Tangazo

February 7, 2013

Kutoka Bungeni Leo

Naibu Waziri, Ofisi ya  Waziri Mkuu (TAMISEMI), Aggrey Mwanri akiwakilisha hati mezani kuhusu Taarifa ya  Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha,2010/2011. PICHA ZOTE/MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Pereira Silima  akiwasilisha azimio la Bunge la Kujiunga na Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Vitendo vya Ugaidi wa Kutumia Nyuklia. Azimio hilo limeungwa mkono leo  katika  mkutano wa kumi kikao cha nane.

Baadhi ya Maafisa Habari Mawasiliano Serikalini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene (wa nne kushoto mstari wa mbele). Wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge leo kuangalia shughuli za Bunge Dodoma.

Baadhi ya Maafisa Habari Mawasiliano Serikalini wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge.

Waziri wa  Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa (kulia) akiongea  na James Mbatia (Kushoto)- katika viwanja vya Bunge leo. Baada ya   Spika Anne Makinda (hayupo pichani), kutangaza rasmi Mitala ya  Elimu inayotumika ni halali na ipo. Katikati  ni Charles Mwijage (Muleba Kaskazini).

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (kushoto), akiteta  Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) ndani  ya ukumbi  wa Bunge.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji  Frederick Werema akisoma Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2012 katika ukumbi wa Bunge leo.

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa  Azzan 'Zungu' akifafanua kanuni mbalimbali  Bungeni leo.

No comments: