia nzuri
ya kuwawekea akiba ya matibabu kwa kuwaingiza kwenye mpango huu wa toto
afya kadi kwani hii ni kumuhakikisha mtoto wako huduma wakati wote
wanapougua”Alisema.
Alisema pia jamii haiwezi kupata maendeleo
ikiwa watakuwa hawana afya bora hivyo ni muhimu kuendelea kuhamasishana
kujiunga na mpango huo kwa lengo la kuweza kunufaika na huduma za
matibabu (habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
No comments:
Post a Comment