Tangazo

January 6, 2013

LUKAZA BLOG EXCLUSSIVE: LUKAZA BLOG SASA KUKULETEA SOMO JUU YA MFUMO MZIMA WA DIGITALI NA MAWASILIANO YA SATELITE KILA JUMATATU

Kutokana Nchini Nyingi za Afrika Ikiwemo Tanzania Kulazimika Kuingia Kwenye Mfumo Mpya Wa Kurushia Matangazo ya televisheni wa digitali na kutoka Kwenye mfumo wa Zamani wa Analogia na Kupelekea Kuleta sintofahamu kwa wakazi wengi wa Tanzania kutokana na kutokuwa na Ufahamu japo kidogo juu ya Mfumo huu na Vifaa vinavyotumika katika Mfumo huu wa Digitali katika kupokea mawimbi hayo ndipo Lukaza Blog Imeamua kila Jumatatu itakuwa inaleta Somo Juu ya Mfumo Mzima Wa Digitali ambapo katika Mfumo huu Tutaangalia Juu ya Ving'amuzi na Satelite na tutaangalia Juu Ya Mfumo Mzima Wa Satelite na Upokeaji wa Mawimbi ya Satelite.
Kutokana Na Watanzania Wengi kutokuwa na Uelewa Juu ya Vitu hivi Ndipo Lukaza Blog Imeamua Kuleta Somo hili la Digitali na Somo Hili litakuwa linatolewa Kila Jumatatu Kupitia wataalamu wetu wa Mambo ya Digitali na Mifumo Ya satelite na Juu ya Aina Gani ya Ving'amuzi inafaa katika Ukanda wetu huu Wa Tanzania.
Kaeni Mkao wa Kula Kuanzia Jumatatu ya Kesho somo letu litakuwa Juu ya Mawasiliano ya Satelite, Satelite ni nini?,Aina Za Satelite? ,Na Satelite za Mawasiliano.
Karibu Katika Somo hili la Mawasiliano ya Satelite Na matarajio yetu Kuwa Wasomaji wetu Mtapata Uelewa juu ya Mfumo Huu na kupelekea Kujua Ni Nini na Nini Kinahitajika Katika Ulimwengu huu wa Digitali 
Lukaza Blog Kwa Kuona Umuhimu wa Kupata elimu hii ya Mawasiliano ya Satelite ambao ndio Mfumo wa Digitali wenyewe Basi tumeamua Kuwaletea Wasomaji wetu Somo hili Kwa Kushirikiana na Wataalamu wetu Wa Maswala ya Mawasiliano ya Satelite ambayo ndio Mfumo Mzima Wa Digitali ili kusudi Watanzania wote tupate elimu ya kutosha katika swala zima la Mfumo wa Digitali. Somo hilo litakuwa linapatikana kupitia anuani hii chini 
 http://josephatlukaza.blogspot.com 
Imetolewa na 
- Josephat Lukaza -
- Lukaza Blog Admin - - http://josephatlukaza.blogspot.com -

No comments: