Na Zawadi Msalla - MAELEZO
Arusha.
Rais
Jakaya Kikwete ameiasa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi Kusini mwa Afrika
(SADC) kuimarisha ushirikiano kati yake na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo
ili kufanikisha utekelezaji wa Mkakati wa pili wa kushughulikia
masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya hiyo.
Rais
Kikwete ameeleza hayo wakati akizindua Mkakati wa kushughulikia masuala
ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya hiyo (SIPO II) jijini Arusha wakati wa
mkutano uliowahusisha wawakilishi mbalimbali kutoka katika Jumuiya wanachama wa
SADC.
Amesema
ili malengo ya Mkakati huo yaweze kufanikiwa ni lazima ushirikiano wa
ndani na nje wa nchi hizo wanachama uimarishwe na kuongeza kuwa SADC haiwezi
Kutegemea mikakati ya ndani ya ulinzi na Usalama ya nchi fulani kutaka kutekeleza
mkakati wake.
"SADC
haitakiwi kuiingilia kwa kutaka kuibadili mikakati ya ndani ya Nchi
wanachama ya ulinzi na usalama badala yake washirikiane kwa karibu kuangalia
nini cha kufanya" Amesema Rais.
Kuhusu
umuhimu wa mkakati huo Rais Kikwete amesema utakuwa muongozo wa
SADC katika masuala yote ya ulinzi, usalama na siasa, na umejikita katika
kutatua vikwazo mbalimbali vya kiulinzi vilivyopo.
Amefafanua
kuwa Utekelezaji wa SIPO na maazimio yake utapelekea hali ya amani na utawala
bora kwa Nchi nyingi za Afrika na kuongeza kuwa katika awamu ya pili ya SIPO
mabadiliko mengi yamefanyika yakiwemo uongezaji wa vipaumbele katika mfumo wa
utekelezaji na ufuatiliaji wa masuala ya ulinzi na usalama.
Uzinduzi
wa SIPO II utaangalia ushirikiano kati ya Nchi wanachama, ushirikiano
katika masuala ya kibiashara, uhakika wa kushughulikia masuala ya
upatikanaji wa Amani na ushirikiano katika nyanja ya habari.
Akieleza
historia ya chombo cha Usalama cha SADC alisema kabla ya kuanzishwa kwa chombo
hicho kulikuwa na ushirikiano wa nchi katika masuala ya ulinzi na usalama na
kubainisha kuwa kuanzishwa kwa SIPO kunatokana na nchi wanachama kuona
umuhimu wa kuwa na chombo kinacho waongoza katika masuala hayo yote.
Awali akizungumza
na wajumbe wa mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Benard Membe amesema kuwa SIPO imekuwa ni nyenzo muhimu nay a kutegemewa na
nchi za SADC katika masuala yote ya usalama.
Amesema SIPO
ilizinduliwa rasmi mwaka 2004 na baadae kufanyiwa marekebisho ya kimsingi mwaka
2007 na kueleza kuwa kutokana na marekebisho hayo ya Mwaka 2007 ilikubaliwa
kuwa mikakati na vapaumbele vya SIPO iwe inapitiwa kila baada ya miaka
mitano.
Aidha
uzinduzi huo utafuatiwa na mafunzo mbalimbali yatakayoendeshwa na wataalamu kwa
muda wa siku nne.
No comments:
Post a Comment