|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Radegunda Maro, wakati ofisa huyo alipofika nyumbani kwa Makamu akiwa na Karani wa Sensa na msimamizi wake kutoka Kituo cha Oysterbay, kwa ajili ya kukamilisha zoezi la Sensa, Agosti, 26, 2012. Picha na OMR |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijiandaa kujibu maswali kutoka kwa Karani wa Sensa, Happyness Masaka (kulia) ikiwa ni sehemu ya kukamilisha zoezi hilo la Senza ya watu na Makazi, lililoanza nchini kote, ambalo litadumu kwa siku saba. Picha na OMR |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Karani wa Senza, Happyness Masaka, baada ya kukamilisha zoezi la kujibu maswali husika katika zoezi hilo, nyumbani kwake Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msimamizi wa Sensa wa Kituo cha Oysterbay, Daria Kailembo (kushoto) ni Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Ttifa, Stanley Mahembe. Picha na OMR | | |
*******************************
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Agosti 26, saa tatu asubuhi, ameshiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya watu na Makazi akiwa kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Dkt. Bilal, ameshiriki katika zoezi hilo kwa kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Karani wa Kituo cha Oysterbay, Happyness Masaka, mbaye alifika nyumbani kwa makamu akiwa ameongozana na msimamizi wake, Daria Kailembo, pamoja na Maofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Stanley Mahembe na Radegunda Maro.
Aidha, Dkt. Bilal, ametumia dakika 25 kwa kujibu jumla ya maswali 37, yaliyoandaliwa ili kukamilisha zoezi hilo.
Akizungumza baada ya kukamilisha zoezi hilo, Dkt. Bilal, amewahasa Watanzania wote kwa ujumla kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa Makarani ili kufanikisha zoezi hilo, ambalo litadumu kwa siku saba. Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais Box 5380 Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment