HALI ya Katibu mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Angetile Osiah imezidi kuimarika na huenda akaruhusiwa wakati wowote kuanzia sasa, imefahamika.
Osiah ambaye amelazwa katika wodi ya Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwishoni mwa wiki iliyopita akisubuliwa na uvimbe kichwani alisema kwa sasa hali yake inaridhisha.
Alisema kutokana na kuimarika kwa afya yake pindi atakapomaliza kutumia dozi maalum kwa ajili ya kusaidia kukausha maji kwenye uvimbe huo.
Kwa hisani ya mamapipiro blog.
Kwa hisani ya mamapipiro blog.
No comments:
Post a Comment