Kundi la SKYLIGHT Band likishambulia Jukwaa kabla ya uzinduzi wa Kinywaji Kipya kinachozalishwa na kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) cha MALTIZA kinachotengenezwa na Kimea halisi kisicho na kilevi uliofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar leo.
Malkia wa SKYLIGHT Band inayokuja kwa kasi jijini Aneth Kushaba (mbele kulia) sambamba na Mariam Lucas wakikonga nyoyo za Wakazi wa Dar waliohudhuria uzinduzi huo.
Meneja wa Kinywaji Kipya cha MALTIZA kinachozalishwa na TBL Bi. Consolata Adam (katikati) akikaribisha wageni kuhudhuria uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika leo jijini Dar.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiorodhesha majina yao kwa warembo maalum waliondaliwa kupokea wageni na kushiriki bahati nasibu ya papo kwa hapo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji cha MALTIZA.
Meneja wa Kinywaji Kipya cha MALTIZA kinachozalishwa na TBL Bi. Consolata Adam akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na kuzinduliwa kwa kinywaji hicho kipya kinachopatikana katika ladha mbili za APPLE na PINE (Pineapple) ambacho amefafanua kwamba Tanzania imekuwa ya kwanza kwa Afrika kuzindua kinywaji cha aina hiyo kisicho na kilevi chenye ubora na kinachotengenezwa na kimea halisi kinachozalishwa hapa nchini.
Bi. Consolata Adam amesema kinywaji hicho kinapatikana katika ujazo wa 330Mls na kimeshasambazwa nchini kote na bei yake ni shilingi 1500, aliongeza kuwa kinywaji hicho ni halisi kisichotiwa rangi na kuwataka Watanzania kujiburudisha na MALTIZA.
Bi. Consolata Adam akionyesha kopo za Ujazo wa 330Mls za kinywaji cha MALTIZA aina ya APPLE na PINE.
Kikundi cha Ngoma kikipamba uzinduzi wa kinywa cha MALTIZA (Deliciously Refreshing),
Sasa kimezinduliwa rasmi.
SKYLIGHT Band na Kikundi cha Sarakasi wakisindikiza uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Masoko iliyoandaa uzinduzi huo wakiburudika na Sebene lililoporomoshwa na SKYLIGHT Band katika shamrashamra hizo.
Pichani Juu na Chini ni Umati wa Wakazi wa jijini Dar uliohudhuria uzinduzi wa Kinywaji Kipya cha MALTIZA ambacho hakina kilevi kinachopatikana katika ladha mbili tofauti APPLE na PINE kinachotengenezwa na kampuni ya TBL uliofanyika Mlimani City leo.
Msanii wa Bongo Flava nchini Mwasiti akitoa burudani huku akisindikizwa na mshehereshaji wakati wa uzinduzi wa kinywaji cha MALTIZA.
Meneja wa Kinywaji Kipya cha MALTIZA kinachozalishwa na TBL Bi. Consolata Adam akiwapa habari njema Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo kuwa kinywaji hicho kinafaa kunywewa na Wakubwa kwa wadogo kwa kuwa hakina kilevi, kinaburudisha na kinarejesha nguvu mwilini. Kulia ni Meneja Mauzo wa MALTIZA Bw. Flavian.
Aliyewahi kutwaa taji la Mr. Tanzania Mario Mpingirwa (kulia) akiwa na Wadau wakishuhudia burudani zilizokuwa zikiendelea wakati wa uzinduzi wa MALTIZA.
No comments:
Post a Comment