Tangazo

February 7, 2013

RAIS KIKWETE ASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Kiongozi  Mhe Fakihi Jundu, Jaji January Msofe, Spika Anne Makinda, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Mathias Chikawe na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Mecky Sadik Februari 6, 2013 baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam. PICHA/IKULU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mchungaji Christopher Mtikila Februari 6, 2013 baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini. Kushoto ni Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman.

Viongozi wa dini ya Kihindu wakielekea kwenye kipaza sauti ili kuomba dua Februari 6, 2013 wakati wa  maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini. Viongozi wa dini za Kiislamu na Kiktristo pia walishiriki kwenye maadhimisho hayo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia  katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa Mahakama ya Rufaa.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

No comments: