Tangazo

November 8, 2017

JOKATE AKUNWA KUONA TOT BADO IMARA, YAREKODI NYIMBO MPYA ZA MKUTANO MKUU WA CCM NA JUMUIA ZAKE

Jokate na Khadija Kopa wakati wa mazoezi ya TOT
NA BASHIR NKOROMO

Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM (UVCCM) Jokate Mwengelo amesema amefurahi na kufarijika sana kuona kundi la Tanzania One Theatre (TOT) likiwa bado lipo imara na kuendelea kutoa nyimbo mpya zenye ubora wa hali ya juu kuanzia maudhui mpaka mpangilio wa mashairi na ala za muziki.


Amesema, uimara wa TOT unafanya kundi hilo kuendelea kutoa mchango mkubwa  kwa kutoa nyimbo

zenye hamasa kwa wananchi na hasa viongozi katika kuenzi amani, umoja, mashikamano wa kitaifa, uzalendo na uchapakazi na pia kuburudisha.


Jokate amesema hayo, alipotembelea mazoezi ya yimbo za Mkutano Mkuu wa CCM taifa, na za Mikutano Mikuu ya Taifa ya Uchaguzi wa Jumua zote za Chama, yaliyokuwa yakifanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.



"Kwa muda mrefu nyimbo zimekuwa ni sehemu muhimu ya kupeleka ujumbe kwa jamii. Nina furahi kuona kwaya ya TOT inaendelea kuenzi hili kwa kutoa nyimbo zenye ubora wa hali ya juu kuanzia maudhui mpaka mpangilio wa mashairi.



Hizi nyimbo walizotunga TOT kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na mikutano ya Uchaguzi Mkuu wa Jumuia za Chama ni nzuri, zinatoa hamasa hasa kwa viongozi wetu wakizisikia nina imani watapata morali ya kuwa bora zaidi katika kazi zao", amesema Jokate.



Nyimbo hizo ambazo ambazo ni kwaya kundi la TOT juzi lilianza kuzirekodi katika Studio maarufu na ya kisasa  ya Highland Studio iliyopo Kigogo jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini alisema TOT imezitunga nyimbo hizo kwa ustadi mkubwa ili kuzifanya kuwa za kiwango bora kulingana na hadhi ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuia zake na pia kuzingatia umuhimu wa mkutano huo mkuu wa CCM taifa na mikutano mikuu ya Uchaguzi Mkuu ya Jumuia hizo za chama.



Amesema wimbo wa CCM umebeba maudhui ya kuwakaribisha Dodoma wajumbe wa Mkutano Mkuu 

wa CCM, ukiwahimiza wajumbe hao kukamilisha kwa kushiriki kwa busara na umakini mkubwa kwenye mkutano huo ili kuhakikisha CCM inapata viongozi bora wenye uwezo wa kuendana na matakwa ya CCM Mpya na Tanzania Mpya na kasi ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.


Tumaini amesema nyimbo za Jumuia za Chama pia zina maudhui ya kuwakaribisha wajumbe Dodoma, lakini wao tofauti na CCM wajumbe wahawafanyi shughuli ya kukamilisha bali wanafanya uchaguzi, hivyo wimbo unawahimiza kuwa kidete kuhakikisha wanachagua viongozi bora ambao watakisaidia Chama kutimiza malengo na ilani yake kwa mafanikio makubwa.



"Kwa upande wa umoja wa Umoja wa Vijana wa CCM tumeenda mbali zaidi, mbali na kuwahimiza kufanya uchaguzi kwa busara zaidi, lakini wimbo umehimiza vijana kujitambua na kuelewa kuwa UVCCM ndiyo chachu ya viongozi bora wa baadae wa CCM na pia watambue kuwa Vijana wa UVCCM ndiyo walinzi wa mstari wa mbele wa CCM hivyo lazima wawe wa kwanza kila mara kueleza mazuri yanayofanywa na Serikali ya CCM lakini pia wawe wa kwa kwanza na kwa haraka kuwajibu wapinzani wanapojaribu kubeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya CCM", alisema Tumaini.



Alisema, katika nyimbo hizo ambazo Jokate ameshiriki kutoa mchango mkubwa kuziboresha kwa namna mbalimbali wakati wa utungwaji, wakati wa mkutano mkuu zitauzwa kwa wajumbe zikiwa kwenye CD na DVD hivyo wajumbe wajiandae kuzipata.

Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Jokate Mwengelo akiwa na Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM Abdul Aziz Salehe (kushoto) na Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini wakati wakishuhudia mazoezi ya nyimbo mpya za Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mikutano Mikuu ya Uchaguzi ya Jumuia za Chama, kwenye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, juzi
TOT WAKIREKODI STUDIO
 Mwimbaji wa TOT akiingiza sauti yake kwenye moja ya nyimbo nne zilizotungwa na TOT kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mikutano Mikuu ya Uchaguzi ya Jumuia za Chama, katika Studio ya Highland, Kigogo, Dar es Salaam, jana.
 Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini akisikiliza kwa makini wakati mwimbaji huyo akiingiza sauti yake kwenye wimbo
 Tumaini akiwa na fundi mitambo wa Studio ya Highland wakati wa kurekodi nyumba hizo
 Waimbaji Nusra Minja na margareth Mwiru wakiimba wakati wa kurekodi kwenye Studio hiyo
 Waimbaji Mroka Emmanuel na Issa Sabby wakiimba wakati wa kurekodi wakiimba wakati wa kurekodi kwenye studio hiyo
 Jerry na waimbaji wenzake wakiimba wakati wa kurekodi

Neca Twalib ambaye ni mrithi wa aliyekuwa mwimbaji nguli na Mkurugenzi TOT John Komba, akiimba wakati wa kurekodi Studio. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments: