Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron |
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema uchunguzi utaanza dhidi ya tuhuma kwamba majajusi wa Uingereza walihusika na mateso dhidi ya wafungwa katika jela wakati kanali Muammar Gadafi alipokuwa madarakani.
Bwana Cameron amesema ni muhimu kwa uchunguzi huo kuangazia madai kwamba kulikuwa na uhusiano wa karibu kati ya maafisa wa upelelezi wa Uingereza na Libya hasa baada ya shambulizi la septemba kumi na moja.
Kulingana la stakabadhi zilizofichuliwa mjini Tripoti hivi majuzi, inadaiwa kuwa huduma za ujasusi nchini Uingereza huenda zilitumiwa kuwahamisha washukiwa wawili wa ugaidi hadi nchini Libya mnamo mwaka 2004.
Akizungumza katika Bunge, Bwana Cameron alisema madai hayo sasa yatachunguzwa pamoja na madai mengine kuwa Serikali ya Uingereza iliyopita iliruhusu uhusiano wake na Libywa kuwa karibu kupita kiasi. Lakini hata hivyo Waziri Mkuu alitahadharisha kuwa watu hawapaswi kuharakisha kulaumu huduma za kijasusio za Uingereza.
Akizungumza dakika chache tu baadaye katika Bunge la Commons, Waziri wa Mashauri ya Kigeni katika Serikali iliyopita ya Labour, Jack Straw, alikariri madai ambayo yamerudiwa mara kadhaa sasa kuwa yeye na Mawaziri wengine walipinga mateso ya washukiwa walipokuwa mamlakani. Chanzo: BBC Swahili

No comments:
Post a Comment