Tangazo

January 21, 2013

Mangula aunguruma Mwanza

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula akiwasalimia mabalozi wa nyumba kumi wa kata 21 za Ilemela na Nyamagana baada ya kuzungumza nao, kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, Januari 20, 2013. Kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula akimtazama mtoto Rehema Basima (2), alipokuwa akiwasalimia  mabalozi wa nyumba kumi wa kata 21 za Ilemela na Nyamagana baada ya kuzungumza nao, kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza Januari 20, 2013.

Mabalozi wa nyumba kumi wakiwa wamepanga foleni ili kupata fursa ya kumuuliza maswali, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula alipozungumza nao kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijibu baadhi ya maswali ya wajumbe wa nyumba kumi, wakati wa mkutano wa wajumbe hao na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akijibu maswali ya wajumbe wa nyumba kumi, alipozungumza nao kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Mangula akizungumza na wajumbe wa nyumba kumi jijini Mwanza.

No comments: