Tangazo

April 25, 2012

SIKU YA MALARIA DUNIANI: MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AZINDUA RIPOTI YA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MIKAKATI YA MALARIA TANZANIA BARA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani, zilizofanyika leo Aprili 25, 2012 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Katika sherehe hizo pia Makamu wa Rais alizindua Ripoti ya Utekelezaji wa Mikakati ya Malaria Tanzania Bara. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe, kuzindua Ripoti ya Mafanikio ya Utekelezaji wa Mikakati ya Malaria kwa upande wa Tanzania Bara, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Malaria Duniani zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo Aprili 25, 2012. Katikati ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda (wapili kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala, Jordan Lugwimbana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: