Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto |
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ilikutana Dar es Salaam wiki iliyopita na kujadili masuala mbalimbali.
(A) Kubughudhiwa Waandishi viwanjani
TASWA inalaani vitendo vya baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu ambao si wastaarabu kuwabughudhi waandishi wa habari za michezo kwa namna mbalimbali wakati wakitekeleza majukumu yao viwanjani na kuwasababishia kwa kiasi fulani washindwe kuyatekeleza kwa ufasaha majukumu hayo.
Matatizo makubwa yameibuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kamati inaona yanasababishwa na kutokuwepo eneo maalum la kukaa waandishi uwanjani, hivyo kujichanganya na mashabiki jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.
Kutokana na msingi huo kikao kiliiagiza Sekretarieti ya TASWA ifanye mazungumzo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusiana na eneo ambalo lilioneshwa miaka ya nyuma kabla uwanja haujaanza kutumika kwamba ni maalum kwa ajili ya kukaa waandishi wa habari za michezo, ili isaidie kupunguza matatizo hayo.
(B) Ushabiki kwa Waandishi wa Michezo
TASWA imesikitishwa na matukio yaliyojitokeza siku za karibuni kwa baadhi ya waandishi wa habari za michezo kuonesha ushabiki wa wazi wakati wakitekeleza majukumu ya kazi zao, hivyo kuwasababishia usumbufu usio wa lazima.
Tunawasihi waandishi wa habari za michezo wajiepushe sana na ushabiki, kwani kwa kuendekeza ushabiki wanakiuka maadili ya kazi zao na pia ni kujidhalilisha wao wenyewe.
TASWA inaamini suala la maadili ya mtu halihitaji kupigiwa kelele sana na chama bali linaanzia kwa mtu binafsi na chombo chake cha habari. Hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kujiangalia na kuwa katika mstari unaokubalika.
Tutaendelea kukumbushana kwa mambo mbalimbali ikiwemo semina kila inapodi kuhusiana na masuala ya maadili na mengine kadri tutakavyoona inafaa, lakini yapo mengine hayahitaji semina ni suala la mhusika binafsi kujitambua mwenyewe.
(C) Tamasha la Wanamichezo Miaka 50 ya Uhuru
TASWA imeunda Kamati ya Watu 16 kwa ajili ya kusimamia masuala ya tamasha la wanamichezo kwa ajili ya miaka 50 ya Uhuru.

Ambapo tamasha hilo litafanyika Novemba 5, jijini Dar es Salaam, hivyo kazi ya kamati ni kuandaa utaratibu wa kuwaenzi wanamichezo wetu waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka hiyo 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Kamati hiyo itaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Uhariri ya gazeti la Raia Mwema, Johnson Mbwambo, ambaye amepata kuwa Mhariri wa Habari za Michezo wa magazeti mbalimbali nchini na pia ni miongoni mwa waasisi wa TASWA.
Pia TASWA imemteua Mhariri Mkuu wa gazeti la SpotiStarehe, Masood Sanani kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Sanani ni Mhariri mzoefu, ambapo pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Tuzo za Wanamichezo Tanzania inayoandaliwa na TASWA, ambayo Mei mwaka huu ilifanya kazi kubwa kuandaa tuzo za aina yake.
Pia wapo Wajumbe wa Kamati hiyo ya Tamasha la Miaka 50 ya Uhuru, ambao ni wahariri wa siku nyingi na wana uzoefu mkubwa na masuala ya michezo na waandishi wa michezo, wajumbe hao ni Said Salim ambaye licha ya kuwa mhariri veteran pia ni mwalimu wa waandishi wa habari, ambapo anaishi Zanzibar, jambo litakalosaidia pia kuhusishwa wanamichezo wa zamani wa Zanzibar.
Mwingine ni Mhariri wa gazeti la ThisDay, Willy Chiwango, ambaye pia mkongwe katika masuala ya taaluma ya habari na mwenye uelewa mkubwa wa mambo ya michezo.
Wajumbe wengine ni:
1. Asha Muhaji-Mhariri Leap Media
2. Rashid Zahoro- Mhariri gazeti la Burudani
3. George John-Katibu Msaidizi TASWA
4. Mahmoud Zubeiry- Mhariri Dimba
5. Mohammed Mkangara-Mhazini Msaidizi TASWA
6. Juliana Yassoda-Naibu Mkurugenzi Idara ya Michezo
7. Majuto Omary-Mwenyekiti TASWA FC
8. Ephraim Kibonde- Mtangazaji Clouds FM
9. Deo Rweyunga-Mkurugenzi Radio One
10. Chacha Maginga-Mtangazaji TBC1
11. Amour Hassan-Mhariri Nipashe
12. Zena Chande-TASWA
Chama cha Gofu Wanawake Tanzania (TLGU).
Katibu wa Kamati atakuwa George John Katibu Msaidizi wa TASWA. Kamati itafanya kikao chake cha kwanza Jumapili Septemba 4, 2011.
(D) Semina ya Waandishi Morogoro
Maandalizi yanaendelea kuhusiana na semina kwa waandishi wa habari itakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao mkoani Morogoro na ile itakayofanyika Oktoba mkoani Arusha, ambazo tunaamini zitakuwa za manufaa kwa wadau wetu.
Ahsanteni.
Juma Pinto
Mwenyekiti TASWA
24/08/2011

No comments:
Post a Comment