Na Mwandishi Wetu
MWANACHAMA Maarufu wa klabu ya Simba, Zakaria Hanspope amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kundi la marafiki wa Simba ‘Firend of Simba’ kufuatia kikao kilichoo juzi, katika hoteli ya JB Delmonte.
Hanspope anachukua nafasi ya Salum Abdallah aliyeongoza kundi hilo kwa zaidi ya miaka mitano na kuleta mafanikio makubwa ndani ya klabu ya Simba, kwa uhamasishaji wa kundi hilo lilijizolea umaarufu mkubwa ndani ya klabu hiyo.
Mbali na Hanspope, wengine waliochaguliwa ni Adam Mgoy anayekuwa Makamu Mwenyekiti, nafasi ya Katibu Mkuu imekwenda kwa Mulamu Nghambi, wakati nafasi ya Katibu msaidizi amechaguliwa Niki Magariza na Juma Pinto atakuwa msemaji wa kundi hilo.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa, Hanspope alisema atajitahidi kufanya kila aliwezalo kuhakikisha kundi hilo linafanya kazi kazi kwa kushirikiana na uongozi kwa lengo la kuleta maelewano yatakayoijenga Simba imara na kuleta burudani kwa wapenzi na mashabiki.
“Sisi ni marafiki wa Simba, tunachokifanya lazima kiendane na tasfsiri ya neno lenyewe na isije ikawa tofauti kuwa ni maadui wa Simba, naomba ushirikiano wa pamoja kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu,” alisema Hanspope katika shukrani zake.
Awali mmoja wa waasisi wa kundi hilo, Jaji mstaafu Thomas Mihayo alisema mwelekeo na dira ya kundi hilo lilipotea, hivyo kuwa na imani kwa viongozi wapya kufanya kazi ambayo itakuwa na faida kwa maendeleo ya Simba.
Jaji Mihayo alisema kundi hili limekuwa na malengo mazuri lakini kinachokwamisha sasa hivi ni wanachama wake kutokuwa wamoja na kuwataka kurudisha umoja na kufuatialia kwa mambo ambayo yanapangwa kwa ajili ya utekelezaji.
Viongozi wa zamani waliomaliza muda wake ni Salum Abdallah (Mwenyekiti),Johnson Masabala (Makamu Mwenyekiti) na Issa Batenga aliyekuwa katibu wa kundi hilo.
No comments:
Post a Comment