MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA WAADHIMISHA SIKU YA WADAU KWA KUTOA MSAADA WA MASHUKA 700 KWA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA MKOANI MBEYA.
MJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA NHIF BI MARIAM WILMORE (WA PILI KUSHOTO) AKIKABIDHI MASHUKA KWA AJILI YA WODI ZILIZOPO KWENYE HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA JUMLA YA MASHUKA 100 YALIGAWIWA ,ANAYEPOKEA KATIBU WA AFYA WA HOSPITALI HIYO BI DORICE NZIGIRWA.
NAIBU MKURUGENZI MKUU WA NHIF BWN HAMIS I. Z. MDEE (MWENYE SUTI NYEUSI), AKITOA MSAADA WA MASHUKA KWENYE KITUO CHA AFYA CHA RUANDA AMBACHO KINAWAHUDUMIA ZAIDI AKINA MAMA WAJAWAZITO,ANAYEPOKEA NI MGANGA MFAWIDHI WA KITUO HICHO, ELIOT SANGA.
MAJUKUMU YA ULEZI KWA KARNE HII NI YA WOTE HAIJALISHI JINSIA ,PICHANI BWN. GIBSON MWALIBWA AKIWA AMEMBEBA MTOTO WAKE WA MWAKA MMOJA NA MIEZI 8,WAKATI MAMA MZAZI AKIPATA HUDUMA ZA MATIBABU KWENYE HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA.
SUALA LA MAHALI SAFI NA SALAMA KWA MAMA ANAYEJIFUNGUA NI VYEMA LIKATAZAMWA KWA JICHO LA KIPEKEE,PICHANI MJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI WA NHIF BI MARIAM WILMORE AKITANDIKA SHUKA KWENYE KITANDA KATIKA WODI YA WAZAZI WA HOSPITALI YA IGAWILO WAKATI AKITOA MSAADA WA MASHUKA KWENYE WODI HIYO, ANAYEMSAIDIA NI NESI MWANDAMIZI BI DORICE MWAKABENGA.
No comments:
Post a Comment