Tangazo

March 13, 2012

Serengeti Breweries Limited (SBL) yachangia Milioni 300 - WIKI YA MAJI 2012.

 Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda akifafanua jambo wakati wa kutangaza udhamini huo wa wiki ya maji jijini Dar es Salaam leo Machi 13.12.
********************
  “Water of Life” (WOL),  ni mpango maalum unaodhamiria kuwezesha upatikanaji wa maji safi ya kunywa na udhibiti wa usafi kwa watu wapatao milioni moja barani Afrika.

Maji yamepewa kipaumbele katika biashara yetu kimataifa.  Kampuni ya Bia ya Serengeti imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa maji safi na salama pamoja na usafi wa mazingira ni jambo linalotiliwa mkazo.
 
Wiki ya maji ambayo itaanza tarehe 16 Machi itaadhimishwa siku ya Machi 22 mwaka huu, ni jukwaa muhimu sana kutangaza na kuweka msisitizo wa umuhimu wa utunzaj wa maji na vyanzo vyake.

Kwa kuiheshimu kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni “Maji kwa usalama wa Chakula”,ni dhahiri kuwa maji yanachukua nafasi kubwa sana na hasa katika ulizalishaji wa chakula na kilimo kwa ujumla.

Tatizo la maji limekuwa likiathiri kila bara duniani na zaidi ya asilimia 40 ya watu hadi kufikia mwaka 2025, watu bilioni 1.8 watakuwa wanaishi katika nchi ama mikoa ambayo haina maji safi kabisa, na theluthi mbili ya idadi ya watu duniani inawezekana wanaishi katika hali ngumu ya upatikanaji wa maji. Kukosekana kwa maji kunawakosesha wakulima kuzalisha mazao ya kutosha kwa chakula na hata kujikimu kimaisha.

Kampuni ya bia ya Serengeti mwaka huu imetenga zaidi ya shilingi milioni mia tatu za kitanzania. Milioni mia moja za kitanzania zikilenga sherehe za maadhimisho mkoani Iringa kwa kudhamini vipeperushi, vijarida na zaidi ya shilingi milioni mia mbili zikilenga kwenye miradi salama ya maji na usafi katika mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Dar Es Salaam na Iringa.

Tunasisitiza kuhusu swala la kuongezeka kwa changamoto za tatizo la maji ulimwenguni, katika utendaji kazi wetu ndani ya kampuni na hata kwenye jamii inayotuzunguka.

Kama kampuni, Serengeti (SBL), inafanya kazi kupunguza matumizi ya maji katika vifaa vya uzalishaji na mfululizo wa utoaji wa bidhaa zetu. Hii inahusisha uboreshaji madhubuti wa maji katika mitambo yetu, kuhakikisha kuwa matumizi ya maji katika maeneo yetu yanazingatiwa, na kupunguza majitaka (na nguvu ya maji hayo katika  uchafuzi wa mazingira) kutoka kwenye mitambo yetu.

Pia tumekusudia kuongeza njia za upatikanaji wa maji kwenye jamii zinazotuzunguka na usimamizi wa vyanzo vya maji.
 
Kama kampuni inayowajibika, kufanya kazi na wengine kuendeleza lengo la Umoja wa Mataifa(UN) la Malengo ya Milenia ya Maendeleo kwa ajili ya maji na usafi wa mazingira na kupitia juhudi za pamoja na wafanyakazi wetu, watumiaji, wateja, wagawaji, mashirika yasio ya kiserikali, serikali, na biashara nyingine tunafanya kazi kwa pamoja ili kuhamasisha na kutoa malengo yatakaotoa suluhisho la muda mrefu la kutatua shida ya maji katika masoko yetu.

Programu hii ya Water of Life(WOL), imekusudia kutoa upatikanaji wa huduma ya maji safi, inaimarisha kazi tunazofanya katika utendaji wetu wa kazi. Tunatumia ujuzi, watu wanaotuzunguka washirika na wadau wetu kuhakikisha kuwa maji safi yanapatikana hasa pale yahahitajika. Kwa Jamii, majumbani na kwa watu binafsi.
 
Biashara yetu imekuwa ikijihusisha na miradi mbali mbali ya maji safi na mazingira  kama ‘Mkuranga water project’ na moja nyingine ambayo ilikuwa ni mradi ambao ulishirikisha makampuni na mashirika yasio ya kiserikali ni mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji katika hospitali ya Amana.

Kampuni ya Bia ya Serengeti na EABL foundation iliwekeza kiashi shilingi milioni 384.6 za kitanzania katika mradi wa Mkuranga na zaidi ya watu 250,000 wamefaidika.

Tunatambua kwamba maji safi ni muhimu kwa maendeleo na kwa kuchangia kuboresha afya ya jamii na kiwango cha elimu na pia kupunguza umaskini. Mradi wa ‘Water Of Life (WOL) ulizinduliwa na Diageo mwezi Juni mwaka 2006 kwa lengo la kutoa maji safi ya kunywa kwa walengwa. Diageo  ilizindua mradi huu katika nchi 14 nyingi zikiwa ni nchi za Afrika, kwa kusadia miradi mbali mbali ikiwemo ya uchimbaji wa visima, visima vya mkono, uvunaji wa mvua, na mbinu za kuchuja maji.

Uwekezaji wetu katika jamii utaendelea kwa kusaidia na kukamilisha kazi yetu katika utendaji wetu, ili kupunguza athari za usambazaji wa maji taka na kuboresha upatikanaji wa maji safi ya kunywa katika mikoa tunayofanya shughuli zetu.
Picha na habari kwa Hisani ya Father Kidevu Blog

No comments: