*********************
Na Ali Meja-Pemba
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano amewataka wananchi kutoita majina ya wafadhili miradi ya maendeleo ili kuonyesha uzalendo na kuwa na uchungu nayo .
Ameyasema hayo wakati akikagua jengo la wizara ya mifugo na uvuvi pemba ambalo limejengwa kwa ufadhili wa macep ,ili kutoa huduma kwa umakini za wazara hiyo .
Akizungumza kwa ufasaha amesema kuwa kazi ya wafadhili ni kutoa fedha tu lakini suala la utunzaji wa maradi ni jukumu letu sisi ambao ndio walengwa wakuu wa miradi hiyo ya maendeleo.
Akisisitiza juu ya suala hilo mbalo limekuwa ni moja ya mambo makubwa yanayotukabili katika miradi mbali mbali kwa sasa ,Hivyo sasa ni wakati wananchi wahusika kuipa majina yao wenyewe ili miradi hiyo iwe na tija kubwa kwa jamii husika.
“Utasikia mtu anasema mradi wa macep mara, assp ,who, au unicef ,lakini kama hili jengo lenu linatwa jadari house kwa maana yake hasa ili kutoa chachu ya kuwa na imani na miradi mbayo walengwa wake wakuu ni wananchi husika.
Alisema waziri Samia kwa msisitizo “sasa kazi iwe kwanu namna ya kulitunza na kulindesha kwa utaratibu mzuri na salama “ alisema waziri samia.
Leo waziri samia akiwa ni siku yake ya pili katika ziara hapa kisiwani pemba amefanya ziara ya kuikagua Ikulu ya wete ambayo ndio lkulu ya makamu wa rais pemba.
Pia samia na ujumbe wake walipitia katika chinjio la ngo,mbe la wete ambalo limefadhiliwa na mfuko wa maendeleo ya jimbo unaotokana na bunge la jumuhuri uya mungano (CDCF) ambao ni mfuko wa mandeleo jimbo na kujionea hali ilivyo katika eneo hilo ,wakati mchana alitembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa barara zaidi ya kilomita 35 katika kisiwa cha pemba unajegwa kwa ufadhili wa mradi mcc kutoka mbamabarau takau hadi finya .
Wakati akiwa katika zira hiyo alipata furusa ya kutembelea ofisi za wa wabunge katika majimbo ya micheweni na mchangamdogo ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa bunge la jumuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia mfuko wa maendeleo .
No comments:
Post a Comment