Tangazo

July 5, 2012

DC Mvomero atembelea Maonyesho ya Kilimo cha Mseto na Shamba Darasa

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Anthony  Mtaka (kulia) akimsikiliza mkulima wa kijiji cha Vitonga Gaitan Kulinyangwa (kushoto) wakati akieleza juu ya kilimo cha mseto na shamba darasa  katika kijiji cha Vitonga Kata ya Mlali wilayani humo Julai 04.12. Mradi huo unafadhiliwa na nchi ya Australia zikihusishwa na nchi nyingine tano za Afrika za Kenya, Ethiopia, Tanzania, Malawi na Msumbiji ambapo utafiti huo imelenga katika kulima mazao mchanganyiko ya mahindi na Mikunde kwa ajili ya kuongeza uzalishaji ngazi ya kaya mkoani humo.

Mkuu wa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Anthony  Mtaka kushoto akimsikiliza mtafiti kiongozi wa taasisi ya serikali katika mradi wa mifumo ya kilimo endelevu ya mahindi na mikunde mashariki na kusini na kusini mwa afrika  (SIMLESA), George Iranga (katikati) akieleza jambo wakati wa maonyesho ya kilimo cha mseto na shamba darasa. Kulia ni mmoja wa wakulima wa kilimo hicho kijijini hapo,  Gaitan Kulinyangwa.

Mkuu wa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Anthony Mtaka (kushoto) akimsikiliza mratibu msaidi wa taasisi ya serikali katika mradi wa mifumo ya kilimo endelevu ya mahindi na mikunde mashariki na kusini na kusini mwa afrika  (SIMLESA), Bashiri Mkoko (katikati) akieleza jambo wakati wa maonyesho ya kilimo cha mseto na shamba darasa yaliyofanyika  katika kijiji cha Vitonga Kata ya Mlali wilayani humo Julai 04.12.  Kulia George Iranga wa taasisi hiyo. Picha kwa hisani ya Juma Mtanda Blog

No comments: