Tangazo

Showing posts with label Burudani. Show all posts
Showing posts with label Burudani. Show all posts

June 6, 2018

Itazame Simulizi mpya iliyopewa jina la ‘Kinyago’

Kwa  nafasi ya upendeleo New Talents tunachukua fursa hii kukupa nafasi ya kwanza kuitazama hii video ya Simulizi mpya iliyo beba ujumbe mkubwa unaotakiwa kuwafikia Wanadamu, kwani Dunia inamambo mengi  ndio maana wengi wanajikatia tamaa kwa kuikosa thamani yao hapa Duniani.

Amini na kwambia Dunia bila changamoto haiwezi kunoga, ndio maana kila kukicha tumekuwa tukikutana na changamoto za hapa na pale kama vifo,ajali na manyanyaso.

 New Talents Tanzania Crew tunakuletea Simulizi ambayo imepewa jina la ‘KINYAGO’ Simulizi hii imegusa pande nyingi  katika maisha ya wanadamu, imeandikwa na Mrembo Rose Peter Maarufu kwa jina la ‘PUKUU’ chini ya usimamizi wa Director Mr.Super News  tunaomba Support yako katika kuufikisha ujumbe uliyomo ndani ya Simulizi hii kwa jamii Asante. 

May 15, 2018

MSANII DIAMOND AZINDUA WIMBO WA COLOURS KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI


Msanii Diamond akipagawisha mashabiki wa Soka waliohudhuria katika Uzinduzi wa wimbo wa Colours maalum kwa ajili ya kombe la dunia 2018 linalofanyika nchini Urusi.
Mkurugenzi wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios akiongea machache kuhusu hafla hiyo,(kushoto) ni Meneja wa Coca-Cola nchini, David Karamagi.
Mkurugenzi wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios akikata keki wakati wa hafla hiyo. Msanii Diamond akisalimiana na Mameneja Waandamizi wa Coca-Cola. Msanii Peter Msechu na bendi yake wakipagawisha mashabiki wa soka waliohudhuria katika uzinduzi wa wimbo maalum alioshirikishwa msanii Diamond utakaosheresha Kombe la Dunia 2018.

Na Mwandishi Wetu.

MSANII wa Bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewapagawisha vilivyo mashabiki wake wakati akiimba wimbo maalum utakaosherehesha Kombe la Dunia 2018 wimbo uitwao Colours nyimbo aliyoshirikiana na Jason Derulo, katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 

 Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo, alisema kampuni ya Coca-Cola Tanzania ni moja ya mdhamini wa mashindano hayo makubwa ya soka duniani na inayofuraha kwa msanii kutoka Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano hayo na kwamba anaimani watanzania watapata mzuka wa soka dimbani na kujisikia sehemu ya mashindano.

April 26, 2018

MSANII DIAMOND KUTUMBUIZA KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI

 Msanii Diamond akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es alaam (katikati) ni Sealouise Shayo, Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini (kulia) ni Meneja wake Sallam SK.
 Msanii Diamond na Nahreel katika mkutano wa waandishi wa habari, wengine ni maofisa wa Coca-Cola na mameneja wa msanii Diamond.
Maofisa wa Coca-Cola wakiwa katika picha ya pamoja na Diamond na Nahreel baada ya mkutano na waandishi wa habari. Msanii nguli wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz, kwa kushirikiana na kampuni ya Coca-Cola ametangaza kuwa ameshiriki kuimba wimbo utakaosherehesha Kombe la Dunia 2018 uitwao Colours. 

Wimbo huo uliotungwa na mwanamuziki Jason Derulo wa Florida, Marekani, Diamond ameshiriki kuweka maudhui ya lugha ya Kiswahili na umetayarishwa na prodyuza Nahreel kwa kushirikiana na maprodyuza kutoka nchi nyingine chini ya udhamini wa kampuni ya Coca-Cola. 

 Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema anayo furaha kupata fursa ya kushiriki kuimba kuimba wimbo wa mashindano haya makubwa ya kidunia na kuitangaza Tanzania na lugha ya Afrika bila kusahau tasnia ya muziki kwa ujumla. 

 “Kwangu hii ni nafasi nyingine ambayo najivunia kuipata ya kutangaza muziki wa kitanzania sambamba na lugha ya Kiswahili kwa kuwa sehemu niliyoshiriki kuimba nimetumia lugha ya taifa la Tanzania ambayo inazidi kupata umaarufu mkubwa duniani”alisema Diamond. 

 Kwa upande wake Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo, alisema kampuni ya Coca-Cola ambayo ni moja ya mdhamini wa mashindano haya makubwa ya soka duniani inayo furaha kwa msanii kutoka nchini Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano haya. 

“Tuna imani watanzania watapata mzuka wa soka dimbani na kujisikia sehemu ya mashindano haya”alisisitiza. Prodyuza nguli wa muziki nchini na kanda ya Afrika Mashariki, Nahreel, ambaye ameshiriki kutengeneza wimbo huu aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa jitihada mbalimali ambazo imekuwa ikifanya kuwanyanyua wasanii wa hapa nchini ambapo mbali na Diamond naye ameshiriki kwenye tukio hili kubwa. 

“Ninayo furaha ya kufanya kazi na Diamond kwa mara nyingine katika tukio hili kubwa la mashindano ya Kombe la Dunia na najivunia heshima kubwa tuliyopewa”

April 11, 2018

BONGO MOVIE KUIBUA VIPAJI VIPYA NA KUHUBIRI AMANI, UPENDO NA UZALENDO TANZANIA

Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza ambaye ni Mratibu wa Tamasha la Iringa ya Kwetu, Kijana Amka tufanye kazi, Steve Nyerere akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea Tamasha la 'Iringa ya Kwetu, Kijana Amka tufanye kazi,' Pembeni (kushoto) ni Msanii Shamsa Ford na kulia ni Msanii Wolper.
Wasanii waliohudhuria utambulisho wa Tamasha la 'Iringa ya Kwetu, Kijana Amka tufanye kazi.
Msanii wa maigizo na filamu nchini, Single Mtambalike maarufu kwa jina la Richie akifafanua machache. Na Mwandishi Wetu. Kundi la Wasanii wa Muziki, Bongo Fleva, Mziki wa Singeli na Filamu nchini wanataraji kutoa elimu ya kujikwamua kiuchumi vijana wa Iringa katika Viwanja vya Mwembe Togwa mkoani Iringa. 

 Akizungumza wakati wa utambulisho wa Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza ambaye ni Mratibu wa Tamasha la Iringa ya Kwetu, Kijana Amka tufanye kazi, Steve Nyerere amesema kuwa Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya 'Kijana wa Iringa inuka tukafanye kazi,'.

 “Tunataka tuwaonyeshe vijana kuwa huyu Wolper, JB au Steve Nyerere awakuwa wasanii maarufu moja kwa moja bali kuna maisha walipitia mpaka kufikia hapo hivyo wanatakiwa kufanya kazi ili waweze kufikia mafanikio kutoka kijiweni na kuwa wajasilimali kama walivyo hawa wasanii wakubwa” amesema Steve. 

 Kwa upande wake Msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini, Msanii maarufu wa Bongo Movies Jacob Steven 'JB amesema wanafika Iringa kwa lengo moja tu la kuhakikisha wanaonana na wasanii na vikundi vya Iringa kwa lengo la kutaka kuwainua kitaaluma kwa kuwapa uzoefu ambao wameupata kwa zaidi ya miaka 20. 

 Amesema tunajua kuna wasanii wengi sana huku mikoani lakini je ni muda gani wanapata nafasi hivyo wanakwenda Iringa na wataacha mabalozi ambao ndio watakuwa maharufu katika kizazi kijacho cha filamu. 

 Kwa upande wake Msanii maharufu wa kike wa filamu nchini, Jackline Wolper amesema umaharufu hauzuii kufanya mambo ya msingi kama ujasiliamali ili aweze kujiongezea kipato. Amesema kuwa licha ya kuwa maarufu bado amekuwa akijihusisha na ufundi cherehani kama sehemu ya kujiongezea kipato katikamaisha yake ya kila siku.
Msanii Jackline Wolper akifafanua machache.
Mwenyekiti Steve akitoa ya Moyoni.

February 7, 2018

MAMA MITINDO AELEZA UKWELI KUHUSU KUSTAAFU KUANDAA LADY IN RED!


Baada ya tetesi kuvuma zilizo jaa ukweli kuhusiana na Mama wanamitindo maarufu hapa Tanzania, Asya Idarous Khamsin kustaafu kuandaa jukwaa la ‘Lady In Red, sasa leo  6/Feb/2018 Asya amedhibitisha  tetesi hizo kama ifuatavyo.

 Akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa King Solomon Asya amesema kuwa Jukwaa la Lady in Red mpaka sasa limedumu kwa muda wa miaka 15 likiwa chini yake.  Pia alifafanua  dhamira ya jukwaa la Lady in Red ambapo alisema jukwaa hilo lilianzishwa kwa lengo la kukuza vipaji vipya kwenye Tasnia ya Mitindo hapa Tanzania, ndio maana jukwaa asilimia kubwa huwa linapandisha upcoming Designers maana ndio jukwaa lao la kujidaia.

Aidha aliongeza kuwa kustaafu kuandaa jukwaa la Lady in Red haimaanishi kwamba ataachana na mambo ya ubunifu, “siwezi kuacha maana ndio kazi inayo niweka mjini” alisisitiza Asya.  “Kilicho kikubwa nimeamua kutoa fursa kwa wanamitindo ambao wamekulia kwenye jukwaa hilo”.

Kumbuka Lady in Red 2018 itafanyika 9/Feb/2018 katika ukumbi wa King Solomon uliopo Dar es salaam- Namanga. Siku hiyo ndipo Asya atakapo jivua kuandaa na kukabidhi Designers wengine jukwaa hilo usikose. Kwako mdau wa mitindo endelea kuisambaza kwa walimwengu wote asante.


November 27, 2017

Kilele cha Tigo Fiesta 2017 yatikisa Jiji la Dar


Msanii Madee kushoto akiwa na Janjaroo na TundaMan kwa pamoja kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam usiku wa kuamkia jana.


Ommy Dimpozi akiwa kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia jana

 Ommy Dimpozi akiendelea kuburudisha katika  jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia jana

Alikiba akiwa na kundi lake wakitumbuiza katika jukwaa la Tigo fiesta liliofanya hitimisho lake usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam.

Vanessa Mdee akiwa na dansa wake wakitoa burudani kwa maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika usiku wa jana  viwanja vya leaders.

Fid q akitoa burudani katika jukwaa la Tigo  fiesta jijini Dar es salaam katika kilele chake kilichofanyika katika viwanja vya Leaders.

Mashabiki wa muziki wakifurahia  burudani mbalimbali zilizotolewa katika kilele cha Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam.

Fid Q akiendelea kuburudisha katika Jukwaaa la Tigo Fiesta .


Mwanamziki Mkongwa wa BongoFleva Afande sele akiwa  katika jukwaaa la Tigo fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders jijini Dar es salaaam.

Maua Sama akiwa na kundi lake akitumbuiza katika kilele cha Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders .

Benpol akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana 


Wasanii Kassim Mganga na Jux wakishirikiana kuimba pamoja kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam juzi.

Richie Mavoko akiwa na kundi lake akitumbuiza katika kilele cha tigo fiesta usiku wa kuamkia jana.

Chege Chigunda akipagawisha maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliojitokeza katika viwanja vya Leaders katika kilele cha Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana.

November 23, 2017

Tamasha la Tigo Fiesta kufanyika Jumamosi Jijini Dar

 Mkurugenzi wa Huduma za Masoko Tigo, William Mpinga(katikati) akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa kutambulisha wasanii watakaopanda katika jukwaa la Tigo Fiesta siku ya jumamosi viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam leo mchana. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Tigo Fiesta, Sebastian Maganga na wengine ni wasanii.

Msanii Ben Pol akizungumza na waandishi wa Habari kwa niaba ya wasanii wa kiume

 Msanii Vanessa Mdee akizungumza na waandishi wa Habari kwa niaba ya wasanii wa kike

 Msanii Barnaba akiwa na wafanyakazi wa kampuni ya Tigo

Mdau akipata picha na msanii Vanessa

Wasanii Aslay na Rich Mavoko wakisalimiana jna wafanyakazi wa duka la Tigo Mlimani city walipotembelea duka hilo leo mchana

Msanii Barnaba akiwa na wafanyakazi wa kampuni ya Tigo

Mkurugenzi mkuu wa Tigo Tanzania Simon Karikari akisalimiana na msanii Vanessa Mdee

November 9, 2017

Mfumo wa kutengeneza na kusambaza filamu za Kitanzania (Bongohoodz) wazinduliwa

Kampuni za utengenezaji filamu za Mashauri Studios na Novitech kwa kushirikiana na Clouds Plus pamoja na Shirikisho la Filamu Tanzania imezindua rasmi mfumo wa kutengeneza, kutangaza, kuonyesha na kusambaza filamu za kitanzania ujulikanao kama Bongohoodz. 

  Akizungumza na waandishi wa habari, mwanzilishi mwenza wa Bongohoodz ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu na Mkurugenzi wa Mashauri Studios, Paul Mashauri, mfanyabiashara ambaye katika miaka ya hivi karibuni alimua kuwekeza katika filamu alisema Bongohoodz inakuja kuwasaidia waandaaji wa filamu nchini kutatua tatizo la wizi wa kazi za sanaa hasa DVDs kutokana na usambazaji wa sinema feki unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu. 

  “Baada ya kutoa sinema kazaa sokoni ikiwa ni pamoja na One Month Date mwaka 2014, Maisha ni Siasa na Bongo na Fleva mwaka 2015 tumegundua kuwa wizi wa kazi za sanaa ‘piracy’ ni mkubwa sana. Lakini kupitia Bongohoodz, watayarishaji wa sinema nchini hawatahitaji tena kusubiri mapato yao au uwekezaji wao urudi kwa kuuza DVDs, "Kimsingi hata katika nchi zilizopiga hatua katika sinema unazungumzia Hollywood (Marekani), Bollywood (India), China Film Industry (China) na Nollywood (Nigeria), mapato makubwa yanatokana na uonyeshaji wa sinema katika majumba ya sinema au ‘theaters’ wao wanaita ‘Box Office’. Kwa sababu wizi wa kazi za sanaa upo dunia nzima," alisema Mashauri na kuongeza. 

  "Lakini mapato ya kwanza wanayopata waandaaji wa sinema au ‘production houses’ yanatoka ‘Box office’ au katika nyumba za kuonyesha sinema. Ndio maana sisi tutasema, kwanini tusionyeshe sinema hizi nchi nzima katika matamasha makubwa ambapo watanzania watapata kuona sinema zinazoburudisha na kufundisha kwa bei nafuu kabisa huku wakifurahia vyakula mbalimbali, muziki, kisha filamu?”

Mashauri alisema kuwa wameanza jitihada za makusudi za kutangaza sinema hizi ikiwa ni pamoja na kuwatangaza wasanii na wazalishaji wa sinema,“Dunia nzima waigizaji wenye majina makubwa ndio wanaovutia walaji au wanunuzi wa filamu, hata kwetu imezoeleka hivyo. Lakini ili muigizaji awe mkubwa lazima kazi yake ionekana, "Kwa msingi huo na kwa ushirikiano wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na wadau wetu Clouds Plus, tumeanzisha ‘reality show’ ijulikanayo kama ‘The Producers’ inayoruka Clouds Plus kupitia king’amuzi cha Azam Tv kila siku jumatatu hadi ijumaa saa moja mpaka saa moja na nusu usiku na marudio siku ya jumapili kuanzia saa nne asubuhi ambapo watanzania wataweza kuona namna sinema zinavyotengenezwa na wasanii wanavyofanya kazi zao," alisema Mashauri. 

  Mashauri alisema kupitia kipiendi hicho watu mbalimbali ambao wanandoto za kuwa waigizaji watajua nini wa natakiwa kufanya kwani wataona fursa ziliziopo katika tasnia ya uigizaji na changamoto zinazowapata waandaji na waigizaji. "Tunategemea kufanya kazi na waandaaji kumi kwa mzunguko wa miezi sita sita na kila Producer atatakiwa kuzalisha sinema ndani ya miezi sita na mchakato wa sinema yake utaonyeshwa katika reality show, sinema yake itatangazwa na kupelekwa sokoni," alisema Mashauri. 

  Naye Meneja wa Clouds Plus, Ramadhani Bukini, alisema Clouds Plus imeungana na Bongohoodz katika kufanikisha ukuaji wa soko la filamu nchini kwa kutoa fursa kwa wazalishaji wa sinema kuonyesha kazi zao na kuzipeleka sokoni kupitia matamasha. “Tumeungana na Bongohoodz tukiamini kuwa lazima kuwe na mbinu mbadala za kuuza sinema. Dunia imebadilika sana na huwezi kutegemea chanzo kimoja cha mapato. Mfano, katika dunia ya leo, aina ya kompyuta zinazoongoza kwa kuuza duniani ni za Apple. Watumiaji wa ‘computer’ hizi hawahamasiki kutumia DVDs. 

Inamaana tunakoelekea hata wenye deki za kuangalia DVDs ni wachache, "Watu wako kwenye simu za mikononi, ndio maana Clouds Plus ikaamua kuungana na Bongohoodz kuja na vyanzo vipya vya mapato kwa tasnia ya filamu Tanzania ikiwa ni pamoja na matamasha makubwa ya kuonyesha filamu. Kama imewezekana katika muziki tunaamini kabisa inawezekana katika filamu," alisema Bukini. Naye mwanzilishi mwenza wa Bongohoodz ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Novitech ambayo inashirikiana na Mashauri Studios katika kutayarisha sinema, 

Mary Mgurusi alisema watanzania wasubirie kwa hamu kazi nzuri za filamu. “Tumeandaa sinema nzuri za kitanzania zenye maudhui tofauti tofauti ambazo tunaamini zinaburudisha na kufundisha. Tayari sinema ya Tatu Chafu imekamilika na tunatarajia kuizindua tarehe 16/12/2017 Mlimani City pamoja na Dar Live Mbagala. Baada ya uzinduzi huo, tunatarajia kuonyesha sinema hii nchi nzima katika mikoa mbalimbali. Zaidi ya Tatu Chafu zipo sinema nyingi katika maandalizi, mfano Tajiri kutoka India, What is Marriage, Rashid Snake Boy Matumla na School Bus," alisema Mgurusi.

November 8, 2017

JOKATE AKUNWA KUONA TOT BADO IMARA, YAREKODI NYIMBO MPYA ZA MKUTANO MKUU WA CCM NA JUMUIA ZAKE

Jokate na Khadija Kopa wakati wa mazoezi ya TOT
NA BASHIR NKOROMO

Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM (UVCCM) Jokate Mwengelo amesema amefurahi na kufarijika sana kuona kundi la Tanzania One Theatre (TOT) likiwa bado lipo imara na kuendelea kutoa nyimbo mpya zenye ubora wa hali ya juu kuanzia maudhui mpaka mpangilio wa mashairi na ala za muziki.


Amesema, uimara wa TOT unafanya kundi hilo kuendelea kutoa mchango mkubwa  kwa kutoa nyimbo

zenye hamasa kwa wananchi na hasa viongozi katika kuenzi amani, umoja, mashikamano wa kitaifa, uzalendo na uchapakazi na pia kuburudisha.


Jokate amesema hayo, alipotembelea mazoezi ya yimbo za Mkutano Mkuu wa CCM taifa, na za Mikutano Mikuu ya Taifa ya Uchaguzi wa Jumua zote za Chama, yaliyokuwa yakifanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.



"Kwa muda mrefu nyimbo zimekuwa ni sehemu muhimu ya kupeleka ujumbe kwa jamii. Nina furahi kuona kwaya ya TOT inaendelea kuenzi hili kwa kutoa nyimbo zenye ubora wa hali ya juu kuanzia maudhui mpaka mpangilio wa mashairi.



Hizi nyimbo walizotunga TOT kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na mikutano ya Uchaguzi Mkuu wa Jumuia za Chama ni nzuri, zinatoa hamasa hasa kwa viongozi wetu wakizisikia nina imani watapata morali ya kuwa bora zaidi katika kazi zao", amesema Jokate.



Nyimbo hizo ambazo ambazo ni kwaya kundi la TOT juzi lilianza kuzirekodi katika Studio maarufu na ya kisasa  ya Highland Studio iliyopo Kigogo jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini alisema TOT imezitunga nyimbo hizo kwa ustadi mkubwa ili kuzifanya kuwa za kiwango bora kulingana na hadhi ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuia zake na pia kuzingatia umuhimu wa mkutano huo mkuu wa CCM taifa na mikutano mikuu ya Uchaguzi Mkuu ya Jumuia hizo za chama.



Amesema wimbo wa CCM umebeba maudhui ya kuwakaribisha Dodoma wajumbe wa Mkutano Mkuu 

wa CCM, ukiwahimiza wajumbe hao kukamilisha kwa kushiriki kwa busara na umakini mkubwa kwenye mkutano huo ili kuhakikisha CCM inapata viongozi bora wenye uwezo wa kuendana na matakwa ya CCM Mpya na Tanzania Mpya na kasi ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.


Tumaini amesema nyimbo za Jumuia za Chama pia zina maudhui ya kuwakaribisha wajumbe Dodoma, lakini wao tofauti na CCM wajumbe wahawafanyi shughuli ya kukamilisha bali wanafanya uchaguzi, hivyo wimbo unawahimiza kuwa kidete kuhakikisha wanachagua viongozi bora ambao watakisaidia Chama kutimiza malengo na ilani yake kwa mafanikio makubwa.



"Kwa upande wa umoja wa Umoja wa Vijana wa CCM tumeenda mbali zaidi, mbali na kuwahimiza kufanya uchaguzi kwa busara zaidi, lakini wimbo umehimiza vijana kujitambua na kuelewa kuwa UVCCM ndiyo chachu ya viongozi bora wa baadae wa CCM na pia watambue kuwa Vijana wa UVCCM ndiyo walinzi wa mstari wa mbele wa CCM hivyo lazima wawe wa kwanza kila mara kueleza mazuri yanayofanywa na Serikali ya CCM lakini pia wawe wa kwa kwanza na kwa haraka kuwajibu wapinzani wanapojaribu kubeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya CCM", alisema Tumaini.



Alisema, katika nyimbo hizo ambazo Jokate ameshiriki kutoa mchango mkubwa kuziboresha kwa namna mbalimbali wakati wa utungwaji, wakati wa mkutano mkuu zitauzwa kwa wajumbe zikiwa kwenye CD na DVD hivyo wajumbe wajiandae kuzipata.

Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Jokate Mwengelo akiwa na Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM Abdul Aziz Salehe (kushoto) na Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini wakati wakishuhudia mazoezi ya nyimbo mpya za Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mikutano Mikuu ya Uchaguzi ya Jumuia za Chama, kwenye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, juzi
TOT WAKIREKODI STUDIO
 Mwimbaji wa TOT akiingiza sauti yake kwenye moja ya nyimbo nne zilizotungwa na TOT kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mikutano Mikuu ya Uchaguzi ya Jumuia za Chama, katika Studio ya Highland, Kigogo, Dar es Salaam, jana.
 Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini akisikiliza kwa makini wakati mwimbaji huyo akiingiza sauti yake kwenye wimbo
 Tumaini akiwa na fundi mitambo wa Studio ya Highland wakati wa kurekodi nyumba hizo
 Waimbaji Nusra Minja na margareth Mwiru wakiimba wakati wa kurekodi kwenye Studio hiyo
 Waimbaji Mroka Emmanuel na Issa Sabby wakiimba wakati wa kurekodi wakiimba wakati wa kurekodi kwenye studio hiyo
 Jerry na waimbaji wenzake wakiimba wakati wa kurekodi

Neca Twalib ambaye ni mrithi wa aliyekuwa mwimbaji nguli na Mkurugenzi TOT John Komba, akiimba wakati wa kurekodi Studio. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO