Tangazo

April 23, 2012

Vodacom yakabidhi kitita cha Milioni 10/- kwa Mshindi wa Pili wa Promosheni ya M-Pesa

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania  Bw. Rene Meza (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari  katika hafla fupi ya kukabidhi fedha kwa mshindi wa pili wa droo kubwa ya mwezi ya promosheni ya  M-pesa  Bw. Revocatus Mkama (kulia) anaejishughulisha na ufundi wa magari jijini Mwanza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza (kushoto) akimkabidhi mshindi wa pili wa droo kubwa ya mwezi ya promosheni ya M-pesa Bw. Revocatus Mkama (kulia) fedha taslimu shilingi milioni kumi  katika hafla fupi iliyofanyika katika Makao makuu ya Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar es salaam.

Mshindi wa pili wa droo kubwa ya mwezi ya promosheni ya M-pesa Bw. Revocatus Mkama ambaye pia ni mkazi wa Mwanza anayejishughulisha na ufundi wa magari akifurahia kitita cha shilingi milioni kumi alizoshinda kupitia promosheni ya M-pesa mara baada ya kukabidhiwa fedha hizo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza.

No comments: