Tangazo

October 13, 2011

PICHA YETU YA LEO - WORLD SIGHT DAY " SEEING IS BELIEVING"




Kamera ya Daily Mitikasi Blog leo ilifanikiwa kupata taswira nzuriii... za Dada yetu Anna Makanza ambaye ni Ofisa Uhusiano wa Benki ya Standard Chartered muda mfupi tu kabla ya kuanza  kwa matembezi ya “Kuona ni Kuamini” yaliyoanzia katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo International House Mtaa wa Garden jijini Dar es Salaam leo hadi Viwanja  vya Mwembe Yanga ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha 'Siku ya Kuona Duniani' ambapo kulikuwa na kambi ya macho kwa ajili ya kutoa huduma za macho bure. Benki ya Standard Chartered ilikuwa na matukio ya kuchangisha fedha kwenye masoko yake 70,  ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kukusanya Dola za Marekani  milioni 100, kwa ajili ya kampeni yake ya 'Kuona ni Kuamini' ikishirikiana pamoja na wabia wake ikiwemo Asasi zisizo za Serikali ili kusaidia kutokomeza tatizo la upofu.




No comments: