Tangazo

April 13, 2012

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA IKULU LEO

Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Jaji Joseph Sinde Warioba, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Walioapishwa ni Mwenyekiti wa Tume, Makamu wake na Wajumbe 30 wa Tume hiyo. Picha na Muhidin Sufiani. OMR

Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Jaji Agustino Ramadhan, kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Muhidin Sufiani. OMR

Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mbunge wa Viti Maalum, Al-shymaa Kwegiyr,  kuwa Mjumbe wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Muhidin Sufiani. OMR

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, na Makamu wake wawili, Maalim Seif na Balozi Seif Idd, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Viongozi wateule na wajumbe wa Tume hiyo baada ya kuapishwa rasmi. Tume hiyo inatarajia kuanza kazi rasmi Mei 01, mwaka huu. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: