Tangazo

September 5, 2011

Mashauriano yamevunjika Libya

Kanali Gadaffi
Wanajeshi wa baraza la utawala wa mpito nchini Libya, ambao wameuzingira mji wa Bani Walid ambao ni mji wa mwisho unaodhibitiwa na wanajeshi watiifu kwa kanali Muammar Gadaffi, wamesema mazungumzo kati yao yamesambaratika.
Kanali Gadaffi

Mmoja wa wapatanishi wakuu wa upinzani ameiambia BBC kuwa raia katika mji huo hawawezi kutembea kwa sababu wanahofia kupigwa risasi au kutekwa nyara na kutumiwa kama ngao.

Amesema wanajeshi watiifu kwa Gadaffi wamewataka wanajeshi hao wa upinzani kutoingia mjini humo huku wakiwa na silaha.

Amesema lililosalia sasa ni kwa makamanda wa jeshi la serikali hiyo ya mpito kuamua hatua watakayochukua.

Serikali ya mpito nchini Libya imesema ina uhakika kuwa mwanawe Kanali Gadaffi, Khamis Gadaffi ameuawa.
Wapiganaji wa waasi nchini Libya

Baraza hilo la kitaifa la mpito NTC limesema Khamis aliuawa kwenye mapigano makali karibu na mji mkuu wa Tripoli na kuzikwa karibu na mji wa Bani Walid.

Muhammad, ambaye ni mwanawe mkurugenzi mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi Abdullah Senussi, pia ameirpotiwa kuuawa.

Hakuna habari zozote zimetolewa kuhusu kifo chake. Kifo cha Khamis kimeripotiwa mara mbili lakini baadaye akajitokeza tangu ghasia za kisiasa kuanza nchini Libya.

Mji wa Bani Walid, ulioko 150km Kusini Mashariki mwa mji mkuu wa Tripoli, ni moja ya miji minne inayodhibitiwa na wanajeshi watiifu kwa kanali Gadaffi.

Miji mingine ni pamoja na miji ya Jufra, Sabha na Sirte

Mwenyekiti wa baraza hilo la NTC Mustafa Abdel Jalil amesema wanajeshi hao watiifu kwa kanali Ghadafi wanapewa msaada wa kibinadam kujisalimisha ili kuepusha umwagikaji zaidi wa damu nchini humo.Source: BBC Swahili

No comments: