Tangazo

February 15, 2013

Picha za matukio mbalimbali ya Mkutano Mkuu wa Wadau wa NSSF unaoendelea jijini Arusha

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akisisitiza jambo mbele ya  Wadau zaidi ya 1000 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa ukiwa ni siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.

Mbunge wa jimbo la Perahamio-Songea,Mh Jenista Mhagama akiomba kupewa ufafanuzi kuhusiana  na Sera na Sheria za fedha ziko salama kiasi gani katika mifuko ya hifadhi ya jamii,kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa ukiwa ni siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Irene Isaka,akifafanua kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo mifuko ya hifadhi ya jamii,ikiwemo sambamba na namna gani inavyoweza kukuza uchumi na kuleta maendeleo makubwa ndani ya jamii.

Mchambuzi Mkuu wa masuala ya Kifedha kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT),Bi.Liku Katekamba akitoa ufafanuzi kuhusiana na usalama wa fedha ndani ya mifuko ya hifadhi ya jamii,na pia amewataka Wanachama kuwa na imani ya mifuko yao ya hifadhi ya jamii.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha mahusiano NSSF,Eunice Chiume  wakati  wa mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa ukiwa ni siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.


Pichani ni sehemu ya Wadau mbalimbali  zaidi ya 1000 waliohudhuria Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa ukiwa ni siku ya pili,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike. Picha kwa hisani ya Matukio-Michuzi

No comments: