Tangazo

May 31, 2012

NMB YAZINDUA PROMOSHENI YA JENGA MAISHA YAKO NA NMB

Mkurugenzi Wa Masoko wa Benki ya NMB, Imani Kajura akifafanua jambo juu ya Promosheni mpya ya Jenga Maisha yako na NMB wakati wa uzinduzi wake Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Masoko wa NMB, Shilla Hatibu Senkoro.

Imani Kajura akionesha moja ya vipeperushi vya Promotion hiyo mpya ya NMB kwa wateja wake.
********
NMB ikiwa ni benki yenye kujali malengo ya wateja wake, inaanzisha promosheni inayowezesha wateja wote wa NMB Bonus Account na NMB Junior Account kuingia kwenye droo ya kushinda; tani ya saruji, mabati ya kuwezekea, amana maradufu, ada za shule, fulana za NMB au mabegi ya shule kupitia promosheni ya JENGA MAISHA YAKO NA NMB. Promosheni ya JENGA MAISHA YAKO NA NMB itachezeshwa kila mwisho wa mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu.

NMB inaamini promosheni hii sio tu kwamba itaongeza tabia ya kujiwekea akiba lakini pia itasaidia wateja watakaoshinda kufikia malengo waliyojiwekea na pia kuboresha maisha yao.

Wateja wote watakaofungua akaunti au kuongeza amana kwenye za NMB Bonus Account au NMB Junior Account watapata riba ya kuvutia ambayo inaweza kuwa hadi asilimia 10 kutegemeana na kiwango cha amana zilizowekwa.

Baada ya ubinafsishaji wa benki ya NMB mwaka 2005, NMB iliendelea kukuza mtandao wake wa matawi, ndani ya miaka mitano matawi yameongezeka kutoka 100 hadi matawi zaidi ya 140. Idadi ya wateja wa NMB imekua kutoka wateja 600,000 mpaka wateja 1,600,000 hiyo ni asilimia 30 au 40 ya watanzania wote ambao wana akaunti katika benki zote za Tanzania ili kurahisisha na kuboresha utoaji huduma.

NMB ilianza kutoa huduma ya ATM kutoka wateja 0 mpaka wateja milioni moja na laki sita na pia namba za mashine za kutolea fedha (ATM) zimekuwa kutoka 0 mpaka 450 na pia NMB ndio benki ya kwanza Tanzania kuanzisha huduma za kibenki kwa kutumia simu ya mkononi, NMB Mobile. Hadi sasa kuna wateja 600,000 wanaotumia huduma ya NMB Mobile

NMB imeendelea kubuni na kuanzisha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya wateja wake. NMB ndio benki pekee Tanzania yenye akaunti kuanzia za watoto wadogo, wanafunzi, wafanyakazi, wakulima na wastaafu. Pia NMB imeendelea kuboresha faida wateja wanazozipata kutokana na kuwa na akaunti NMB.

Hivisasa mteja wa NMB ana chaguo pana la njia za kupata huduma; anaweza kupata huduma ndani ya benki, kutumia ATM, kutumia NMB mobile au huduma ya Intaneti.

NMB ni benki inayowajali sana wateja wake hata wakati wa shida, mwaka jana, 2011 NMB ilizindua huduma ya NMB Faraja inayomwezesha mteja wa NMB Personal Account kupata mkono wa pole kati ya shilingi 600,000 hadi 1,200,000. Hadi sasa, huduma ya NMB Faraja imewanufaisha wateja wengi wa NMB, nchi nzima.

Utafiti uliofanywa na NMB uligundua kuwa wateja wengi wanaweka akiba ili kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea. Miongoni mwa malengo hayo ni kujenga nyumba, kusomesha watoto na kufikia malengo mengine muhimu maishani mwao.

No comments: